Mtaa maarufu Dar wabadilishwa jina!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtaa maarufu Dar wabadilishwa jina!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tusker Bariiiidi, Apr 3, 2009.

 1. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Wakati baadhi ya Mashujaa wetu ambao wamechangia taifa letu la Tanzania kabla na baada ya uhuru hatuwaenzi ama tumewasahau kabisa... Mtaa mmoja maarufu sana hapa Dar es Salaam uitwao Kisutu ambao unaanzia Makutano ya Zanaki Freedom Electronics au Neha Batteries na Upanga/Ally Hassan Mwinyi (Haidery Plaza) umebadilishwa jina unaitwa Pramukh Swami Street Swali langu ni je
  • Kwanini?
   • Maana yake ni nini?
    • Kwa ruhusa ya nani?
     • Na kuna ulazima gani ?
  Juzi kuna watu wasiojulikana walijaribu kufuta jina hilo kwa kulimwagia rangi nyeusi lakini sijui iliishia wapi???
   
 2. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwani Kisutu maana yake nini? Huu mtaa wakazi wake wengi wana asili ya Asia kwa hiyo ni vyema jina lika-reflect ukweli huo. Mbona tulipowanyang'anya shule zao, walizojenga wenyewe halafu tukayapa majina ya kimatumbi ( Jangwani, Azania, Tambaza n.k.) hawakulalamika? Wakati umefika wa kuwatambua kuwa nao ni sehemu ya jamii yetu kama wewe na mimi! Unaweza kukuta hata hili jina ndilo jina la asili la mtaa huo. Kwa wale tunaokumbuka Kisutu halisi (pembeni mwa Central Library) ilikuwaje wala hili halitupi taabu.

  Amandla......
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Mkuu Tusker Bariiiidi heshima mbele.

  Tanzania yote yanawezekana kama tumewapa (binafsisha / genisha)wageni viwanda,Dhahabu,Tanzanite,Almasi na rasilimali zetu zote wewe unashangaa nini mtaa kuadilishwa jina.

  Haya ni matokeo ya kukubali kuendelea kutawaliwa na watu walioksa dira.Leo wameanza kubadili majina bila aibu tukikubali kesho watatupangia hata sehemu za kupita.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mnh... :(
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Aliwahi kuulizwa swali kama hilo bwana mmoja sina uhakika ni nani katika manispaa, maelezo yake yaliniridhisha. Ni kwamba majina ya kila mtaa huchaguliwa na wakazi wa mtaa husika kwa kupitia serikali zao za mitaa. Na hii haibagui hilo jina ni la asili gani iwe sea view, mtogole au hata Pramukh Swami ili mradi ni chaguo lao. Sasa kwa kuzingatia idadi ya watanzania waasia wanaokaa eneo hilo nadhani jina hilo ni sawa tu.
   
 6. Oloronyo

  Oloronyo Member

  #6
  Apr 3, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maana halisi ya jina la mtaa huo Shastri Nārāyanswarupdās (December 7, 1921), commonly known as Pramukh Swāmi Maharaj, is a Hindu sadhu, Indian social worker, and spiritual Guru of an international Hindu organization known as the BAPS Swāminārāyan Sansthā (Bochasanwasi Akshar Purushottam Swaminarayan Sanstha). His life work primarily revolves around teaching principles of bhakti yoga, self-realization, and service to society as taught by Bhagwan Swaminarayan.
  The followers of Pramukh Swami Maharaj believe that he is the fifth spiritual successor of the Bochanwasi Akshar Purushottam Sanstha. Presently, Pramukh Swami is the leader of Bochasanwasi Shri Akshar Purushottam Sanstha.
  Birth: 7 December 1921; Magshar Sud 8, VS 1978.
  Birthplace: Chansad, Gujarat.
  Initiation: 10 January 1940; Posh Sud 1, VS 1996.
  Guru: Brahmaswarup Shastriji Maharaj, Brahmaswarup Yogiji Maharaj
  Spiritual Head Since: 23 January 1971; Posh Vad 11, VS 2027.
  Villages Visited: Over 15,500.
  Countries Visited: Over 50.
  Homes Sanctified: Over 250,000.
  Letters Read & Replied: Over 500,000.
  Personally Counseled & Comforted: Over 810,000 people.
  Discourses Delivered: Over 20,000.
  Mandirs Built & Consecrated: 713.
  Sadhu Disciples: Over 800.
  Guinness Book of World Record holder: Largest Hindu Temple in the World called Akshardham [1]
  Guinness Book of World Records holder: Only Person in the World to consecrate 713 Temples in 5 Continents between April 1971 to November 2007
   
 7. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2009
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  tatizo sio jina,
  Ila KWANINI ubadilishwe jina,
  Haya mambo inabidi yafanyike kwa uwazi,
  Otherwise unakaribisha utata na maswali lukuki.
   
 8. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Uwazi upi unaouzungumzia ndugu?kama kibao cha jina si kimebandikwa? na taratibu za kubadili zilifanyika tena zikawahusisha wa kazi wa eneo hilo na kama wewe ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo utakuwa ni miongoni mwa wale wasio hudhuria mikutano ya mitaa.
   
