Mtaalam wa network? Soma hii

Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,289
781
wazo limenijia
Huku shamba kwetu watu wanasumbuka sana na NET, nimewaza kuanzisha huduma ya WI-FI, lakn i know next to nothing kuhusu masuala ya network! wataalam na gurus nisaidieni, ni vitu gani nahitaji na kwa gharama gani ili niweze kuweka net inayopatkana ndani ya eneo la 3-8km radius. Nitafurahi nikipata mchanganuo mzuri na options zilizopo, bila kusahau gharama za hardware na software zote zinazotakikana.
Shukrani mbele wakuu!
 
Ni wazo zuri mkuu,kabla ya kukupa ushauri tungependa kujua nini lengo lako wewe,je ni kuwawezesha wanashamba wako wao kwa wao kuwasiliana kwa kutumia hiyo Wifi (LAN) au wao kuwasiliana na watu wengine walio nje ya huko shambani(WAN). Kwani kila moja ina tofauti zake na gharama zake ingawa moja ni baba wa mwingine(LAN+LAN=WAN)

Nimeanza kwa swali ni kwakuwa kama unataka hii ya pili kuna baadhi ya vitu vitakuwa nje ya uwezo wako hivyo inakulazimu kutegemea miundombinu iliyopo.Kama hii ya kwanza basi huitaji kumtegemea mtu,unaweza kufanya wewe mwenyewe.

Samahani kwa kujibu swali kwa swali.http://www.afroit.com
 
Asante mkuu,
Lengo ni WAN ili wanakijiji tupate net iliyo fast, najua nitahitaji ISP-na kwa huku ni TTCL (labda na wengine kwa kadri wataalamu mtavonishauri) Wanakijiji wanasumbuka sana na vi-dongo vya voda na zain, kukiwa kitu fast najua itasaidia sana. Nachohitaji ni mchanganuao wa hardware na software nazohitaji, na je nitalazimika kulipia "frekwensi"? na mambo yote yanayohusika ningependa kufahamu kwa undani.
Thanksi
 
Kuna jamaa wanatengeneza routers/wireless devices. Wanaitwa MikroTik, networking solutions zao nadhani ni nafuu zaidi compared to others especially for the environment you are describing. Devices zao zinatumia RouterOS, which have built-in support for managing a hotspot, if that is what you need. And of course, you will still need a connection from an ISP to add to your wireless infrastructure for internet connectivity. Check out these guys for the routers, they are listed on MikroTik's website:

ASAA Trading Co., Dar es Salaam, Tel: + 255-22-2121046

Ni authorized distributors wa products za MikroTik/RouterBoard. Then depending na budget yako, contact the major ISPs na angalia options zao zina gharama gani kwa eneo lako.

Check out MikroTik at: MikroTik Routers and Wireless

A list of MikroTik's clients: MikroTik Routers and Wireless
 
Mkuu ushauri binafsi ni kuwa kabla ya kuanza lolote pata kwanza ufafanuzi wa kutosha kuhusu matakwa ya wanashamba,gharama za ISP na mengineyo.Kubwa mno ni ISP kwani wireless is nothing than kufikisha kwenye AP,hivyo kama ISP atasua basi hautafanikisha lengo lako. Nimekukusanyia baadhi ya documents ambazo zitakusaidia katika project yako,Nimejaribu kuupload ila imenitoa so kama vp nitumia e mail yako kwenye PM yangu ili nikutumia.
 
Nadhani kama walisema wataalam wengi juu naomba niongeze kiduchu.
Kwana inabidi ifanyike au ufanye survey ya uhakika kujua au ku project real requirement

  • Je kuna Network yeyote ina exist?

  • Je Ni komytuta ngapi kwenye LAN zinatakiwa kunganishwa kwenye internet
  • Je hizi kompyuta zitakuwa kwenye jengo moja ? ziko majengo tofauti au floor tofauti? Kama ni majengo yako mbali mbali je kuna clear line of sight kati ya jeonga moja na jingine?
  • Watumiaji wa internet watahitaji huduma gan? Kutuma na kusoma email? wanatakiwa waweze kudowload file kubwa mara kwa mara ( Movie, Miziki) Hii itakusaidia kujua Bandwidth utakajohitaji kutoka Kwa ISP.Hii inaweza kukusaidia kujua gharama utakazoitaji kulipa kila mwezi.

Ni maswali kama haya na mengine ndo yatakupa mwanga wa vifaa na gharama ya project yako. eg utajua

  • AP Routers a na switch ngapi utahitaji.

  • Urefu wa UTP cable utakazohitaji kuunganisha kompyuta na switch/router au kama kompyuta zako zitatumia wireless

Kwa hiyo si rahisi kupata mchanganuo sahihi hata wa kukadiria kama baadhi ya vitu kama hivi havijulikani. Kama unataka japo makadirio inabidi wewe uwe surveyor uje na data/picha zaidi wataalam wakusaidie .

