Kwa kweli msuya amekosea sana kutoa hiyo kauli kwa sababu kwa yeye kuwa waziri mkuu katika moja ya tawala za nchi hii ni wazi kwamba hawezi kutenganishwa na matatizo lukuki yanoikumba nchi yetu tangu mwaka 1961.

Alipaswa yeye binafsi akiri makosa yake aliyotenda wakati akiwa mtawala then atuombe radhi, baada ya hapo ndio akituhumu na chama chake na serikali ya JK. Vingenevyo atakuwa amekengeuka.
Wewe vipi bwana? Msuya wakati wao walihakikisha nchi ina umeme unaolingana au kuzidi kidogo na matumizi ya nchi. Sasa tuwaulinze ni mradi gani serikali za awamu zote tatu baada ya ile ya kwanza umejengwa? hamkujua mahitaji yanaongezeka? hamkujua vyanzo hivyo vinazidi kupungua uwezo ama kwa mitambo kuchakaa au mabwawa kudhofishwa na siltation process.

Ni upumbavu na ujinga kuhalalisha matatizo ya leo eti kwa sababu historia ya nchi imepinda. Kwani muliomba uongozi mkawafanyie nini Watanzania kama si pamoja na kurekebisha yale ambayo awamu zingine hazikufanikiwa kurekebisha au kuyafanya vizuri.

Kwa kweli niliwahi kusikia kiongozi mmoja akisema wenzake wote waliomtangulia hawakuyamaliza matatizo ya watanzania na kwamba na yeye kipindi chake kitapita atakuja mwingine maana yake eti matatizo haya hayatakwisha nilisikitika sana na kwa kufikiri kwangu nilihisi kiongozi yule alighafirika na kwamba ipo siku atawaomba msamaha wananchi. Kwa kifupi historia ya nchi inatusaidia kuindaa nchi kukabili chanagamoto za sasa. hatuwezi kuwalaumu wenzetu waliotutangulia kwa kushindwa kufikia malengo yao au kufikia matumaini yetu. Lakini tutawalaumu pale tu ambapo rasilimali tulizowakabidhi hazikutumika ipasavyo katika kusaidia kuleta maendeleo ya Mtanzania.

Hivi Nyerere angekuwa mlafi na rasilimali asilia za nchi hii katika kipindi cha miaka 25 awamu zilifuata baada yake zingekuwa zinategemea nini? Kama unachimba madini huwezi kujenga miundo mbinu ya kuzalisha umeme uweze kuwauzia majirani zako unategemea nini kama si kuiletea umasikini.
Unawezaje kuuza nyumba ya urithi na usijenge ingine, unawezaje kuuza nyumba uliyojenga na pesa zake ukazitumbua. Ndugu watanzania huko ni kuleta umaskini. Msuya aliyefunguka macho na masikio na kuamua kusimama kidete leo kutoa kauli zinazoitayarisha serikali kujirekebisha ni bora kuliko mamuliki 100 wanaonyamaza nyuma ya blanketi la UCCM. Mkapa, Mwinyi, na wengineo wafanye hima kuongoza msimamo bora wa kuishauri serikali ifanye hima kurebisha kero hizi namshukuru Msuya na kuwakemea wote watakao ona mzee huyo amekosea leo.