 9. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Kwa wale tunaokumbuka Kisutu halisi (pembeni mwa Central Library) ilikuwaje wala hili halitupi taabu.

  Kwangu mimi ni sawa na mtu aseme baada ya miaka 20 ijayo kuwa
  Kwani Msasani ni nini?? Wakati huo pamevunjwa pote na watu wamelipwa fidia tunaokumbuka Msasani halisi( Nyuma ya Namanga) ilikuwaje wala halitupi taabu.
  Wakati huo Barabara ya Msasani inayopita Oysterbay imebatizwa jina inaitwa King George OBE Street.
  Nawasilisha!
   
 10. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  The followers of Pramukh Swami Maharaj believe that he is the fifth spiritual successor of the Bochanwasi Akshar Purushottam Sanstha. Presently, Pramukh Swami is the leader of Bochasanwasi Shri Akshar Purushottam Sanstha.

  Kama ni hivyo basi Mtaa wa Kivukoni unaopita mbele ya Kanisa la Azania Front uitwe Martin Luther,ule wa Sokoine unaopita mbele ya Saint Joseph uitwe Pope John Paul au St.Joseph.
  Nawasilisha!
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwani Kisutu ndiyo jina lake la asili? Kabla yake mtaa ulikuwa unaitwa nini? Mimi shule ya Kisutu naikumbuka kwa jina la D.A girls! D.A. ilitokea wapi? Nakumbuka wakati jina la shule linabadilishwa kuwa Kisutu watu wengi walilalamika kuwa association yeyote na eneo la Kisutu itawaharibia sifa wanafunzi wa shule hiyo! Leo mnatetea jina hilo? Iko kazi.

  Amandla.......
   
 12. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Hivi karibuni utasikia Mtaa wa Zanaki nao utaitwa Bochasanwasi Shri Akshar Purushottam Sanstha Street
  Karibu sana Fundi Mchundo.
   
 13. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwani tatizo liko wapi? Kwani jina la Zanaki linatokea wapi? Au kwa vile baba wa taifa alikuwa mzanaki ikawa nongwa?

  Asante kwa kunikaribisha, Mkuu.

  Amandla.........
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Kama wewe ni mkazi wa maeneo hayo uliyoyataja nenda washawishi na wakazi wenzako kisha mpeleke ombi lenu kwenye serikali ya mtaa wenu na jina litabadilishwa tu, acha kulalamika chukua hatua.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Naona hukuijua Kisutu original!
  Mimi nakataa hiki kitabia cha kujifanya tunaenzi jina kumbe tuna kiajenda kasiri. Hii nchi ni yetu wote, wamatumbi, wahindi na wazungu. Kama wakazi wa eneo la Msasani wa wakati huo wakiamua kupaita King George OBE Street kuna ubaya gani? Mbona majina mazuri tu ya mitaa ( Bagamoyo rd, Kilwa rd, Upanga rd, Pugu rd n.k.) tumeyabadilisha kutokana na sababu za kisiasa! Leo wakaazi kutaka jina liwa-reflect imekuwa nongwa?

  Amandla....
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  acha kutetea ujinga. when u go to rome do like romans. hawana sababu ya msingi ya kuita jina wanalopenda. mbona pretoria wanataka kuibadili na kuiita jina la kisauz?
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Fundi, List haiishii kwenye mitaa tu, inaenda hadi kwenye majengo, mashule na viwanja vya ndege. Nadhani tutaelewa tu pale tutakapoanza kuwa na "China Towns" katika baadhi ya mikoa (minamo karne hizo). Pale tunapowaenzi wanasiana, tena wabadhirifu kwa vigezo visivyoeleweka ua kukubalika, au kwa lengo la kuwatunuku tu; vivyo hivyo tutakavyowakubalia wowote wale popote pale watakaokuwa na lengo la kubadili majina halisi ya sehemu zao kwa makubaliano yao wenyewe.
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Jina la kisauz ndiyo lipi? Mbona huko huko Sauz mpaka leo wana nyimbo za taifa mbili? Na hilo la Pretoria mbona wameshindwa kubadili? Kwenye sheria hatulazimishi kitu. Kama alivyosema mwenzangu, tuanze kujihusisha na mambo ya jamii. Twende kwenye mikutano. Tusome magazeti. haya ya kulalamika after the fact hakutatufikisha mbali.

  Amandla....
   
 19. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mziwanda, sababu zake za kutetea amezitoa nami kama yeye sioni kama anachotetea kuwa ni ujinga. Bali maelezo yanaoonesha ukweli wa mambo kuwa, pale tunapokubali Mafuta house kubadili jina, au Old Bagamoyo Rd kuitwa jina jingine, ni criteria gani zinafuatwa mpaka mabadiliko hayo yanakubaliwa as opposed kwa kubalishwa jina la huo mtaa hivi karibuni?
   
 20. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa mmoja alipobadilisha jina la mtaa kumuenzi baba yake alisema alifanya hivyo kwa sababu baba yake alikuwa mwafrika wa kwanza kuwa na redio! Hawa si angalau wanamuenzi kiongozi wao wa dini!

  Amandla.......
   
Loading...