Noel Shao
Member
- Jan 19, 2017
- 89
- 185
HISTORIA ITAZAMWE SAKATA LA KUWAFUKUZA WATANZANIA HUKO MSUMBIJI..
NA: Noel C Shao
Huwezi taja historia ya Msumbiji bila kuitaja Tanzania, kadhalika South Africa, Angola, n.k jina Tanzania lazima litachomoza katka historia za mataifa hayo. Kwa kuwa kitovu na vuguvugu la kupambana na ukoloni katika nchi zao ulianzia hapa Tanzania. Hata Joaquim Chissano, Armando Guebuza, Samora Machel wanajua haya.
Walipanga mipango yao hapa, walilala kwetu, walikula Tanzania, walisoma hapa, n.k
Tukifanya hayo tulisukumwa na utu, tukaweka udugu mbele, n.k tuliamini Afrika moja ni Afrika HURU. Na sote ni wamoja. Uhuru ulipatikana na historia kuandikwa.
Je kinacho endelea, kuwafukuza Watanzania wanaoishi msumbiji ni sawa au siyo sawa?
Majibu yote yanaweza kuwa sawa. Suala la mtu kuishi katika njia nyingine bila kibali ni kinyume cha Sheria. Na Kama ni nje ya utaratibu wa Sheria za nchi hiyo lazima waisimamie Sheria.
Naunga mkono kwa asilimia 100% kuwaondoa watu wasio na vibali katika nchi yoyote. Na katika kutekeleza hilo ni vema hisia zikawekwa pembeni na sheria kufuatwa. Hata hapa kwetu hatupaswi kuona kuna huruma kwa wahamiaji haramu na Wao wanao ishi bila vibali. Wapo maeneo mengi, hatupaswi kuwahifadhi, yafaa waondolewe kwa kufuata utaratibu. Hawa wana gharama nyingi hasa kiuchumi na kiusalama.
Donald Trump alipo ingia madarakani aliwafukuza wakenya na wasudani waliokuwa wanaishi Marekani kinyume na Sheria. Kadhalika kuwaondoa wahamiaji haramu.
Cha msingi alicho Fanya Trump na wanacho takiwa kufanya mamlaka ya msumbiji ni Kutazama Utu. Wangewapa muda wa kuondoka, kuondoa vitu vyao, kuhamisha fedha na familia zao. Si kuwaondoa mithili ya magaidi, na kuwatesa kama mateka wa vita.
Wanacho kifanya msumbiji ni mfano wa mtu unayesumbiliwa na panya ndani ya nyumba na kuamua kutumia shoka kuwauwa! Wenye akili timamu wakikukuta msaada watakao kupa ni kukupeleka hospitali kwa matibabu ya akili.
Msumbiji, Wangetaza nyuma, wangeangalia historia, mchango tuliowapatiwa hadi kujipatia Uhuru wao. Damu za watanzania zilimwagika kwa ajili yao, tulihifadhi uhai wao na mengine mengi.
Hawakupaswa kusahau historia hii, yamkini rais Felipe Jucinto Nyusi kaamua kuiuza historia hiyo. Au Ana makusudi ya kufanya hivyo. Madhara yake ni makubwa hasa kutia doa uhusiano wa kidiplomasia. Inakuwaje Tanzania nasi tukafanya kama wanayo Fanya? Kenya wakafanya hivyo, south Africa nao vile vile, Tukazoana kama wanyang'anyi na wahalifu sugu?? Tutakuwa tuna jenga au kuzidi kumeguwa historia ya Afrika?
Afrika ni mama katika tumbo moja, wote ni wamoja, tunatenganishwa na mipaka tu. Lakini letu moja, tumeshiriki tamaduni moja, historia yetu haipishani. Kuendelea kutafutana hakuwezi kuwa suluhu ya matatizo tuliyo nayo .
Sheria ni Sheria, ukivunja Sheria sharti uadhibiwe kwa Sheria, ila wakati mwingine Sheria hizo hupindishwa kwa busara na hekima kwa maslai ya utu na ubinadamu.
Noel C S.