Msukuma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msukuma

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by X-PASTER, Oct 28, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Msukuma Akiwa Mahamani

  Kuna jamaa mmoja mkoani Mwanza, alikamatwa kwa kosa la kuwa na silaha aina ya gobore kinyume cha sheria. Siku ya mahakama kabla ya kesi yake kuanza, kulikuwa na kesi nyingine ya wizi wa ng'ombe.

  Mshtakiwa wa kesi ya ng'ombe ktk utetezi wake alijitetea kuwa yule ng'ombe alikuwa amemrithi toka kwa baba yake na alimpata tangia akiwa ndama.

  Hakimu na wazee wa baraza baada ya kuridhika na utetezi, Mshtakiwa akaonekana kuwa hana kesi ya kujibu na akaachiwa huru kuendelea kumiliki ng'ombe wake....

  Jamaa yangu Maganga kwa kuwa alikuwa mahakamani na alisikiliza ile kesi ya wizi wa ng'ombe, akaona kuwa na yeye bora aige kile alichokisikia kwenye kesi ya wizi wa ng'ombe.

  Kesi yake ilikuwa kama hivi:

  Msoma Mashtaka: Bwana Maganga unashtakiwa kwa kosa la kumiliki, bunduki aina ya Gobore kinyume cha sheria.

  Hakimu: Mshtakiwa unaweza kujitetea?

  Maganga: Bwana Mheshimiwa hakimu, kwa kweli huu ni uwonevu na wivu tu, Hili ligobore nililipataga kwa Babu yangu mzaa Babu yake na Babu yangu, Yaani tangia likiwa kibastora kidogo hakiyamungu, nimelitunza mpaka leo limekuwa limebarehe na kuwa Ligobore likubwa kabisaaa... Bwana mheshimiwa hili ni la kwangu kabisa, tangia likiwa dogo.

  Hakimu: Kwa kuwa umeitunza tangia ikiwa bastora ndogo, kwa hali hiyo umeihakikishia mahakama kuwa hilo gobore ni la kwako.

  Maganga: Ndio Bwana Hakimu. Ni la kwangu kabisa bila shaka

  Hakimu: Na kwa kosa hilo la kuwa na bunduki yenye kukuwa na kuongezeka ukubwa. Nakuukumu kifungo cha miaka mitano jela na kazi ngumu, ili hiwe ni fundisho kwa wengine.

  Na kwa kuiepusha hilo ligobore lako lisifikie kuwa RPG, Mahakama inaitaifisha kwa manufaa ya umma...

  Kooooooooooooorrrrtiiiiiiiiii....!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hey Wasukuma....Mupo?...Getege wanamayo?
   
 3. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  doh!!!!
   
 4. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Msukuma hategemei Gobore PJ, bashosha ng'ombe mwana wane kama angesema ile kesi ya ng,ombe ni ya MSUKUMA hapo sawa, atakuwa Kabila lake jamaa semaga kaona apindishe ukweli kama CCM....The Dong ategemee Gobore?aaaaaaaaahhhhhhh wapi...mkono kwa sana, Kumbuka kuvote kwa SLAA tarehe 31.10. tumutoe KIWETE
   
 5. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  THE DONG awe na gobore la nn tena mwanawane.....
   
Loading...