MSUMBIJI: Mwanamke wa Kitanzania abakwa mpaka kufa. Serikali imefungwa plasta?

Kwa utaratibu unapoenda kuishi nchi yeyote ya nje unatakiwa kwenda kwenye ubalozi wa Tanzania wakutambue ili iwe rahisi kwa kutoa msaada. Unakuta watu wanaejiendea tu mahali bila ya utaratibu yakitokea matatizo mnataka serikali i act. Ni jambo baya linalofanyika msumbiji lakini kuitupia lawama serikali moja kwa moja ni upuuzi na kukosa akili. Hili suala ni gumu kulikurupikia tu moja kwa moja.
 
Nadhani kuna nyuzi zipo ambazo zinazo ongerea matatizo ya balozi zetu.
Balozi zetu kiujumla hazina misaada kwa raia, nadhani zipo kwa ajili ya mahusiano ya kibiashara baina ya nchi na nchi.
Imekuwa kawaida askari wa msumbiji kupora na kuwatia mahabusu raia wa tanzania na ni kawaida kwa askari wa msumbiji kuto kuheshimu utu wa mtu. na kesi/ malalamiko haya ukiyafikisha ubalozini itanibezwa na kuonekana wewe ni kioja.
Kuna la kujifunza kutoka kwa nchi kama Nigeria inajali raia wake. Tukubali, tusikubali, angekuwepo Baba wa taifa ili swala lisingefikia hatua hii. Viongozi wamekosa uzalendo, kwao ni bora uhusiano wa kidiplosia zaidi kuliko utu wa mtanzania.
Tunaomba maafisa wa kibalozi muliopo kwenye ofisi za kibalozi nje ya mubadilike, mjue mko hapo kwa ajili ya kuwatumikia watanzania, bila ubaguzi wa kikabila,kikanda, na kidini. Fanyeni kazi kwa kuwatumikia watanzania, sio wote watanzania waishio nje ya nchi wanafanya uharifu.
Binafsi namshukuru mkurugenzi wa uhamiaji mtwara, mhagama kufatilia na kutoa taarifa za swala zima linaendelea, ambao balozi wetu msumbiji limemshinda. Hii inaonyesha kwa jinsi gani balozi zetu ziko weak.
 
unaishi wapi wewe rais ameshatoa amri raia walioko nje ya nchi kama wana makosa wasitetewe waache wanyongwe....huyo atakaewatetea unataka atumbuliwe?
Unaleta uchochezi, Rais alisema endapo hao watanzania watabainika wamejihusisha na madawa ya kulevya.Unapata faida gani kuongea uongo hapa?
 
Najuta hata kusoma huu uzi maana roho inaniuma kama kidonda kibichi, halafu kwanini kila siku ni waTZ tu ndio tunaonewa na majirani zetu halafu hawa wakuu wetu huwa wanaona aibu kutetea watu wao. ina uma aaaaaaaaaa basi tu
 
Habari Jf

Jamani, Hii inasikitisha sana tangu kuanza kusikika kwa sakata la watanzania kufurushwa uko msumbiji mengi yametokea lakini serikali yetu inaonesha kuwakandamiza watanzania kuwaonesha hawakuwa wakiish kihalali kabisa.

Okay Yote sawa mtu kwao lakini serikali ya msumbiji inafata utaratbu kuwarudsha watanzania?

Je, sisi huwa tunavunja sheria kuwarudsha kistarabu??

Maofisa wa msumbiji wamekuwa wakifanya vitendo vya kikatili ikiwemo kuwapora mali zao, pesa, na hati za kusafiria.

Sikuridhika nliamua kufunga safari kwenda mtwara kuonana na wahanga.

Katika yote kilichoniumiza nlipofanya mahojiano na mwanamke ambaye rafiki yake kutoka Morogoro alokuwa akiishi Msumbiji kubakwa na maofisa wa Msumbiji mpaka kufa akiwa anawahishwa hospital huko Msumbiji.

