Msimamo wetu sisi CHADEMA asilia

Msimamo wetu sisi CHADEMA asilia

mwenzio slaa kastafu siasa ww vp bado ujastafu.

SLAA kastaaf siasa za vyama tu na sio amestaaf hata kutupa mwongozo wa sehemu na mambo sahihi ya kufanya kwa wakati gani. Na itategemea kwa sababu yupo tayari kama wananchi wataona anahitajika sana kurudi ulingoni kwa matakwa yao yupo tayari kurudi. Siasa hazina mwisho nikuambie.
 
lazima tukubali contradiction ndani ya ccm ni kubw a kuliko tatizo la ukawa, na tayari magufuli ni kama anakimbia na mpira wake mwenyewe bila kumpasia mtu wala kocha wake mkuu, ashindwe, au ashinde, ni lazima sana ccm itabadilika sana, nahisi kitu cha kwanza tutakachoona ni revolt against their chairman, muda pale uraisi utaisha, nikiingia rohoni kwa pinda, balali , profesa muhongo, mark mwandosya, warioba, hawa ni watu wana maudhi kwa sasa ya rohoni, lakini baada ya tarehe 25 octoba yatakuwa maudhi ya wazi, ni kwa mtazamo wangu, hawa ni watu wazima, amabo wamefanya uamuzi wa uvumilivu, wakiamini kuwa kwa nini tumuachie chama mwenyekiti wa mpito ( miaka kumi imepita) na aondoke ili tukichukue chama cha nyerere kutoka kwenye mitandao na uswahili uliokithiri, naamini hii itakuwa sooner than later, hapo contadictions za magufuli hatutazizungumzia, kwani kama suala ni mabadiliko, basi mabadiliko kutoka kwa kikwete, tofauti na mabadiliko ya lowassa ya kutoka CCM kwenda chadema. magufuli atataka mabadiliko ya mfumo wa utawala wa nchi, na ndani ya CCM, na pamoja na uongozi wote kutoka wilaya hadi taifa, watu wa poyoyo, jazba na matumizi mabaya ya nguvu za umma, mitandao ya watu na blind followers ( bulembo, nape, makonda etc) , kwa hiyo situation ya siasa tanzania ndani ya nchi na ndani ya ccm yenyewe, bado iko very fluid, bunge bado hapo, na contradiction za zanzibar bado hapo

Kamanda nadhani ungeanzisha topic ya ccm then ukaongelea mambo yako hayo. Huku hayatuhusu. Kama wewe ccm basi hapa umepotea.
Nasema chadema asilia tunajiandaa na matukio hasa baada ya uchaguzi mkuu. NI LAZIMA TUTASHINDWA HILO HALINA UBISHI. Kitu kikubwa ambacho kitatufanya tushindwe nadhani kila mtu anakifahamu wala siyo siri ya kuficha. Kukumbatia MAFISADI. HAPO NDIPO TUMEPOTEZEA MWELEKEO. kama ni ndege ikishapoteza mawasiliano basi inaenda kuanguka hakuna namna. Chadema au ukawa hivyo hivyo inaenda kuangukia pua. Hivi sasa ipo speed 360 inaelekea shimoni. Hakuna atakayeweza itoa shimoni labda makamanda wetu Dr Slaa na Prof Lipumba warudi ulingoni. Kama sivyo tunaona kabisa baada ya uchaguzi tumeshajichimbia kaburi! Hakuna kukwepa. Hapo ndipo tutakapoona mafisadi wakitukimbia baada ya mission yao kuwa imetimia. (Mission accomplished ).
 
Safi sana kamanda kwa kujitambua, hata mimi ni chadema siwezi kuuza utu wangu kisa feza anazotoa mzee low.... Nipo pamoja na Dr SLAA

tuko pamoja nasubiri tar25 lazima waadhibiwe wanatufanya sisi mazuzu. miaka yote hii tunayumba na chama leo gafla bin vuuuuuu tena kwa kuvunja na kuvuruga katiba na taratibu zote na michakato ya kumpata mgombea na anapewa kugombea urais tena siyo wa chama tu wa vyama vyote, tutaendelea kuhoji nini kilitokea na tunasubiri tr25 tukiadhibu chama alafu mny/k atatueleza vizuri ilikuwaje kuaje yale tuliyokubaliana yakavunjwa na hili balaa kutoka ccm. kufaidi miga...... wafaidi wao, sisi tuambulie kuwasindikiza ikulu, nani kasema..... tar25 ifike haraka. ninahasira sana watu walivunjwa mikono kwaajili ya chama leo wanaoneka hamnazo kweliii........!! kweliii......!! ahaaa....!!
 
msimamo wangu binafsi sitaki unifuate wala si kushauri ubadirishe wako, siwezi kuunga mkono ufisadi au kumuunga mkono fisadi, bado sijaona hoja nzito kutoka kwa Lowasa au wapambe wake ya kuwaridhisha watanzania
 
