mchovu wa fikra
JF-Expert Member
- Jul 16, 2016
- 335
- 396
SITASHABIKIA SIASA TENA MAISHANI MWANGU,NITAKUWA MTAZAMAJI TU!!!!
MWANAUME MSIMAMO BWANA.
MWANAUME MSIMAMO BWANA.
ADC wanasema "DAIYA DAIYA" yaani "mbele kwa mbele"
Hiki ndicho kipindi cha kumtukana SHONZA , lakini ujumbe anaowafikishia ni mahususi kabisa. mjiongeze la sivyo MBOWE atawachezea sana tu
Pole...SITASHABIKIA SIASA TENA MAISHANI MWANGU,NITAKUWA MTAZAMAJI TU!!!!
MWANAUME MSIMAMO BWANA.
Tumekusikia, kwahiyo..?CCM hakuna Ombwe la Uongozi...NITAELEZA:
Ukimtathmini Rais Magufuli utaweza kuhitimisha pasi na shaka kwamba Utawala wake unashabihiana mno na utawala wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume. Kwa vigezo vyovyote vile vya Utawala na Uongozi,kama alivyo Rais Magufuli, Karume alitawala kwa mkono wa chuma,alitawala kidikteta katika nyanja zote za maisha ya Wazanzibari kisiasa, kiuchumi na kijamii:
Mifano michache Magufuli na Karume wanavyoshabihiana:
Kwa hakika Rais Karume alitawala kwa hofu na vitisho visivyomithilika kwa wapinzani na wakosoaji wake, mara nyingi pia akimtisha hata Nyerere. Ya Magufuli tunaona dalili ya hali tete sana huko mbele ya safari, THE WRITINGS ARE ALREADY ON THE WALL FOR EVERYONE TO SEE.
- Tangu Mapinduzi ya Januari 12, 1964, Zanzibar haikuwa na Katiba wala sheria, bali iliongozwa kwa Amri za Rais(Presidential Decrees), kadri alivyoona inafaa....Rais Magufuli haonekani kujali katiba wala sheria, bali kauli na amri zake ndo zinapaswa kufuatwa, na wasaidizi wake kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanasisitiza hilo -tufuate kauli za Rai
- Kwa mujibu wa Gazeti la The Tanganyika Standard la 9/3/1968, Karume aliapa kutofanya Uchaguzi wala kuwa na Katiba Kisiwani kwa miaka 50 tangu 1964 - 2014 kwa madai kwamba Chaguzi zote ni vyombo vya mabeberu kuwakandamiza wananchi.....Rais Magufuli amepiga marufuku vyama vya siasa na wanasiasa kufanya kazi zao tangu sasa 2016 - 2020 kwa madai kwamba vinamzuia kufanya kazi yake ya Urais; mashaka ni makubwa sasa miongoni mwa wafuatiliaji wa siasa kwamba Uchaguzi Mkuu wa 2020 unaweza kufutwa kwa madai kwamba hali ya Usalama itakuwa hairuhusu.
- Wakati wa Karume, raia au kiongozi yeyote aliyelalamika au kumkosoa Karume, hata juu ya upungufu wa chakula tu, aliitwa mchochezi na adui wa Mapinduzi na hivyo mhaini....nyakati hizi za Magufuli, raia yeyote, viongozi wa upinzani, na chombo chochote cha habari wanaonekana kukosoa, kujadili au kuhoji utendaji wa serikali ya Magufuli wanaitwa wachochezi, adui wa kauli mbiu ya Hapa Kazi tu na hivyo wanakamatwa na kushikiliwa siku kadhaa kabla ya kufikishwa mahakamani na kufungiwa/kutishiwa kufungiwa biashara zao.
- Enzi za Karume, nduguyo akigongewa mlango usiku na kutakiwa kwa mahojiano na serikali usingemwona tena milele....wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM,July mwaka huu, Rais Magufuli alizungumza waziwazi kuwa yeye hana uvumilivu wa kukosolewa na kwamba wote ambao watathubutu kumpinga "watapotezwa" . Amesikika pia akisema yeye hajaribiwi na wote watakaothubutu kumpinga "atawashughulikia" kwa nguvu zote.