Tukio hilo liltokea usiku maofisa hao walivamia nyumba ya huyo mdada kisha kumbaka kwa zamu hatimaye akawa na hali mbaya hadi anakuja kupata msaada kupelekwa hospitali hali yake ilikuwa mbaya sana na kufariki dunia

Je, serikali hawajui haya? Mbona hawazungumzii lolote?
Kwanini wanaishia kuwakandamiza watanzania na kuwaonesha dunia watanzania wale hawakufata sheria?

Nimeweza kuona vibali vya wengine walofankiwa kurudi navyo vibali vya kuishi na kufanyia kazi lakini bado wamewafurusha.

Kama sheria hao wote wamevunja sheria za ukaazi?

Yupo mwingine ambaye alikuwa akiishi na mkewe na mtoto na mkewe ni mjamzito lakini alipohitaji kurudi na mkewe Tanzania maofisa wa Msumbiji walimkatalia.Je, sheria ipi inayoruhusu hayo??

Mbona wao wanarudishwa na familia zao ikiwa wamekuja nazo?

Serikali ya Tz inawaogopa Msumbiji kutetea Raia wao?

Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi alizaliwa Tanzania na kusoma Tunduru na kupata mafunzo ya kijeshi hapa Tanzania.

Lakini watu hawa ambao wamesaidiwa na Tanzania wameshindwa kuagiza vikosi vyao wawarudishe kistarabu na kufata utaratbu bila kuvunja sheria?

Vipi wawafukuze kama Mbwa? Wamewafunga mahabusu bila kuwapa chakula siku tatu.

Wakawapakiza kwenye malori bila ya chakula wala mali zao.

Inasikitisha Mtanzania mwenzetu anabakwa mpaka kufa serikali haina inalosema?

Tuna serikali tuna majanga?

Wenzetu raia wao akiguswa tu hadi Rais wa nchi ataongea.

Sisi mbona hawathamini watanzania na kuwaonesha dunai raia wa Kitanzania wana makosa?

Hakuna ofisa wa Msumbiji alochukuliwa sheria mpaka sasa kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ndani ya Msumbiji.

Ofisa mmoja ambaye mama yake ni mtanzania na baba yake ni Msumbiji ameambia chanzo chetu kawaida na maofisa wa Msumbiji hufanya vitendo vya kikatili kwa wageni.

Ameongeza na kusema kuwa tatizo mabalozi wa Tanzania pia sio wakali kutetea raia wao bali kuwakandamiza.

Anazidi kusema kuwa anaumia sana kuona watanzania wenzake kwa wanayofanyiwa lakini hana mamlaka ya kuweza kuzuia.

Amethibitisha pia kuwa ni kweli mwanamke huyo wa kitanzania alibakwa na maofisa wa Msumbiji wapatao sita hadi saba kwa uchunguzi wake.

Jamani tuungane tusaidie wenzetu lazima tujifunze kupendana serikali inahisi hawa watu sijui manyani sijui sio raia wao nashindwa kuelewa.
Sio kama naunga mkono matukio hayo (kama kweli yametokea), lakini naamini serikali ina uwezo mkubwa zaidi wa kupata taarifa sahihi. Haya mambo ya diplomasia(hasa kwa nchi tunazopakana nazo) yanatakiwa kuangaliwa kwa umakini sana.Serikali makini haiwezi kufanya maamuzi kwa kutegemea habari za mitandaoni bila kuzichunguza na kuzithibitisha. Watanzania inatakiwa tujue kwamba serikali ipo macho wakati wote, hata kama inaonekana haijasema lolote, lakini inafanya kazi usiku na mchana. Kuna baadhi ya hatua zinazochukuliwa na serikali huwa haziwekwi hadharani, na wote tunajua jinsi serikali hii iliopo madarakani isivyopenda kuona mwananchi wa kawaida ananyanyasika lazima wote tujue kwamba zipo hatua zinachukuliwa.
 
Sorry!!
Taifa zima lipo busy na madawa ya kulevya. Hayo mengine yamefungiwa macho kwanza!!
 
Back
Top Bottom