PreGE2025 Msukuma afurahishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati katika Mji wa Serikali Mtumba

PreGE2025 Msukuma afurahishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati katika Mji wa Serikali Mtumba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu 'Musukuma' akiwa sehemu ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ameelezwa kufurahishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati katika Mji wa Serikali Mtumba na kuipongeza wizara kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa asilimia 94.

Katika maelezo yake, Musukuma amesema watumishi wote wakihamia katika jengo kutawazesha watumishi hao kukaa sehemu moja na kufanya kazi zao kwa ufanisi tofauti na ilivyo sasa ambapo watumishi wamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni Kikuyu na Mtumba.

Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Naye, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. Khatibu Kazungu, amesema kuwa watumishi wa Wizara ya Nishati wanatarajia kuhamia katika jengo hilo kabla ya mwezi Mei 2025 kwa kuwa kazi kubwa tayari imeshafanyika.

 
Back
Top Bottom