- Wakati wa Karume, mfumo wa mahakama wa kawaida ulipigwa marufuku. October 1966, Rais alijipa madaraka ya kuteua mahakama maalumu za kusikiliza makosa ya kisiasa kama vile uhaini, uhujumu uchumi na ubadhirifu wa mali ya umma; mahakama hizi hazikufungwa na kanuni zozote katika kusikiliza kesi, huduma za kisheria kwa watuhumiwa zilifutwa na mawakili kupigwa marufuku Zanzibar......nyakati hizi, Magufuli ameunda Mahakama Maalum ya "Mafisadi", na bila shaka lengo lake hasa ni kudhibiti raia na wanasiasa wa upinzani watakaothubutu kumkosoa.
- Mwaka 1971, katikati ya baa la njaa Visiwani humo, Karume alipiga marufuku uagizaji wa chakula - mchele, sukari, na unga wa ngano kutoka nje, akisisitiza kuwa Zanzibar ilikuwa na uwezo wa kujitegemea kwa chakula....miezi michache iliyopita, Magufuli alipiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje, akidai kwamba nchi ilikuwa na uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha.
- Kwa hofu ya jamii ya Kizanzibari kufikiwa na fikra na mawazo mapya ya maendeleo, Karume alipiga marufuku vijana wa Kizanzibari kwenda nje kwa masomo ya elimu ya juu ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; alipiga pia marufuku Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar....hapa tumeona jinsi Utawala wa Magufuli unavyosumbuka sasa kudhibiti taratibu za vijana kujiunga na vyuo vikuu pamoja na kuwaondosha vijana ambao tayari wako masomoni kwa visingizio kwamba hawana sifa; pia amezuia Bunge kuoneshwa LIVE!
NB.
Simulizi juu ya Utawala wa Karume zapatikana katika maandishi ya wachambuzi mashuhuri wa siasa za Zanzibar kama vile Prof.Issa Shivji, Joseph Mihangwa na Mwanaharakati Yericko Nyerere.
Ni wakati muafaka sasa vyama vyetu vya siasa vinavyojiita ni vya upinzani vijipime kama vinatosha kua vyama vya upinzani ama ni upinzani uchwara?Hizo research zako za kuwa machinga na bodaboda wameacha kuiunga mkono CHADEMA ulizifanyia wapi?
Na ulienda kwa hao watu ukiwa katika sura ipi maana asikwambie mtu ile kuwaruhusu machinga warudi kufanya biashara maeneo mliyowakataza kidogo mkarejesha matumaini ila wengi wao bado hawana imani na siasa ya chama chako wewe mtoa uzi.
Kiukweli napenda nikushauri urejee maneno alioyaongea Mbunge wa Chama chako Ndg Bashe alisema serikali inacheza muziki wa CHADEMA so lengo limetimia kwa asilimia nyingi sana nguvu walizotumia serikali kuhakikisha UKUTA never exist ni nyingi sana utadhani walikuwa wanapambana na watu wale wa Uturuki waliotaka kupindua nchi.
Juliana Shonza bado haujakomaa kisiasa kwa hizo tathmini zako zisizo na uhakika. Umeshhakuwa na uhakika wa chakula cha kila siku hapo ulipo hauna kashikashi ya aina yoyote kama ilivyo kwa upinzani ila hayo ulioyaandika wewe yakiandikwa kwa serikali inakuwa ni uchochezi.Ila time will tell
Machinga hawana imani na serikalo tena wala hao bodaboda hawana hiyo imani nanyi tena wanasubiri tu ikifika muda wa kuwahukumu kwenye mabox ya kupigia kura watafanya kile wanachokililia sasa hivi maana wanapitia wakati kgumu sana katika historia ya Tanzania.
