Msingi wa nyumba ya vyumba vitatu

Msingi wa nyumba ya vyumba vitatu

Maria Nyamhanga

Senior Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
130
Reaction score
25
Naomba msaada kwa wataalam na wenyeuzoefu.

Ninakiwanja mkoa wa mara, nimedunduliza vipesa vyangu kiasi cha milioni 4. Je naweza jenga msingi imara wa vyumba vitatu self contained?
 
Kwa ufundi,cement,mawe nk....sina uhakika vizuri,lakini raha ya ujenzi ni kuanza,ukishaanza utaona nyumba inanyanyuka tu,ata Kama una uwezo wa ku nunua mifuko kumi ya cement we anza tu Mjomba ,husisubiri mirioni nyingi ndio uanze.
 
Kwa ufundi,cement,mawe nk....sina uhakika vizuri,lakini raha ya ujenzi ni kuanza,ukishaanza utaona nyumba inanyanyuka tu,ata Kama una uwezo wa ku nunua mifuko kumi ya cement we anza tu Mjomba ,husisubiri mirioni nyingi ndio uanze.

Asante kwa ushauri...
 
Unaweza. nakuhakikishia kwa asilimia 100. Pata fundi mzuri mwambie akupigie hesabu. Akikupigia lete hapa hesabu zake tuzifanyie vetting.
 
Naomba msaada kwa wataalam na wenyeuzoefu.. ninakiwanja mkoa wa mara, nimedunduliza vipesa vyangu kiasi cha milioni 4. Je naweza jenga msingi imara wa vyumba vitatu self contained?
Mtafute fundi m-discuss labour charge na ramani,then hapo utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupiga mahesabu vizuri
 
unaweza. Nakuhakikishia kwa asilimia 100. Pata fundi mzuri mwambie akupigie hesabu. Akikupigia lete hapa hesabu zake tuzifanyie vetting.

Jamani na mimi naomba mnisaidie hivi msingi unaweza chukuwa cement mifuko 19 peke yake?

Nimempa ramani fundi , ramani ya vyumba vitatu master na living room na dinning na jiko na store room na chumba kidogo cha kufulia nguo.

Amechimba msingi na msingi wa nyuma kwa nyumba hiyo zimekula course 10 kulingana na usawa wa nyumba kwa mbele ambapo zimekwenda course 4 na sehemu zingine course 3.

Sasa kwavile hii ni nyumba yangu ya kwanza sijui sana sana kwamba hivi ndio imechukuwa gharama yote hiyo japo nimesimamia sio siku zote siku zingine alikuwa yeye na mafundi wasaidizi tu.

Naomba ushauri na mimi.
 
unaweza. Nakuhakikishia kwa asilimia 100. Pata fundi mzuri mwambie akupigie hesabu. Akikupigia lete hapa hesabu zake tuzifanyie vetting.

Samahani na bado anataka mifuko 8nya kutengenezea zege la foundation na nondo kama 16 za milimita 12 na vitu vingine nitakumbuka baadaye. Je ni sahihi kwa kukamilisha msingi huo?

Asante kwa msaada
 
samahani na bado anataka mifuko 8nya kutengenezea zege la foundation na nondo kama 16 za milimita 12 na vitu vingine nitakumbuka baadaye. Je ni sahihi kwa kukamilisha msingi huo?
Asante kwa msaada

Hayo mahesabu ni sahihi. Hata hivyo endelea kusimamia closely.
Hongera sana na kila la heri katika ujenzi...
 
hayo mahesabu ni sahihi. Hata hivyo endelea kusimamia closely.
Hongera sana na kila la heri katika ujenzi...

Asante kunijibu. Hata mimi nimesita na hesabu hiyo. Je unaona kaniibia au siyo?
Asante kwa sasa nimesimama mpaka mwenyewe niwepo ndio atafanya kazi
nimesita sana mifuko 19 imekwenda kwenye msingi na haujakwisha? Jamani nyumba si ya kitajiri hiyo?
 
