Msimamo wetu sisi CHADEMA asilia

Msimamo wetu sisi CHADEMA asilia

Kama kweli wewe ni mwanaCHADEMA basi hufai kama asivyofaa huyo Dr Slaa, mna vikao vya Chama halafu unakuja huku na uharo wa kipindupindu! utakuwa mamluki huko, sio bure.

Vikao vya Chama vilifanyika lini mara ya mwisho?
 
hhahahahahahah CCM fanyeni mambo yenu bana tumemkubali lowasa kama nyie ni chadema asilia anzisheni chama chenu slaa is no longa chadema so hiyo asilia sijui ya wapi hahahahahah CCM wameshikwa kweli. Jiitwni chadema mliostaafu
 
Unapoona mtu anadhubutu kunyanyua mdomo wake huku akimsifu lowasa kua nikamanda na akimtuhumu dr.slaa kua ametumwa na CCM mtu huyo muangalie kwa jicho la tatu. Watu wanahoji vitu vya msingi wewe unakuja na tuhuma zako ambazo hazina hata kamshiko. Lowasa amewalisha nini nyinyi? lowasa shida yake yeye awe rais na sio kutatua kero za watanzania kamaanavyo jinasibu kwenye majukwaa. Angekua ana nia ya kutatua asingetuibia kias hicho. Kama lowasa alikua anaona CCM, mfumo wake ni mbaya na hakuna demokrasia kwanini walichukua fomu ya urais? watanzania ifike mahali tuziache akili zetu zifanye kazi natupunguze mihemko ya vyama vya siasa "Politician ain't humanitarian" tunakazi ya kuijenga Tanzania yetu. Epuka matapeli
Kwa hiyo unataka kusema hujui kuwa watz wameichoka CCM na MFUMO WAKE PAPA WA KIFISADI hivyo wanahitaji mabadiliko? Alikuwa sahihi kuchukua fomu kwa sababu hakuwa na sababu ya kuhama CCM.Kwa sasa cha msingi ni kuing'oa CCM na MFUMO WAKE WA KINYONYAJI then mengine baadae
angalau tuokoe rasilimali zilizosalia kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho!
 
Tunatawaliwaje na chama kimoja miaka hamsini bwanaaaa.DELETE CCM TUIJENGE TANZANIA MPYA!
 
wana jf
nikiwa kama mkereketwa na mfuasi wa dr slaa nazidi kuhamasisha wanachama na wapenzi wa chadema asilia kufuata na kuenzi mawazo ya kamanda wetu wa ukweli ambaye tunapaswakujiuliza yafuatayo
1) ni kwa nini mchakato wa kutafuta mgombea urais haukufuatwa kama ilivyokuwa imepangwa.
2) ni kwa nini mtu amechukua takribani wiki 2 tu tangu alipohamia kutoka ccm na kuteuliwa kuwa mgombea urais
3) ni kwa nini viongozi waandamizi makamanda walitupwa nje hivihivi bila kuthamini michango yao
4) ni kwa nini yule fisadi mkuu kutoka ccm kama mlivyokuwa mnatuhubiria na kupitia magazeti ya mwanahalisi pia tuliamua kumkumbatia. Ni nani alimsafisha ?
5) ni kwa nini viongozi wetu mliamua kuwachukua makapi yote kutoka ccm wakati mliapa hamtachukua tena makapi kutoka ccm.
6) makamanda mnazungumzia mfumo gani huu wa ccm ambao ni mbaya na ukilinganisha na limfumo baya zaidi kupita yote niliyotaja hapo juu. Tunaweka misingi gani ya utawala bora ?????
Tafakari chukua hatua haraka !!

makamanda tumekerwa sana nautaratibu uchwara huu uliotumika kumleta pwagu huyu alie tufilisi,mimi kama kamamnda na mkereketwa wa dr slaa sitamchagua mwizi,ntakuwa naisalitinafsi yangu,ntakuwa nasaliti kile ninacho kiamini,nitakuwa naisaliti elimu yangu na nitakuwa ni mpuuzi wa kile nilichokua nategemea kwa ajili ya taifa langu,kumchagua mwizi,fisadi,na kibaka kisa kubadili chama,hpana sitafanya hivyo.nitamchagua magufuli kwa sababu ni mzalendo na mtendaji na siyo kuidhulumu nafsi yangu
 
Safi sana kamanda kwa kujitambua, hata mimi ni chadema siwezi kuuza utu wangu kisa feza anazotoa mzee lowasa. Nipo pamoja na Dr SLAA

Kama mnamuunga mkono achaneni na siasa kama yeye. Mwenzenu amesha fanya biashara nakuchukua chake nyie mnabaki na kelele.ACHENI HIZO...MABADILIKO HAYAZUILIKI NI POPOTE HATA NDANI YA CHADEMA.
 