Good Luck
 
Mkuu,
lengo ni kuwaunganisha wateja walio sehemu mbalimbali (si LAN ndani ya jengo moja), yaani mtu akiwa na laptop au komputer yake amabayo ni wireless ready akiskan network ndani ya 5km aikute "amoeba network" kisha alogin kwa user name na pswd yake. Wazo ni kutokuwa na limitation ya watu watumie vp (as malipo yatakuwa pay as you go - yaani kwa mb).
Asante
 
Kutokana na ukubwa wa eneo unalotaka kulihudumia labda pia ungeuliza gov ina restrictions gani.
Kuhusu system gani itakufaa zipo nyingi sana kutokana na maeneo ya sehemu husika milima/ mabonde / tambalale nk. Jaribu hawa jamaa wanaitwa "Ayrstone AyrMesh" System zao zipo simple kuinstall na ku-manage halafu siyo ghari vile kulinganisha na wireless infrastructures zingine eg cisco gears. www.ayrstone.com wana mfano wa wireless networking. angalia ona kama itakufaaa.
 
kama nimekupata na kuna mtaalam kilongwe kakueleza nadhani kazi uliyonayo ni kuongea na ISPs Wako wengi Bongo Simbanet,Africaonline,Satcom,TTCL, etc. It sound to me na kwa jinsi ulivyosema kufikisha internet kwako hapo satelite inaweza kuwa ni suluhisho zuri.

Kama alivyosema mtaalam 1ja. ikifanyika hiyo sana sana kitakachobaki ni kuweka AP (Access Point) katika center position ya eneo unalotaka. Na ili kungeza siganal quality and strength kwa wateja utahitaji Omni directional Antena kuyapa nguvu mawimbi yayotoka na kwenda ndani ya AP husika

Kuna Acess Point za breezenet 2.5 MgHz. zinafanya kazi kwenye unlicenced frequency. Nadhani kwa sasa kuna product nyingi lakini by the time napiga piga mzigo breezenet was the best.
 
Naomba kuongezea japo kwa ufupi

Kwa jinsi nilivyokuelewa kwa ukubwa wa eneo uliloweka(3-4km) basi moja kwa moja kwa jinsi ninavyoona unataka uwe sub ISP...

ok mchanganuo usio rasmi ni huu hapa kwa mawazo yangu:

NB: hapa ni mbali ya mahitaji usika na mahitaji ya watu hapa naongelea roughly technical installation

Kwanza kabisa tukichukulia kwa eneo lenye ukubwa wa 4km ... kitu kitakachokupunguzia gharama na kuweza kukupa huduma stahiki (avalailability,reachability and flexibility of services ) ni kuweza kutengeneza Mfumo mzima wa mawasiliano ujulikanao kwa jina la MESH....

MESH: ni aina ya network system Implementation ambayo vifaa vyote vya mawasiliano vinakuwa vinawasiliana in a randomly way( kwa lugha nyepesi ni kuwa kwa kila kifaa kimoja kinawasiliana na vifaa vyote vyilivyopo katika njia tofauti

mfano kwa eneo lako mathalani tuchukulie kuwa utaweka POP(point of presence) /AP kama sita(6), device ya kwanza inatakiwa iwe na connection kwa kila devices tano zilizobaki... na vivyo hivyo kwa device zingine ili kuweza ku eliminate Downtime ya eneo fulani kama kuna failover itakayotokea(redundancy guaranteed)

Kingine unachotakiwa ni kuwa na kitu tunaita NOC(network operation Centre).. hapa ndipo patakuwa central point ya system yako) kwa maana ikiwa utaamua kuchukua connection kutoka TTCL(which is inevitable hence their have DSL option kwani provide local wengine itabidi uwe na point to point connection ambayo itakuwa gharama zaidi na kwa mji unaotanuka inaweza ikaleta shida ikiwa kutatokea barries zozote katikati na hasa kama hauko katika urban areas )

Kuna vendors wengi wa wireless device ambao wanauza device zao kwa gharama nafuu na ni durable (all wether devices)... mfano.. airmax , senao, skypilot na nyingine nyingi( almost usd 150 to usd 200 per device)... na device hizi zinapatikana kwenye FR tofauti lakini FR amabazo ni free licence ni za 2.45 pamoja na 5.xxx(sikumbuki) na hasa ni nafuu pia kwa end user... kwa backbone yako unaweza ukatumia frequency nyingine hata za kulipia kuepusha interference

NB: kitu cha kuangalia ni kuwa usikimbilie unafuu tu hasa kwa zile Backbone devices kwani moja kati ya shida wanazopata ma ISP wetu ni tatizo la hali ya hewa ambalo lina haribu sana device zetu (HALI ya Joto) device inachemka na matokeo ya ke inafail

hakikisha kwa ufanisi zaidi Cell-sites zako ziwe zina redundancy connection na power backup
 
Back
Top Bottom