Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,607
- Thread starter
- #221
Umeandika maneno meeengi, lakini hayana content yeyote.Ni kweli CHADEMA wamekosa uongozi na umakini kwa sababu mtu kama huyu mleta mada alipaswa alalamikiwe na viongozi wa chadema kwani ni zaidi ya mchochezi.
Mleta mada ni mtu wa ajabu sana anayefikiri mchuano utakaofanyika kati ya CHADEMA na JWTZ, FFU, Magereza, JKT na vikosi vingine maalum ni kama mechi ya simba na Yanga wanaocheza kwa kutumia mpira mmoja.
Mleta mada anasahau kuwa Chadema hawajawahi kufanya fujo kwenye maandamano lakini wamekua wakipoteza watu wao na kwa sasa wameona hali inaweza kuwa ni mbaya na msiba mkubwa kwa taifa ambao utaacha uadui mkubwa kati miongoni mwa watanzania.
Hawa vijana wa CCM ni waajabu sana ,kwa sasa ndio wanaochochea maandamano. Na walikua wanayasubiri kwa ham kubwa ili waone taifa likinuka damu. Na kuhakikishia wewe mleta mada risasi zikiwaua watu mamia ,maelfu ujue ndio laana ya nchi hiyo.
Damu ina tabia ya kuongeza unasiri na visasa.
Ni aibu kubwa kabisa kwa mtu na akili zake tena msomi kushabikia maandalizi ya kuua watu. Huu ni Ujinga mkubwa kupita maelezo. Hata kama ni siasa za kufukuzwa kwenye chama sio hivyo. Hivi vyama vimeanzishwa na watu sio vyama vya kimungu mpaka mtu unahamasisha mauaji na chuki kwa kiwango hiki.
Ninaimani waliokuwa wanaiunga mkono CCM sio zaidi ya 52% kwa mwaka jana. Afrika na Tanzania hakuna uchaguzi huru na wa haki kwa kiwango cha chama tawala kushinda kihalali kwa 58% hapo maguvu ya dola na kila aina ya uchafuzi ni lazima ufanyike kwenye nchi changa kidemokrasia. Kwa hiyo baada ya uchaguzi tulipaswa kufanya juhudi za kuwaunganisha hawa watu ambao wanaonekana walikua na nguvu zinazolingana japo mmoja alikua anatokana chama dola na mwingine upinzani.
Sio busara kwa vijana wa CCM kuendeleza zile hulka za kupata madaraka kwa kupiga watu na kujenga chuki.
Kama mnataka kuheshimika ni lazima muheshimu wengine.
CCM ndio walio na dhamana ya amani ya nchi hii lakini cha ajabu nao wamekua ndio wanaotoa matamko na lugha zisizo na staha kwa watu wengine. Mara ****** ,nyumbu, kushikishwa ukuta, kushughulikiwa na wafungwa gerezani, majipu, mafisadi,majizi n.k. Huku ni kujenga uhalali wa kuwachukia wengine bila sababu za kisheria.
Siasa za kupata umaarufu kwa kujenga chuki kwa wengine ni hatari sana.
Naamini mwaka kesho Uchaguzi wa CCM utakua wa kutisha kama hawa vijana hawatafundwa na kuwa wazalendo waachane na vita ya madaraka yatokanayo na chuki.
Nilitegemea kuwasikia wanaCCM wapenda amani wakijitokeza na kumpongeza Mbowe na Chama chake kwa kuepusha mauaji na vurugu ambazo zingeweza kutokea lakini badala yake wanajitokeza na kuonyesha wazi kutofurahishwa na hatua ya chadema ya kusitisha maandamana.
Hivi inawezekana kweli kwa binadamu kufurahia mwenzako akipigwa risasi kwa kuvaa tisheti na kushika bendera mkononi tu. Ajabu kabisa.!!
Usifikiri askari aliyekua amemuua Mwangosi hata kama ataachiwa huru ataishi kwa furaha kila anapokumbuka tukio la kumtoa mtu utumbo akiwa ameshika kalamu na karatasi tu. Very sad kwa msomo kama mleta mada kufurahia maandamano ya kumpinga Rais wa nchi. Huyu mleta mada hafai hata ndani ya CCM. Ni mtu wa chuki na mchochezi aliyepitiliza. Angalieni mwinyi anavyoishi maisha marefu na ya amani kwa upendo wake kwa watanzania. Chuki ni sumu mbaya sana kwenye maisha ya binadamu. Kujito kwa Dr. Slaa chadema ni hiyari yake alibembelezwa sana akakataa sasa kuendeleza siasa zake za chuki kwa utawala wa JK na kuhamasisha watu kuandamania na kuua itakua sio kuwatendea watanzania haki. Amejitoa basi . Tangu enzi za kudai uhuru watu walitofautiana na wakatengana kisiasa na baada ya uhuru pia mambo hayo yapo mpaka leo. Kudanganya watu eti kitakuja chama chenye mwenyekiti anayeongoza kwa mfano ambao hata mbinguni haupo ni unafiki ,uongo na upotoshaji. Tofauti ndani ya vyama hazikuanza leo na hazitaisha leo. Ishu sio Mbowe wala Lowasa, wala Slaa . Ishu ni wanasiasa wasaka tonge kujichomeka ndani ya vyama kutumikia chama tawala kwa ahadi ya vyeo ambavyo ndani ya chama tawala vinapatikana kwa mamlaka waliyopewa na katiba. Ni rahisi sana kuhama upinzani kuliko kuhama CCM kwenda upinzani pasipo na vyeo kama Ukuu wa Wilaya,uRC, ubalozi,uwaziri, ukuu wa idara na mashirika mbalimbali tena kwa mishahara minono. Upinzani hakuna kitu zaidi ya kuwekwa mahabusu makesi kila kukicha.
Ukiona mtu ametoka CCM na kwenda upinzani ujue amejitolea kweli kweli lakini ukiona mtu ametoka Upinzani na kurudi CCM ujue amechoka kuishi maisha magumu.
Nawapongeza wanaChadema kwa kuamua kuachana na maandamano na kulinda amani ya nchi yetu. Nilikua nayapinga sana haya maandano mwanzo mwisho na sasa yameahirishwa nawaunga mkono viongozi wa CHADEMA kwani kupingana na dola sio jambo la busara. Siasa nzuri ni mazunguzo na sio nguvu ,matusi na vurugu.
Big up Mbowe kwa kuepusha shari.
Nawaomba wale wote wanaojua umuhimu wa amani wajitokeze kumuunga mkono Mbowe.
Pongezi pia kwa mh. Rais kwa kujitokeza na kueleza furaha yako ya kukutana na kushikana mkono na Mh. Lowasa , umeonyesha kuwa unajali umoja na upendo wa watanzania pamoja na ukweli kuwa wafia vyama kama mleta mada hupenda kupandikiza chuki kuliko kujenga amani.