Naunga mkono jamaa wa asili ya bara -asia ni sehemu ya Tanzania. Ndio makuli waliojenga reli ya kati na mishahara yao ndio wakajenga hayo maghorofa tuliyokuja kuwapora.
Kisutu ni eneo kubwa lenye mitaa lukuki hivyo huo mtaa mmoja kupewa jina la kihindi its fare. Majina ya wakoloni wazungu bado yako kibao. Mitaa kibao kwenye pwani ya makombe (oyter-bay ni ya kizungu.
Mtaa wa heshima ya Uhuru, Independence ukaitwa Samora,majina ya maeneo kibao ni ya wazalendo ama ya kizalendo. msasani ni kwa Mzee Mussa Hasani, kulikuwa na bonde la mpunga, wamakonde wakashindwa kutamka Musa Hasani, wakaita Mcha Achani hatimaye Msasani. Mikocheni ni kwenye pori la miti ya mikoche. magomeni kwenye malundo ya magome ya miti barabarani. sambamba na baadhi ya mikoa, Dodoma, Idodomya, alipozama tembo kwenye tope. tabora, ni Matobolwa
.waacheni jamaa zetu wapate mitaa ya majina yao.