Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Dr. Sajjad Fazel

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
435
421
Habari wakuu,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake.

Karibuni sana.

JamiiImage.jpg

Kama umejibiwa maswali na mtu mwingine na haijakufaa ni kosa lako. Mimi nitajibu maswali zote mwenyewe kama Daktari.

Ugonwa wa Corona (COVID-19)


MPYA: Jinsi ya kujenga kinga ya mwili


Je papai inaweza kuwa na Corona?


Ugonjwa wa Kisukari


Chanjo ya Corona


Kuendelea kupata dondoo za Afya kwa kupitia video, Bofya Hapa: Subscribe
 
Dawa unayoiamini kuwa inatibu kabisa vidonda vya tumbo tafadhari.. hasa home made(mbadala) au yakisasa

Vidonda vya tumbo hutokana na tatizo la acidity. Ni muhimu kujuwa kwanza kama unayo acidity pekee au umeambiwa na daktari kwamba unayo vidonda vya tumbo. Kama unayo vidonda vya tumbo, unaweza kuwa na bakteria ya "H.Pylori". Madawa zake ni tofauti na mtu aliyokua na acidity pekee.

Je uliambiwa nini na daktari?
 
Mm napenda kuuliza swali langu hili.
Jee kuna dawa ambay inaweza kunisaidia kwenye tatiz la U T I maana kiuno kinanisumbua na wakat napima nimeambiw nna U T I .NAOMBA KAMA KUNA DAWA NZUR

U.T.I ni infection ya mirija ya mkojo. kama daktari alikupima na kweli unayo tatizo hilo, Basi nitakushauri hivi:
  1. Dawa Amoxiclav 500mg kutwa mara mbili kwa siku 7. (Hii dawa unaua vimelea na kuondoa maambukizi)
  2. Dawa Cital (Hii dawa itakusaidia kuondoa maumivu kwenye mirija ya kukojoa)
  3. Kunywa maji mengi kama lita 3 au 4 kila siku (unapokunywa maji unapunguza idadi ya vimelea)
Asante
 
mkuu hivi ni kweli kisukari ni ugonjwa ambao unarithi/unakuwepo kwenye ukoo fulani?

Kuna aina mbili ya Kisukari.
Aina ya kwanza ya kisukari (type 1 diabetes) unaweza kurithi. Kama mtu anaugonjwa huu kwenye familia yake basi anaweza kuipata kwa kurithi na ni lazima atunze maisha yake (ulaji bora na mazoezi)

Aina ya pili ya Kisukari (type 2 diabetes) siyo wakurithi. Hilo linatokana na jinsi mtu anavyoishi maisha yake pekee.
 
Naomba kuuliz inawezekan mtu akatumia vidonge vya kutoa mimba na baada ya mda akablidi ila baada cku kadhaa mimba ikawa bado haijatoka??? Msaada please

Niyo inawezekana. Sema haitokei sana. Mara nyingi huwa mimba inatoka lakini pia inakwenda na stage ya mimba iliyofika. Case kama hiyo inatokana mara chache sana. Ni muhimu kama mtu anatatizo hilo akwende kwa daktari wafanye ultrasound kuhakikisha mambo yako sawa.
 
Ninatatizo la meno je ntapata dawa ya kutibu meno

Tatizo aina gani? Meno inauma? Au kuna tatizo na dalili zingine pia?
Mara nyingi dawa inaoitwa "Quadrajel" inasaidia kwasababu inatibu tatizo la vimelea, kuchubuka na kuondoa maumivu. Hii dawa ni yaku pakaa kutwa mara mbili. Lakini ni vizuri ukamuone daktari wa meno ili tatizo ijulikane.
 
Ndugu yangu ana tatizo la watoto kufia tumboni kabla ya kuzaliwa...mimba ikifika miezi tisa unakuta mtoto ameshafariki.. je tatizo hilo afanyeje?? Je anaweza kuzalishwa mapema kabla ya mimba haijafika miezi tisa?? .. Imeshatokea mara mbili... Pia akiwa mjamzito anakosa hamu ya kula..huwa anakula kidogo sana kwa muda wote wa ujauzito..
 
Back
Top Bottom