Jifikirie upya kabla ya kuja na hizo blabla zako hata kama familia ya Mzee Nyerere hawajaongea na Lowasa ila kwa hatua waliyofikia CHADEMA ni nzuri sana katika kufanya siasa yaani mlikuwa mnawatangaza kwa wananchi bila kupenda katika majukwaa yenu ya siasa wao wapo Indirect kupitia vinywa vya wanasiasa wenu.
Usiwe mbeya sana hayo ya kumpigia simu huyo mtoto wa Mzee Nyerere wala sisi hayatuhusu.
Tunahitaji siasa safi na utawala bora unaofuata sheria na katiba ya nchi .
Umeandika vyema...nimeguswa na kauli yako kuwa Zitto amesahau udikteta aliofanyiwa na akakubali kujiunga na CHADEMA kupinga udikteta..!!Ni wakati muafaka sasa vyama vyetu vya siasa vinavyojiita ni vya upinzani vijipime kama vinatosha kua vyama vya upinzani ama ni upinzani uchwara?
Vyama hivi ambavyo ndani yake haviishi migogoro na misukosuko,ambayo inaashiria ukandamizwaji na uminywaji wa demokrasia ndani yake leo vinatuaminisha utawala uliopo ni wa kidikteta..
Nani hakumbuki sakata la Zitto alivyodhubutu kutangaza kugombea urais kupitia chama chake cha Chadema,na baadae anatafutiwa zengwe na kufukuzwa chamani,leo hata yeye mwenyewe ameusahau Udikteta aliofanyiwa enzi zile na anaunga mkono harakati za Chadema kutuaminisha Magufuli ni Dikteta.
Nani hakumbuki kilichomkuta Dr. Slaa, au nani hakumbuki upinzani wa Dr. Slaa, ulikua ni upinzani imara wenye masilahi mapana kwa taifa letu,lakini Dr. Slaa alivopinga kuja kwa Lowassa chamani akaambiwa ni bora yeye aondoke ili Lowassa apate nafasi,. Chama kinaendeshwa na maamzi ya mtu mmoja mbona sisi wanachama hatukushirishwa kwenye mchakato wa kumpokea Lowassa ama kumkataa, na sisi ni wanachama? Si kweli kwamba kila mwanachama wa chadema alifurahishwa na kitendo hicho, chama kinaongozwa kama familia yenye mfumo dume.
Nani pia hakumbuki jinsi mchakato wa kumpata katibu mkuu wa sasa wa chama chetu?,mchakato uligubikww na mizengwe kibao,ilimradi tu mwenyekiti anaamua nani akae kwenye nafasi hiyo, na kwa nn mwenyekiti kang'ang'ania madaraka? Chma hakina utamaduni wa kuachiana uongozi?..hayo yote na mengine yanaonesha wazi upinzani wa Chadema ni Upinzani Uchwara, M/kiti anakanyaga katiba ya chama hivi leo akiingia ikulu atashindwa kukanyaga katiba ya nchi?
Nani hakumbuki kua hichi chama ndo chama kilichoanzisha vuguvugu la ufisadi pale bungeni miaka kadhaa iliyopita na waziwazi wakatuaminisha kua Lowassa ni mtuhumiwa namba moja wa Ufisadi,leo wanakuja na ngojera za kutuaminisha Lowassa ni mtukufu kwa kua wamekalia hizo nyaraka za ushahidi...hivi hapa napo panahitaji usomi kiasi gani kujua hawa ni wapinzani uchwara? Maana sio Slaa,sio Tundu Lissu, sio Peter Msigwa, sio Mnyika,na wala si Mbowe wote walimtuhumu Lowassa.
Kwa majirani zetu na penyewe kumenuka,Lipumba alijihudhuru tena kwa mbwembwe,kwa kuitisha press leo anatangaza yeye ndo mwenyekiti halali wa chama,kwani hivi vyama havina katiba? Sasa kama nyie wenyewe ni madikteta kwenye vyama vyenu, huo mnaotuamini ni udikteta uchwara mtaweza kupambana nao?
