Mtaa wa kwa Kindande Temeke visa vyake

We mtoto wa Kota nyamaza!!

Unajiita Da Hustla halafu unaogopa watu wenye nyembe mfukoni!!! Watu hadi kesho wanatembea na full-loaded gun, na ukimzingua anaku-shoot, unakuja kuogopa kisu halafu bado unajiita Da Hustla!!!
We unafikiri kuwa Hustla ni kuwa msela mavi au ku-hustle ki old school hivo na mambo ya bisi bisi,wembe na mapanga...watu wana hustle kwa kutumia brains sio kwa kutumia hayo mataka taka,na ndo tofauti kati ya watoto wa mjini kinondoni(sio ile ya uswazi) na huko swekeni sijui tandika ,temeke,tandale ,mwananyamala etc
 
Wa kuja wewe!!!
 
Utakuwa wa kuja wewe, Dar ukafikia kota!!!

Huwezi kuwa husler halafu ukaogopa life la mtaa la kwa sababu hata ukitumia brain, kwenye hustling utazinguana tu na watu!!

Au mtoto wa kishua hujui nini maana ya hustle?!!
 
Du mimi nilizani blazili ya kinondoni mosco ndo balaa kumbe kuna kiboko yake
 
Kama ndo hivo mbona Dar kwa kipuuzi sasa kama izo fleva zenye?
 
Kama ndo hivo mbona Dar kwa kipuuzi sasa kama izo fleva zenye?
Sasa ukienda Arusha halafu ukakutana na Mdundiko huwezi kujiuliza mdundiko na Arusha wapi na wapi?!

Miaka kadhaa iliyopita nilitembelewa na mshikaji wangu mmoja... foreigner!

Nilivyokuwa boya wakati ule, eti siku ya kwanza kumtembeza nikampeleka city kumuonesha "tulivyo na bonge la jiji" wakati anakotoka, hizi flyovers zinazoshabikiwa leo Dar kule kwao zilijengwa hata kabla hajazaliwa!!!

Tena nakumbuka tumefika pande za Gymkhana jamaa akaonesha wazi kwamba ameboreka na ile tour, na akaja ku-enjoy siku ya pili yake tulivyoenda Mafia!!!

Nilijiona boya ile mbaya!!

So, YES, hizo ndo flavor za Dar labda siku nitembelewe na Msukuma ndipo nitampeleka akaangalie flavor za Kisukuma Sukuma kama vile Mabugando n.k 😀🤣😅!!

Wasukuma msini-mind, nawatania tu!!
 
Hebu toa maelekezo vizuri,hao single mother nna jambo nao
 
Mwanzoni miaka ya 2000 nliiingia dar kwa Mara ya kwanza, mzee aliniacha kijijini kuja kufight maisha jijini alipokaa sawa kidogo mwamba nikapata nafasi ya kuingia town!

Vingunguti kwa mnyamani ndio mzee alikaa miaka hiyo.

Ile napanda dala dala pale kiembe mbuzi niingie tuition chaaap wahuni wamepita na wallet [emoji23] nafika karume Sina hata mia na simu Sina. Taabu niliyopata siku hiyo acha na vile nilikua ndio nimeingia mjini ilikua balaaa.

Nilifanikiwa kurudi jioni Nikamwambia mzee, akaniambia changamka wewe mjini hapa, akanichukua tukaenda vichochoro kwa vichochoro aisee, yaani matusi matusi tu, uhuni uhuni, bangi bangi, gongo gongo, umalaya umalaya, mchanganyiko wa hatari, mzee ananiambia mwanaume lazima ujue kuishi mazingira yote,

Hatumaye tukafika kwa hao mateja, nashangaa wanamuamkia mzee kwa heshima kabisa Ila wamechoka kinyama. Baada ya salamu mzee akawaambia nimekuja kumtambulisha mdogo wenu, wahuni walifurahi kinyama, wananipa ushauri niwe makini kitaa nisije kuwa Kama wao na vitu vingine positive, nikaanza kubadili mtazamo wangu juu yao, nikaona kumbe wale ni wagonjwa Kama wagonjwa wengine, ni wahanga tu wa maswaibu ya dunia.

Akawaambia mmepiga asubuhi kawallet na kasimu kake wakaomba msamaha pale, Ila walishauza muda huo. Mzee akawapa buku tukasepa.

Leo ni mwaka wa kumi na nane Niko town sijawahi pata shida na vijana wenzangu nilijifunza jinsi ya kuishi nao.

MEISHO.
WAO NI WAHANGA WA MASWAIBU YA DUNIA TUJIFUNZE KUISHI NAO NA TUKIWEZA TUWASAIDIE.
 
Wahuni wana utu sana ukienda nao sawa, halafu huwa wanahitaji vitu vidogo vidogo sana, ukiwaelewa tu unaishi kibosi sana hata ulinzi wanakupatia. ukijifanya huwajui hiyo mitaa utapata taabu sana
 
Duh
 
So wazawa wote wapo uswahilini?
Hakuna mzawa anayekaa ushuani anayeweza kushangaa au kuponda Uswahili wa Dar es salaam kwa sababu bado atakuwa na ndugu wa kutosha huku Uswahilini, na maisha ya Kiswahili yataendelea kuwa sehemu ya maisha yake!!!
 
Hakuna mzawa anayekaa ushuani anayeweza kushangaa au kuponda Uswahili wa Dar es salaam kwa sababu bado atakuwa na ndugu wa kutosha huku Uswahilini, na maisha ya Kiswahili yataendelea kuwa sehemu ya maisha yake!!!
Basi sawa
 
mdogo wangu pole sana ila shukuru mungu tu sasa hivi huko ndio kumepoa sna, way back mitaa ya huko ulikuwa huoni hata kuku kufugwa, familis nyingi zilihalibika , watoto walikuwa wezi hatari danger zone za way back " stombagi" plus na talban camp hapo mbele ya makaburi kuelekea raha leo, " teqwin" " kwa mayawa a k.a santamigo" kwa keni" damu ya simba , from 2003 kurudi nyuma aisee ilikuwa mbaya kupitiliza coz sisi tumeishi hyo mitaa
 
Uswahilin kuna vituko sana picha linaanza tu kwanza demu anakuja kukutongoza mwenyewe alafu kibabe huku anakuchamba kinyama ukimkataa visa vyake utahama mtaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…