Fundi anataka milioni 1.2 kuezeka nyumba ya vyumba vitatu

Mindset100

Member
Joined
Jun 23, 2026
Posts
26
Reaction score
73
Hapa wazee napigwa? Nyumba ina vyumba vitatu na iko mstatili ameniambia milioni moja na laki mbili, vifaa vyote ni vyangu maeneo ya Dar iko sawa? Na mwingine kaniambia laki nane na nusu lakini ananiambia ninunue mbao buguruni eti mbao moja 18,000/= hapo vipi?😀

Ukubwa wa nyumba mita urefu mita 10 upana mita 9.

Alianza na milioni 1.5 hapo milioni moja na laki mbili kashuka na aligoma katakata akasema hata iwe milioni 1 hapana.
 
Hapa wazee napigwa? Nyumba ina vyumba vitatu na iko mstatili ameniambia milioni moja na laki mbili, vifaa vyote ni vyangu maeneo ya Dar iko sawa? Na mwingine kaniambia laki nane na nusu lakini ananiambia ninunue mbao buguruni eti mbao moja 18,000/= hapo vipi?😀
Mzee hii mbona unafanya mwenyewe tu, labda kama ni ke ama bonge nyanya.
 
Yale maisha kama unafanya kazi ya kuondoa maisha lazima iendane maan ukipona ni ulemavu wa kudumu asa 200k atajimudu vp mpe mkuu
Ambatanisha picha ya jengo hapa unaweza kuta jengo lenyewe linasadifu usije bila ushaidi tukatoa mawazo kumbe unamnyonya fundi
 
kati ya kazi rahisi za ufundi wetu huu kwangu ni roofing.
Chaguo ni lako mkuu wa milini ama wa laki i nane , ungekutana na sisi hata 500,000, tungefanya na material ungenunua unapo taka wewe.
Ila huyo aliekuambia kununua mbao buguruni kuna namna atapata hela nyingi kuliko wa milioni
 
Hapa wazee napigwa? Nyumba ina vyumba vitatu na iko mstatili ameniambia milioni moja na laki mbili, vifaa vyote ni vyangu maeneo ya Dar iko sawa? Na mwingine kaniambia laki nane na nusu lakini ananiambia ninunue mbao buguruni eti mbao moja 18,000/= hapo vipi?😀

Ukubwa wa nyumba mita urefu mita 10 upana mita 9
Vyumba vitatu na sebule na dinning au vyumba vitatu milango nje? Inaweza ikawa nyumba ya vyumba vitatu lakini ikawa na vitu kibao, kitchen,stoo, public toilet ya ndani, etc,

Mbao za buguruni ujanja mwingi, we umejengea Maeneo gani? Nikupe fundi
 
Nyumba mstatili tu mzee imetoka mbele varanda tu kidogo.
 
Back
Top Bottom