Ifike pahala watanzania tuamue kutokuwaunga mkono nyie upinzani uchwara, kama miaka kadhaa mlituaminisha kua Tanzania inahitaji rais mwenye maamuzi,rais asie chekacheka mwenye kusimama hadharani na kukemea ufisadi na ubadhairifu wa mali za umma, Mungu si kiziwi kasikia maombi yenu katupa kiongozi ambaye leo tuna sababu lukuki za kujivunia,kiongozi ambaye hajamaliza hata mwaka lakini tayari tumeshaona dira na mwelekeo wa wapi tunaenda,
Cha ajabu kila anachokifanya kizuri kwa watanzania nyie kwenu ni kuponda tu, hivi ni kweli hamuoni,Majipu yaliyotumbuliwa,hamuoni elimu bure?,hamuoni pesa zilizookolewa kupitia watumishi hewa?,hamuoni pesa zilizookolewa kwa kudhibiti ukusanyaji kodi?,hamuoni pesa zilizookolewa kwa kufutwa kwa maazimisho ya siku kuu za uhuru na muungano?,hamuoni ni sh ngapi zimeokolewa kwa kuzuia safari za nje?,hamuoni hata jitihada za serikali kubadili mfumo wa elimu ambao ulikia umechakaa?,hamuoni hata madawati? Mnachoona ni Udikteta uchwara..
Hivi ukuta utatumia sh ngapi? Kwa nini hiyo bajeti msiielekeze kutatua kero za wananchi kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na serikali? Kama kweli mna uchungu na sisi(watanzani) leo hii huu ukuta unamfaishaje mkulima,mama ntilie?mwanafunzi?wazee?,na watanzania wa kawaida hata wafanyabiashara,....lakini huo mnaouita udikteta uchwara ukimuuliza mtanzania wa kawaida atakuambia amepata elimu bure,shirika la ndege limefufuliwa,bomba la mafuta kutoka Uganda linajengwa ambalo litareta ajira na kukuza uchumi,reli itajengwa ndani ya miaka mitatu,elimu bure nk..
BORA UDIKTETA UCHWARA KULIKO UPINZANI UCHWARA
View attachment 391088
CHALI KABISA, NGINJA NGINJA, KIFO CHA MENDE, UKUTA PWAAAAA. Icheki hiyo ngumi ya Magufuli
Acha hasira, subiri mpaka Oktoba 1.Hapa ndio nimeshafika ukomo wa ufuasi wangu kwa hiki chamaaa
Kwa mtu ambae kichwani ni betry low anaweza kuandika hayo ila nakuambia ukuta umefanikiwa sana jeshi linafagia wamefagilishwa bila kupenda polisi wanafanya mazoezi ya kukata vitambi kisa ukuta sasa nguvu kubwa ya nini wakat CHADEMA hawana hata upanga wala sindano wakiulizwa ukuta viongozi wa CCM ukuta shonza umekimbilia kupost ukuta huoni kama imefanya kazi?Leo nitaanza bila salamu,
Ndugu wanajamvi, kwa siku za nyuma kidogo, takribani mwaka mmoja uliopita niliwahi kuandika hapa kuwa CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi na nikasema katika maneno ya hitimisho la andiko langu hilo kuwa;
Nakumbuka vizuri, niliambulia matusi mengi kama ninavyotaraji hata leo pia. Kama nilivyosema wakati huo nitasema tena leo kuwa WATANZANIA wameshapoteza IMANI na chadema na uongozi wake. Wasomi, wanataaluma, na makundi mengine yenye influence kwenye jamii hawaiungi tena mkono chadema, nimeshangazwa hata bodaboda na machinga nao wanajitenga mbali na chadema.
Waandishi makini wameacha kabisa kuwaunga mkono chadema, hata wale ambao waliwaandika vizuri kwenye social media akina Mwanakijiji, Chahali na hata Pasco wamekuwa wakiwashushua kila uchao juu ya maamuzi yao na uelekeo wao.