Kwa matofali msingi unakula tofali 800 hadi 1000 inategemea na eneo pamoja na ukubwa wa nyumba. Tofali hizo zitakugharimu kama 1300 ama chini ya hapo za Nchi 6 ndio nzuri kwa msingi. Hela inayobaki inatosha kabisa kujenga msingi maana kuna nondo, cement, mbao na ufundi.

Fanyakweli wangu usiogope ila uhakikishe unawasimamia mafundi ukifumba macho tu wanakuibia. Ujumbe nyumba imara hujengwa kwa stage haichipui kama uyonga.
 
Na bado anataka mifuko mingine 10 na nondo 16 za ml. 12 na wire na vikorokoro vingine?Nina kokoto nusu lori.

Je kwa ushauri wako kwani ni lazima kuweka msingi nondo? Najuwa kule kwenye lenter ni lazima niweke nondo, kwani ni lazima na chini? Nisaidie kaka
 
asante kunijibu. Hata mimi nimesita na hesabu hiyo. Je unaona kaniibia au siyo?
Asante kwa sasa nimesimama mpaka mwenyewe niwepo ndio atafanya kazi
nimesita sana mifuko 19 imekwenda kwenye msingi na haujakwisha? Jamani nyumba si ya kitajiri hiyo?

Fundi akipata mwanya tu umeumia. ila principle ni kwamba kama hujamkamata live usimwambie kitu ili asihisi kama unamstudy.
 
Mbona mi naona mil nne kwa msingi tu ni nyingi sana wakuu
 
Kwa mkoa wa mara huko msingi tunatumia mawe ambayo kupatikana ni rahisi sana tena unakuwa msingi imara wa karne nzima bila mpasuko..hapo kusanya vifaa uanze kiongozi huna haja ya kusita....hatua moja mbeelee mwaka si unaona unaanza kukatika slowly..KIMBIZAAA.
 
Aisee Hongera kaka, Sijui mi nimeibiwa? maana fundi alipandisha kozi 8, tofali zilizotumika ni 1500, ni nyumba self contain 3 bed rooms, 1 ikiwa master , kitchen, dinning, sitting store na bafu! lakini baadae niligundua kuwa gharama zingepungua kama tungeka kitu kama steps kwenye kutafuta ile level ya ardhi na uzuri ardhi niiliyoipata udongo ni mzuri tofauti kidogo na maeneo mengine ya Mji wa Arusha ambapo kuna ile kitu wanaita nguselo yaani udongo mfinyanzi.

Nakushauri cheki na fundi uone kama mnaweza punguza gharama kwenye tofali na cement kwa namna hiyo ya kuweka steps ambazo kama zitakuwa well planned zitapendesha nyumba lakini kikubwa inategemea na taste yako juu ya mwonekano wa nyumba yako.

ZINGATIA:
hufanyi majaribio hapo kaka, na ni kitu cha maisha yako so unatakiwa kuridhika kwa kutoa doubt zozote zinazoweza kujitokeza.
 
ufundi =500,000/=, kokoto lori 2= 300,000/-; cementi mifuko 20 =280,000/- tofali 1000= 1300,000/= kuchimba msingi= 100,000/=;Mchanga lori 2=80000/= Misc exp 300,000/= Total = ?????? Anza kama unayo hiyo pesa
Nashukuru mkuu kwa mchanganuo...
 
Kwa mkoa wa mara huko msingi tunatumia mawe ambayo kupatikana ni rahisi sana tena unakuwa msingi imara wa karne nzima bila mpasuko..hapo kusanya vifaa uanze kiongozi huna haja ya kusita....hatua moja mbeelee mwaka si unaona unaanza kukatika slowly..KIMBIZAAA.

Asante Kobe.. unafikiria mawe yanaweza kuwa trip nhapi hivi. Msaada zaidi.
 
Kama ni msingi tu wa kawaida bila kumwaga jamvi, inatosha na unaweza kunyanyua na ukuta kidogo
 
Back
Top Bottom