Hilo liko wazi bado wapo wanachadema wengi tu ambao wanasimamia misingi ya Chadema asilia, sio hii ya Mbowe kubadili gia angani na kuuza chama.

Wagombea ubunge na udiwani wa Chadema, wengi sasa wanapigania maslai yao kwa maana ya viti wanavyoviwania.

Utashangaa baada ya uchaguzi dharau za wabunge zitavyoibuka dhidi ya Chama, ule utiifu kwa chama wote umeisha, Na mpaka sasa ndani ya Chadema hakuna wa kusimamia wala kufuatilia maendeleo ya wagombea majimboni zaidi ya wao wenyewe kukuruka.

Sasa hivi huwezi kuona umoja kama ule wa awali, wabunge kusaidiana kwenye majimbo, mbunge wa jimbo A kwenda kusaidia mgombea wa jimbo B.

Nakumbuka 2010 wabunge wengi sana kama sio wote walitembeleana majimboni, kupeana nguvu na kubadilishana uzoefu lakini leo kila mtu na lwake.

Sasa hivi hakuna vikao vya kamati kuu kujadili mwenendo wa kampeni , ila Kuna vikao vya Mbowe na Team Lowassa.

Hakuna matamko ya Chama, ila Kuna matamko ya team Lowassa, Mbatia akiwa akitangulizwa mbele kama kondoo wa kafara.

Yuko wapi John Mnyika Naibu katibu mkuu Bara, yuko wapi Tumaini Makene msemaji wa Chama, Salumu Mwalimu ni kama anaburuzwa tu , japo alizunguka Tanzania nzima na watu tukamwelewa kuwa kijana ni hazina ya chama lakini leo kapotelea wapi? hatujui pengine nafsi inamsuta kwa kutenda asiyoyaamini.

Kwa kweli bado naiota Chadema yangu ya awali, Chadema ya kujitolea, Bila kujali gharama ama muda.

Japo sijui itarudi lini lakini bado naiota, Chadema ya makamanda wa ukweli sio hao wa sasa wa plastic.

Chadema ya Silinde, Lema, Sugu , Wenje, Lisu, Mdee, Mnyika, Msigwa wakiongea utapenda uendelee kuwasikiliza.

Na ndio waliochangia vijana wengi kujikita kwenye siasa kuanzia serikali za mitaa mpaka ubunge, sasa hivi si ajabu kijana wa miaka ishirini ni mwenyekiti serikali za mitaa, Madiwani ndio kabisa vijana wadogo kabisa ndio wanawania.

Ila hii Chadema ya Sumaye, Masha, Babu duni, duh!! Mungu atunusuru.

Chadema itaendelea kuwa Chadema tu viongozi watapita kama ilivyokuwa kwa Kabouru, Zitto, Arfi na sasa ni Slaa wote walikwenda na wafuasi wao Chama kimeendelea na kitaendehayo Katika mfumo wa kidemokrasia aliyekuja Jana na aliyekuja juzi wote wanapewa nafasi sawa ndivyo Chadema imekuwa ikifanya na ndio maana umeona chama kimekua, Kauli kama " Chadema asilia" ni kauli za kugawa chama ambazo zinaletwa na watu wanaoutumwa na chama tawala kuvuruga Chadema. Chadema hakuna Chadema asilia na Chadema nyingine hata waasisi wa Chadema hawajipachiki majina hayo Chadema itaendelea kuwa ya wote wenye mapenzi mema na chama. TUNASIMAMA NA TUTASHINDA.
 
DAH MIMI jamani nimechoka , nimechoka mie tena sana tu. vilio haviishi kila uchao wananchi wanalia wanadai bora ya jana kuliko leo. Kama vile viongozi hawasikii wala kuelewa vilio vya wananchi wanazidi kutonesha vidonda na majeraha ya ugumu wa maisha kwa kauli za kebehi ati "malofa na wapumbavu, kapigeni mbizi kama hamna nauli, ati wingi wa magari na foleni zake ni utajiri, kama hampati maji mnamezea nini dawa?, pesa za mboga". Hivi watanzania nawauliza na tafadhalini nijibuni, ati nyie ni kwamba ni wavumilivu sana? Waoga sana, Mmezeoea shida? Hamjitambui au tumeumbwa kuteseka?

Hospitalini twalazwa watatu, ikiwa wajawazito basi tuhesabu watu sita kwenye kitanda cha 4 kwa sita! dawa hakuna, sio siri maskini anakufa kwa kukosa elfu 2000 tu. Asiyekuwa nacho ndio analimwa kodi kubwa, bali mwenye nacho anapeta tu babake yaani anaiona Tz kama imewekewa kiyoyozi wakati maskini anaiona Tz kama tanuru la moto.