Kwa mara nyingine tena, LEO umefanyika uamuzi mwingine wa kuchekesha na wenye kuudhi. Uamuzi unaoendelea kuthibitisha kuwa Uongozi wa CHADEMA umekosa dira, maono na hawana tafakuri sahihi juu ya mabadiliko ya wakati na namna bora ya kuendesha siasa za sasa. Walipodhani kuwa FEDHA zinaweza kuwa THINK TANK ya chama na kusahau BRAINS matokeo yake ndio haya, mnakosa strategic plan na mnaishia kughairisha mikakati bila sababu za msingi zenye kueleweka kwa watu na kupoteza influnce zaidi, actually hata wanachama wanawadharau kwa mwendo huu.
Labda ilikuwa utani, lakini UONGOZI wa chadema wanapaswa kufahamu kuwa Naibu Katibu Mkuu wao na wanachama wao 27 wako korokoroni hivi sasa kwa sababu ya mpango wao wa hovyo. Watu hawa tumaini lao ilikuwa ni kuungwa mkono lakini uongozi wao umewasaliti, umewatanguliza kama CHAMBO then mpango umeahirishwa. Lakini kuna vijana chungu mzima, ambao walikuwa driven na UKUTA wakajikuta wanamtukana Mkuu wa Nchi na Serikali yake nao wananyea debe wakati uongozi wao unaghairisha kiutani utani, opresheni iliowafikisha jela.
Hivi visingizio kuwa familia ya Nyerere imekutana na Lowassa na kumuomba, naomba nisitolee maelezo ila nitampigia simu personally msemaji wa familia hiyo Ndugu Makongoro ili ikiwezekana kesho ama keshokutwa afanye press, au aende Clouds au Efm kuthibitisha kuwa walikutana na Lowassa na kumuomba a-abort mpango mzima.
UKUTA chali, kama nilivyotegemea.
Jioni Njema...!!
kwa hiyo kwa vihoja vyako hapa jukwaani, ulikuwa unataka watu wapigwe kesho?Execuse zinazotolewa ndio zinaudhi zaidi, Siku kumi nyuma unasema tumekutana na Viongozi wa dini tumezungumza nao na mkasema kuwa UKUTA uko pale pale leo mnasema tumezungumza na Viongozi wa dini (kama vile ni kitu kipya) na kuongeza tumezungumza na familia ya Mwalimu Nyerere (haijawahi kutokeo) tumeamua Kughairisha UKUTA, sio kuvunja kabisa bali kughairisha eti wakitegemea kutakuwa na tension kama ya awali.
Hesabu mbofu sana hii
Sidhani kama elimu yako ina msaada katika upendo wako na chama chako. Hao vijana walioshika mabango wangekuwa wameenda hivyo mbele ya Lowasa ungesema wamelipwa ili wafanye hvyo. Any way siasa ndivyo zilivyo lakini elewa kuwa research hauwezi kuifanya ukiwa unaangalia TV au kusikiliza mtu fulani anchosmulia maana hizi TV na vyombo vyote vya habari sasa hivi vinaongea na kusifia tu serikali ili waepuke rungu la kupigwa BANN na serikali inayoongozwa na chama chako.Unadhani kujua kama unaungwa mkono na mtu ama kundi la watu unahitaji research kubwa ya kukodi madokta na maprofesa. Observation ya kawaida kabisa ya macho yako inatosha kukuthibitishia kuwa watu gani uko nao. Machinga walienda kumpokea Magufuli Lumumba wakiwa na mabango yao na wakarudishwa kufanya kazi kwenye maeneo yao na Mkuu wa Nchi akapendekeza itengwe siku na ufanyike utaratibu wa kuwafanya machinga wafanye biashara zao bila usumbufu. Bodaboda wao walitoa na tamko kabisa kuwa hawaiungi mkono CHADEMA, kwa simple Observation hiyo ilitosha kujiridhisha kuwa chadema haiungwi mkono na makundi hayo.
