MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,238
- 50,413
Video hapa inaeleza Mozambique wanawasaka Watanzania na kuwanyan'ganya kila kitu, huku wakiwapiga na kubaka wanawake zao. Hata ukiwa na kibali wanachana na kunyakua kila ulicho nacho, simu, hela na kipigo.
Sielewi mbona wameingiwa na wazimu wa namna hiyo ghafla, na je wanalenga Watanzania tu au hata na Wakenya pia? Ubalozi wa Kenya utoe tamko nini hatima ya raia wetu maana hii ni hatari. Afrika leo hii imeingiwa na kichaa, hamna cha undugu wala nini, mzungu alituchorea mipaka na kutuambia tubaguane kwa misingi ya hiyo mipaka.
Hawa Msumbiji kuna historia ipo kwamba Watanzania wengi walimwaga damu wakati wa kuwasaidia kupata uhuru. Hayo yote hawayajui, ila kama jinsi huwa nasema siku zote, kuna vijana wa leo kwenye hizi nchi ambao hawana ajira na hawajui hizo historia za Afrika.
Kule Afrika Kusini kuna vijana hata hawajui Mandela alipigania kitu gani, maana ufisadi wanauona tena ukifanywa na akina Zuma ilihali wao maskni na njaa tupu, hivyo huwa wanakurupuka na kufukuza wageni kama mbwa.