Auwiiiiiiii uuuiiiiiiiiiiii naumia mimi jamani, Eee Mwenyenzi Mungu waongoze watanzania kufanya chaguo sahihi.
 
Hamuwezi kuzuia mabadiliko kwa kuleta maigizo hapa!Ninyi masisiem halafu mnaigiza eti Chadema asilia!mmechoka kuandamana sasa mnakuja hapa na staili nyingine!
 
ni muhimu kutambua Nguvu ya upinzani na siyo Nguvu ya chadema. Umoja ni Nguvu , utengano ni dhaifu. Kwa hiyo twende mbele na tuone ukubwa wetu na mapungufu yetu ndani ya Ukawa, kumbuka kampeni za miaka ya nyuma , dhihaka kubwa ya CCM ili kuwa udini, kuwa chadema ni wakristo, na CUF Waisilamu, umeona tumeungana imekufa, hawa shambulii vyama tena wanamshambulia mtu - lowassa
na issue ni ufisadi, nadhani bidiii kubwa iwe kwenye hiyo. Fisadi kwa nini hawampeleki mahakamani, wenyewe wana usafi gani, escrow etc

Pongezi sana ndugu pia wanaojiita chadema asilia ni ccm ndo sasa wanajigeuza kuuaminisha umma wa watanzania kuwa kuna kundi hlo na chadema imemeguka
 
Tangu hawa wageni wamehamia chadema ni aghalab wao kujibu hoja .jibuni hoja za mtoa mada
 
Wana jf
Nikiwa kama mkereketwa na mfuasi wa Dr Slaa nazidi kuhamasisha wanachama na wapenzi wa chadema asilia kufuata na kuenzi mawazo ya kamanda wetu wa ukweli ambaye tunapaswakujiuliza yafuatayo
1) ni kwa nini mchakato wa kutafuta mgombea urais haukufuatwa kama ilivyokuwa imepangwa.
2) ni kwa nini mtu amechukua takribani wiki 2 tu tangu alipohamia kutoka ccm na kuteuliwa kuwa mgombea urais
3) ni kwa nini viongozi waandamizi makamanda walitupwa nje hivihivi bila kuthamini michango yao
4) ni kwa nini yule fisadi mkuu kutoka ccm kama mlivyokuwa mnatuhubiria na kupitia magazeti ya mwanahalisi pia tuliamua kumkumbatia. Ni nani alimsafisha ?
5) ni kwa nini viongozi wetu mliamua kuwachukua makapi yote kutoka ccm wakati mliapa hamtachukua tena makapi kutoka ccm.
6) makamanda mnazungumzia mfumo gani huu wa ccm ambao ni mbaya na ukilinganisha na limfumo baya zaidi kupita yote niliyotaja hapo juu. Tunaweka misingi gani ya utawala bora ?????
Tafakari chukua hatua haraka !!


Unafiki 100% umekusukuma kuandika ulichoandika.






Slaa yuko CCM mfuate huko wewe na masalia wenzako.
 
CHADEMA ASILI wala wasiwe na shaka; wakae tayari kukirudisha chama mikononi mwao kuanzia tarehe 26 ya mwezi ujao. Kwanza, watu wajiandae kusikia hawa waliokiuza chama watakapoanguka kwenye majimbo yao halafu na mtu wao atakapokataliwa mara ya pili na Watanzania wengi zaidi. Na litakuwa funzo zito kwa wanasiasa wetu; waache kuchezea hisia za Watanzania na hatima yao. Hivi walianzaje? Hata sijui...
 
Unapoona mtu anadhubutu kunyanyua mdomo wake huku akimsifu lowasa kua nikamanda na akimtuhumu dr.slaa kua ametumwa na CCM mtu huyo muangalie kwa jicho la tatu. Watu wanahoji vitu vya msingi wewe unakuja na tuhuma zako ambazo hazina hata kamshiko. Lowasa amewalisha nini nyinyi? lowasa shida yake yeye awe rais na sio kutatua kero za watanzania kamaanavyo jinasibu kwenye majukwaa. Angekua ana nia ya kutatua asingetuibia kias hicho. Kama lowasa alikua anaona CCM, mfumo wake ni mbaya na hakuna demokrasia kwanini walichukua fomu ya urais? watanzania ifike mahali tuziache akili zetu zifanye kazi natupunguze mihemko ya vyama vya siasa "Politician ain't humanitarian" tunakazi ya kuijenga Tanzania yetu. Epuka matapeli

Tunachotaka ni mabadiliko ya kuiondoa ccm madarakani. Hata Ukawa wangeweka jiwe tumeichoka ccm na mfumo wao wa kuliibia taifa na kulindana.
 
Dr slaa atabaki ngao ya kupinga ufisadi hasa kumpinga Lowasa waziwazi.
 
Back
Top Bottom