Kuhusu eti chadema wamepata Promo ni wazo la kijinga, yaani hiyo itafanana na kunywa sumu na kunusurika kisha useme nilikuwa nataka nitangazwa kwenye vyombo vya habari nijulikane, sawa utajulikana with very bad reputation, kuwa coward aliyejaribu kujiua, sasa maisha yatakuwa na faida gani..? Itafafa na CUF siku moja wakitulia wasema mgogoro wetu ulitusaidia promo.
Kama walidhani kuwa chadema haisikiki na haijulikani na wakaunda mpango huu ili wapate kick ndio kusema kuwa unathibitisha uzi wangu kuwa chadema kuna ombwe la uongozi, hawana think tank ya kuwashauri strategy za maana za kuwapa kick...this shit demoralize wanachama, then unasema umepata kick, u accept a defeat bila maelezo ya kuonyesha ushujaa wako then unajigamba kuwa umesikika, na unajulikana. Kwani shida ya chadema ni kujulikana???? OMBWE la UONGOZI
Sijajua huyu Shonza alisahau nini CDM. Jamani msaidieni akachukue alichosahauSasa wewe kama CHADEMA ina Ombwe la Uongozi si uache ife ili iwe furaha yako.
Kwa nini mnamjibu huyo? hakuna kitu kizuri kama kum-ignore mtu. Mimi humu huwa nachagua wa kumjibu! Kuna "takataka" nyingi sana humu covering all walks of life! Lazima uwe macho unamjibu nani! Mnapoteza muda kwa mtu ambaye ni platform politician!Shonza ni mwanamke asiyejitambua huwez kuwakuta wakina bulaya na halima mdee mitandaoni wakitoa uharo fuatilia interview ya jana eatv ya bulaya aliulizwa maswali mengi ya mtego kuhusu wasira lakin kamwe hakuonesha kumponda wasira pale ndo utagundua akili za mtu mwenye akili angakuwa huyo dada wa udsm mweeeee siasa ni mzunguko ccm haiwez kuwa hapo milele pia hawez kunipa ujumbe huyo katoa wapi huo uwezo?
Kwani kaanza leo kutokufa moyo muulize kama angelikufa Moyo wakati anaelezwa kuwa anatumika angelikuwa hapo alipo?" Yawezekana kazoea tabia aliyonayo " hawezi iacha ILA NAAMINI UNAFIKI UNAKIKOMO CHAKE TU, IPO SIKU
Tafsiri ya ukuta ni mwisho wa kufikiri...Makonda,Tatizo kubwa la Mbowe ni kuanzisha hoja zisizo na ushawishi kwa wananchi baada ya kushindwa analialia....hadi leo asubuhi kulitoka taarifa kuwa wameahirisha wakaleta propaganda kukanusha,matokeo yake..,chali ndembendembe kifo cha mende...chaliiii!
Kwa mtu ambae kichwani ni betry low anaweza kuandika hayo ila nakuambia ukuta umefanikiwa sana jeshi linafagia wamefagilishwa bila kupenda polisi wanafanya mazoezi ya kukata vitambi kisa ukuta sasa nguvu kubwa ya nini wakat chadema hawana hata upanga wala sindano wakiulizwa ukuta viongozi wa ccm ukuta shonza umekimbilia kupost ukuta huoni kama imefanya kazi? Kirefu cha ukuta kishasambaa jamii imejua maaana ya ukuta halafu unaandika watanzania unajumuisha wote hadi wale milion 6 zile takwimu za asilimia 65 ya wanaomaliza udsm ni ****** zipo sahihi na nyie ndo zao lao mnajidhihirisha hapa mana unataka wapigane raia wa kitanzania ili iweje? Unataka kuwa Kiongoz unaehamasisha migogoro!!!!! halafu pia post yako ni ya kichochezi.
Sina la kuongezaHapa ndio nimeshafika ukomo wa ufuasi wangu kwa hiki chamaaa