Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi, Juma Raibu Juma

CalvinPower

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,571
883
Mh. Juma Raibu Juma,

Uliahidi kushirikiana na Madiwani wote pamoja na Watendaji wa Halmashauri katika kufanya kazi kwa bidii , weledi na kuzingatia maadili ili kuharakisha Maendeleo ya Manispaa ya Moshi na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025.

Mimi nikiwa mwanachama wa ccm nakutambua kama diwani na Meya wa Manispaa ya Moshi mjini, naomba usome machache katika barua hii na utusaidie sisi wanyonge tunaonyanyaswa na baadhi ya watendaji ama watu wenye vyeo bandia hapa Moshi Mjini, hususani hapa jengo kuu la stendi Moshi.

Kuna mtu mmoja anatambulika kwa jina la Method, yeye ni afisa wa mazingira hapa moshi mjini ila amekuwa kero sana na mla rushwa mkubwa sana hapa katika manispaa yako.

Mimi kama mama lishe wa eneo husika amekuwa akininyanyasa sana mpaka kupelekea kukamata bidhaa zangu kwa kisingizio cha uchafuzi wa mazingira. ili niweze kupatiwa bidhaa zangu lazima nimpatie sh 10,000/= kila siku. hii ni kero kwetu sisi ambao tunajitafutia riziki.

Tumepaza sauti sana kwa meneja wetu wa jengo la stendi ila bado tunakosa msaada ila ila tunashukuru sana meneja wa stendi ana utu.

Mstahiki Meya mlisema mtatupigania sisi wanyonge tukiwa na imani kwamba maisha yetu yatakuwa na hauweni ila tunasikikitika sana kuona yanazidi kuwa magumu, leo nibekwaruzana na huyu Method tukatupiana maneno ila yeye alienda polisi nakunifungulia kesi kuwa nimemtukana na kumwambia atakufa kama alivyokufa raisi wetu mpendwa Magufuli. ameamua kumuingiza Marehemu Magufuli ili apate kiki ya upande wa pili.

Huyu sii binaadam bali ni shetani tu. ugomvi wangu na yeye unenda polisi na kumuunganisha na Rais wetu alietuweka hapa mjini? kisa yeye ana sauti, afisa, hapana tusifike mahali tukamlea hivi atatuharibia.

Naomba sana swala hili lisiishie hivi hivi bali chukua muda ufike kituo kikuu cha polisi kesho ulifuatilie ( 22/04/2021 ) na huyu afisa apewe onyo kali.

Nawasilisha.
 
Huyu ndio yule aliyeamuru madiwani wavue barakoa ? hawa vijana walijua sana kucheza na akili za jiwe !
Ndiyo huyo huyo, lofa kweli kweli huyu meya... Wewe unayelalamika achana na huyo meya hakuna kitu hapo, nenda TAKUKURU watamdaka fasta huyo mla rushwa...
 
Wewe ni mwana CCM;

Wewe ni mkazi wa Manispaa ya Moshi;

Andiko lako ni mazungumzo binafsi na Meya wako;

KWANINI UMELILETA HUKU⁉️‼️⁉️
 
meya mwenyewe tapeli tapeli, ashukuru uchaguzi ulikuwa haramu kamwe asingekuwa meya wa Moshi.
R.I.P Magufuli!.
 
  • Mshangao
Reactions: vvm
Mh. Juma Raibu Juma,

Uliahidi kushirikiana na Madiwani wote pamoja na Watendaji wa Halmashauri katika kufanya kazi kwa bidii , weledi na kuzingatia maadili ili kuharakisha Maendeleo ya Manispaa ya Moshi na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025.

Mimi nikiwa mwanachama wa ccm nakutambua kama diwani na Meya wa Manispaa ya Moshi mjini, naomba usome machache katika barua hii na utusaidie sisi wanyonge tunaonyanyaswa na baadhi ya watendaji ama watu wenye vyeo bandia hapa Moshi Mjini, hususani hapa jengo kuu la stendi Moshi.

Kuna mtu mmoja anatambulika kwa jina la Method, yeye ni afisa wa mazingira hapa moshi mjini ila amekuwa kero sana na mla rushwa mkubwa sana hapa katika manispaa yako.

Mimi kama mama lishe wa eneo husika amekuwa akininyanyasa sana mpaka kupelekea kukamata bidhaa zangu kwa kisingizio cha uchafuzi wa mazingira. ili niweze kupatiwa bidhaa zangu lazima nimpatie sh 10,000/= kila siku. hii ni kero kwetu sisi ambao tunajitafutia riziki.

Tumepaza sauti sana kwa meneja wetu wa jengo la stendi ila bado tunakosa msaada ila ila tunashukuru sana meneja wa stendi ana utu.

Mstahiki Meya mlisema mtatupigania sisi wanyonge tukiwa na imani kwamba maisha yetu yatakuwa na hauweni ila tunasikikitika sana kuona yanazidi kuwa magumu, leo nibekwaruzana na huyu Method tukatupiana maneno ila yeye alienda polisi nakunifungulia kesi kuwa nimemtukana na kumwambia atakufa kama alivyokufa raisi wetu mpendwa Magufuli. ameamua kumuingiza Marehemu Magufuli ili apate kiki ya upande wa pili.

Huyu sii binaadam bali ni shetani tu. ugomvi wangu na yeye unenda polisi na kumuunganisha na Rais wetu alietuweka hapa mjini? kisa yeye ana sauti, afisa, hapana tusifike mahali tukamlea hivi atatuharibia.

Naomba sana swala hili lisiishie hivi hivi bali chukua muda ufike kituo kikuu cha polisi kesho ulifuatilie ( 22/04/2021 ) na huyu afisa apewe onyo kali.

Nawasilisha.
Huko moshi mna vituko. Rudisheni Chadema wenu.miaja mwingine mitano mtajifunza kitu
 
Back
Top Bottom