Unapoona mtu anadhubutu kunyanyua mdomo wake huku akimsifu lowasa kua nikamanda na akimtuhumu dr.slaa kua ametumwa na CCM mtu huyo muangalie kwa jicho la tatu. Watu wanahoji vitu vya msingi wewe unakuja na tuhuma zako ambazo hazina hata kamshiko. Lowasa amewalisha nini nyinyi? lowasa shida yake yeye awe rais na sio kutatua kero za watanzania kamaanavyo jinasibu kwenye majukwaa. Angekua ana nia ya kutatua asingetuibia kias hicho. Kama lowasa alikua anaona CCM, mfumo wake ni mbaya na hakuna demokrasia kwanini walichukua fomu ya urais? watanzania ifike mahali tuziache akili zetu zifanye kazi natupunguze mihemko ya vyama vya siasa "Politician ain't humanitarian" tunakazi ya kuijenga Tanzania yetu. Epuka matapeli

epuka matapeli kwa kutoichagua ccm.....vyovyote vile ...kura yangu nilishaamua miaka karibu mitatu nyuma kwamba october 2015 ....kura yangu haitaenda ccm....bora nichague kivuli kuliko ccm..........
 
taFuteni chama kingine ...kwani unang'ang'ania chadema kunani..kama nyie ni wafuasi wa Dr silaa kastaafu siasa nyie nanyi muamue moja sio mnakuwa wanafiki wanafiki tuu hapa.. tunafanya kazi kama mchwa sio kuanza kukosoana hapa ni kwa manufaa ya nani ya Dr Slaa?? watanzania wanataka mabadiliko mnawasaidiaje? weka Kipaza sauti Chini wengine wanyanyue wauze sera .. msituzingue sisi.. Chama ukawa ..akili za kindorobo ndorobo kama CCM..

CHAGUA MOJA WEWE NI MOTO AU BARIDI HATUTAKI VUGUVUGU HAPA
 
wana jf
nikiwa kama mkereketwa na mfuasi wa dr slaa nazidi kuhamasisha wanachama na wapenzi wa chadema asilia kufuata na kuenzi mawazo ya kamanda wetu wa ukweli ambaye tunapaswakujiuliza yafuatayo;

1) ni kwa nini mchakato wa kutafuta mgombea urais haukufuatwa kama ilivyokuwa imepangwa.

2) ni kwa nini mtu amechukua takribani wiki 2 tu tangu alipohamia kutoka ccm na kuteuliwa kuwa mgombea urais.

3) ni kwa nini viongozi waandamizi makamanda walitupwa nje hivihivi bila kuthamini michango yao.

4) ni kwa nini yule fisadi mkuu kutoka ccm kama mlivyokuwa mnatuhubiria na kupitia magazeti ya mwanahalisi pia tuliamua kumkumbatia. Ni nani alimsafisha ?

5) ni kwa nini viongozi wetu mliamua kuwachukua makapi yote kutoka ccm wakati mliapa hamtachukua tena makapi kutoka ccm.

6) makamanda mnazungumzia mfumo gani huu wa ccm ambao ni mbaya na ukilinganisha na limfumo baya zaidi kupita yote niliyotaja hapo juu. Tunaweka misingi gani ya utawala bora ?

Tafakari chukua hatua haraka !!

tapeli
 
Kamanda nadhani ungeanzisha topic ya ccm then ukaongelea mambo yako hayo. Huku hayatuhusu. Kama wewe ccm basi hapa umepotea.
Nasema chadema asilia tunajiandaa na matukio hasa baada ya uchaguzi mkuu. NI LAZIMA TUTASHINDWA HILO HALINA UBISHI. Kitu kikubwa ambacho kitatufanya tushindwe nadhani kila mtu anakifahamu wala siyo siri ya kuficha. Kukumbatia MAFISADI. HAPO NDIPO TUMEPOTEZEA MWELEKEO. kama ni ndege ikishapoteza mawasiliano basi inaenda kuanguka hakuna namna. Chadema au ukawa hivyo hivyo inaenda kuangukia pua. Hivi sasa ipo speed 360 inaelekea shimoni. Hakuna atakayeweza itoa shimoni labda makamanda wetu Dr Slaa na Prof Lipumba warudi ulingoni. Kama sivyo tunaona kabisa baada ya uchaguzi tumeshajichimbia kaburi! Hakuna kukwepa. Hapo ndipo tutakapoona mafisadi wakitukimbia baada ya mission yao kuwa imetimia. (Mission accomplished ).
Nimeshindwa kukujibu miezi miwili toka ujoin humu naona kama nitapot muda wangu
 
tuko pamoja nasubiri tar25 lazima waadhibiwe wanatufanya sisi mazuzu. Miaka yote hii tunayumba na chama leo gafla bin vuuuuuu tena kwa kuvunja na kuvuruga katiba na taratibu zote na michakato ya kumpata mgombea na anapewa kugombea urais tena siyo wa chama tu wa vyama vyote, tutaendelea kuhoji nini kilitokea na tunasubiri tr25 tukiadhibu chama alafu mny/k atatueleza vizuri ilikuwaje kuaje yale tuliyokubaliana yakavunjwa na hili balaa kutoka ccm. Kufaidi miga...... Wafaidi wao, sisi tuambulie kuwasindikiza ikulu, nani kasema..... Tar25 ifike haraka. Ninahasira sana watu walivunjwa mikono kwaajili ya chama leo wanaoneka hamnazo kweliii........!! Kweliii......!! Ahaaa....!!


