Dr Adinan
Member
- Jul 11, 2021
- 14
- 20
Siku moja tukiwa tunaongea na wagonjwa katika mijadala ya kawaida kuhusu kudhibiti kisukari na presha, mgonjwa mmoja aliuliza swali la muhimu sana.
Dr. Mimi nashangaa, ninamuiga mume wangu aina ya vyakula na kiwango lakini yeye ameweza kudhibiti ila mimi siijaweza. Tatizo nini?
Wagonjwa wengi wamekuwa wakiiga tiba ya wenzao au wakati mwengine wagonjwa wa kisukari wamekuwa wakiwapatia wengine tiba zenye manufaa kwao. Hii ni nzuri, wakati mwengine hufanya kazi. Mara nyingi tiba hii haishushi sukari kwa mwengine, haifanyi kazi.
Sababu ya muhimu ni moja. Sababu yenyewe ni rahisi kwelii na huwa tunapenda sana kuitumia kutaoa mfano. Huwa wakati mwengine tunatumia kiganja cha mkono na vidole vyake kufahamisha.
Ushaanza kufahamu? Nakupa hint, mtu huanza hivi, watu ni kama vidole...
Kama vilivyo vidole havilingani.....Ahaaaaa naona umeanza kujibu.... Binadamu pia hawafanani kwa kila kitu. Tunatofautiana. Ndiyo, tuko tofauti. Si unaona hata huazimi suruali kwa kila mtu!
Ndiyo maana dozi ya dawa kwako inaweza kushusha kisukari na kukidhibiti lakini kwa mwingine ikashusha sukari zaidi au isishushe kabisaa.
Kiwango cha chakula unachotumia kinaweza kuwa sawa kwako na kushusha sukari, lakini kwa mwingine kikasababisha sukari ipande.
Sasa toa mkono wako, angalia vidole. Sema haviko sawa. Na sisi hatuko sawa. Hivyo ninahitaji matibabu mahususi kulingana na uhitaji.
Kama umeshaamini hivi, nasi tunaamini hivi hivi ndiyo maana tukasema tukusaidie kudhibiti kisukari kwa ushauri. Tunaendelea pale hospitali ilipoishia. Tunakusindikiza na kubaki nyumbani na wewe!
Fahamu unavyoweza kushusha sukari unapojiunga na MloPlan leo.
Kwahiyo, sababu ingine ya wagonjwa kushindwa kudhibiti kisukari ni kuiga tiba ya wengine.
Endelea kunifuatilia nikupatie dondoo muhimu zitakozokuwezesha kudhibiti na kuepuka madhara ya kisukari.
Unaweza kusoma sabau zingine kwa kubonyeza HAPA
Kumbuka: Fahamu. Fuatilia. Fanya. ili uFurahia