Leo nitaanza bila salamu,
Ndugu wanajamvi, kwa siku za nyuma kidogo, takribani mwaka mmoja uliopita niliwahi kuandika hapa kuwa
CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi na nikasema katika maneno ya hitimisho la andiko langu hilo kuwa;
Nakumbuka vizuri, niliambulia matusi mengi kama ninavyotaraji hata leo pia. Kama nilivyosema wakati huo nitasema tena leo kuwa WATANZANIA wameshapoteza IMANI na chadema na uongozi wake. Wasomi, wanataaluma, na makundi mengine yenye influence kwenye jamii hawaiungi tena mkono chadema, nimeshangazwa hata bodaboda na machinga nao wanajitenga mbali na chadema.
Waandishi makini wameacha kabisa kuwaunga mkono chadema, hata wale ambao waliwaandika vizuri kwenye social media akina Mwanakijiji, Chahali na hata Pasco wamekuwa wakiwashushua kila uchao juu ya maamuzi yao na uelekeo wao.
Kwa mara nyingine tena, LEO umefanyika uamuzi mwingine wa kuchekesha na wenye kuudhi. Uamuzi unaoendelea kuthibitisha kuwa Uongozi wa CHADEMA umekosa dira, maono na hawana tafakuri sahihi juu ya mabadiliko ya wakati na namna bora ya kuendesha siasa za sasa. Walipodhani kuwa FEDHA zinaweza kuwa THINK TANK ya chama na kusahau BRAINS matokeo yake ndio haya, mnakosa strategic plan na mnaishia kughairisha mikakati bila sababu za msingi zenye kueleweka kwa watu na kupoteza influnce zaidi, actually hata wanachama wanawadharau kwa mwendo huu.
Labda ilikuwa utani, lakini UONGOZI wa chadema wanapaswa kufahamu kuwa Naibu Katibu Mkuu wao na wanachama wao 27 wako korokoroni hivi sasa kwa sababu ya mpango wao wa hovyo. Watu hawa tumaini lao ilikuwa ni kuungwa mkono lakini uongozi wao umewasaliti, umewatanguliza kama CHAMBO then mpango umeahirishwa. Lakini kuna vijana chungu mzima, ambao walikuwa driven na UKUTA wakajikuta wanamtukana Mkuu wa Nchi na Serikali yake nao wananyea debe wakati uongozi wao unaghairisha kiutani utani, opresheni iliowafikisha jela.
Hivi visingizio kuwa familia ya Nyerere imekutana na Lowassa na kumuomba, naomba nisitolee maelezo ila nitampigia simu personally msemaji wa familia hiyo Ndugu Makongoro ili ikiwezekana kesho ama keshokutwa afanye press, au aende Clouds au Efm kuthibitisha kuwa walikutana na Lowassa na kumuomba a-abort mpango mzima.
UKUTA chali, kama nilivyotegemea.
Jioni Njema...!!