unajipendekeza anakujua nani chadema weye... Yashinda sumaye pamoja na uwaziri mkuu kahama chama ni wewe bana ...fungasha virago nenda lumumba kwenye maslai binafsi ...sie tunawapa wananchi kitu wanatakaga nayo ni...mabadiliko
 
Sasa wewe kioo chako ni Dr. Slaa..bado unafanyanini chadema and then unajiita chadema asilia..waachie watu chama chao lala mbele kama Dr Mihogo alivyofanya...
 
msimamo wangu binafsi sitaki unifuate wala si kushauri ubadirishe wako, siwezi kuunga mkono ufisadi au kumuunga mkono fisadi, bado sijaona hoja nzito kutoka kwa Lowasa au wapambe wake ya kuwaridhisha watanzania

SASA KAMA KWELI UNAITAKIA CHADEMA MEMA SI UNGESUBIRI UCHAGUZI UISHE? UNAVOJITAHIDI KUPONDA NI KWASABABU UNAONA CHADEMA ITASHINDA NA WEWE UTAKUWA UMEPOTEZA NDO MAANA UNAJITAHIDI KUIPIGIA CCM KAMPENI?
kUNA VYAMA VINGI KAMA HAUKO NA CHADEMA SASA HAUHITAJI KUWA NAYO BAADA YA UCHAGUZI TAFUTA CHAMA KINGINE TU MBONA VIKO VINGI? HATA CCJ NASIKIA ITARUDI BAADA YA CCM KUSHINDWA ..ALL THE BEST HUKO UNAWEZA KUWA NA NAFASI YA KUFANYA MAAMUZI YAKO..
 
Na hizo ni sababu tosha kwa nini kura yangu sitawapigia. I'd rather vote for Magufuli, sio hao makamanda hata sera hawana!!!!
 
Kwenda zako gamba ww mnafiki mkubwa cdm hawana elemnt kama zako are u pretending?
 
Jamani msimpe Slaa haki maana aliacha wito wa kulisha kondoo wa Bwana mpaka akawaka tamaa akaoa kinyume na maadili ya wito alioukubali na kuutumikia. Kikubwa msijifiche nyuma ya Dr. Slaa kuichafua Chadema nani kawalazimisha kubaki Chadema sepeni basi msituvuruge. Eti Chadema Asilia??? Hivi kama ww Chadema unaweza kweli kuishabikia CCM kisa Slaa?? Mashetani nyie.
 
msimamo wangu binafsi sitaki unifuate wala si kushauri ubadirishe wako, siwezi kuunga mkono ufisadi au kumuunga mkono fisadi, bado sijaona hoja nzito kutoka kwa lowasa au wapambe wake ya kuwaridhisha watanzania
tatizo kubwa cdm viongozi wetu na wanachama wetu wanaangalia mbele tu hawahui kuwa kushinda ni mikakati.walichojua lowasa ana wafuasi wengi madhila mengine wakasahua.hata wale wenye upeo mkubwa waipotahadharisha walionekana wanachelesha safari wakatupwa nnje.sasa wameanguka vibaya hawajui kilichowaangusha wanatoa visingizio dhaifu kuibiwa kura
 
Chadema asili wapi wewe mnafiki tu. Uasili wako ni nini, unajitokeza leo.

Dr namtafsiri kama aliyeasi mageuzi aliyoyapanda na kukuza kwa muda mrefu.

Kwa kuwa wewe mleta Mada ni mfuasi wake basi staafu maana Dr amestaafu.
 
Wadau na wanye mapenzi mema na chadema asilia. Tunawashukuru wote ambao waliamua bila unafiki kumpigia kura Dr Magufuli na hasa kwa kuzingatia ushauri wa Dr Slaa na Prof Lipumba. Allah awabariki makamanda hawa!
Kama tukivyokubaliana chadema asilia tunawataka viongozi wote waliopo sasa kujipima na kuachia madaraka ili chama kiundwe upya vinginevyo uchaguzi ujao utafika tukajikuta hatujapiga hatua yoyote.
Ujio wa Dr Slaa sasa utakuwa chachu ya mabadiliko ndani ya chadema. Tunategemea mafisadi tuliowapokea chadema wataondoka wakati wowote na kwenda walipotoka au kuanzisha chama chao. Baada ya hapo tutamwomba sasa Dr Slaa arudi kundini kuongoza jahazi jipya. Asalaam aleikhum
 
Back
Top Bottom