Msimamo wangu

Msimamo wangu

Sijui ni huu msimamo ndio wanauogopa au ni hicho alichozungumzia huyo jamaa hapo juu kuwa pesa sina na sura sina atanitaka nani
hv bado hujalegeza masharti? mwaka wa 5 huu ujue
 
espy aje hapa athibitishe kwa umma wa jf, miaka mitano sio haba na mengi yamekuwa upside down. Aseme je huu msimamo wake bado upo. Ingekuwa vizuri kama ungeeleza your current marital status...

Kama ulikuwa 25, sasa upo 30.. kama ulikuwa 28 manake age is really catching up now...

Hii misimamo kwa sisi wenye nature ya ubahili haitufai kabisa
 
Mm niko mbali kabsa huku mporoto tukuyu
MSIMAMO WANGU

1. Changu ni changu, cha mume/mpenzi wangu tunashea.

2. Mwanaume bahili akae mbali na mimi.

3. Sina huruma na pesa ya mwanaume, labda atakaekuwa mume wangu wa ndoa.

4. Ntafanya majukumu yote kama mpenzi/mke wake, lakini when it comes to my money asahau, imeandikwa "mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho" so let him provide.

5. Ni marufuku mambo ya joint a/c eti mmoja wetu anaweza kutoa pesa pasipo saini ya mwingine sitaki.

6. Pesa zangu ni zangu ata password simpi, bora nimpe Mama yangu ata nikifa ajifutie nazo machozi.

7. Hata kama nina pesa kuliko yeye, mwanaume ni lazima awajibike, sio pesa yake awanufaishe wengine, maana kuna wanaume ndani wabahili ila nje wanahonga balaa.

8. Nyumba tutasaidiana kujenga, na itakuwa na jina langu au kama tutakuwa na watoto nao tutawaweka humo. Kaka tayari unayo/unazo basi uhakikishe zinakuwa na majina ya watoto pindi tutakapowapata.

9. Ni marufuku ndugu wa mume kujihusisha na mali zetu, narudia tena ni marufuku ndugu wa mume kujisogeza karibu na mali zangu mm na mume wangu! Hizi haziwahusu kabisa tena mkae mbali.

10. Nikitangulia mbele za haki kabla yako ole wako uoe mwanamke mwingine, nitakutokea ndotoni hadi ujute.

NIMEMALIZA
 
espy aje hapa athibitishe kwa umma wa jf, miaka mitano sio haba na mengi yamekuwa upside down. Aseme je huu msimamo wake bado upo. Ingekuwa vizuri kama ungeeleza your current marital status...

Kama ulikuwa 25, sasa upo 30.. kama ulikuwa 28 manake age is really catching up now...

Hii misimamo kwa sisi wenye nature ya ubahili haitufai kabisa

Yaani bado bila bila ex darling, hapa nina mpango wa ku-update niongezee misimamo zaidi maana naonana hiyo ilikuwa michache, ikifika 20 itapendeza.
 
Yaani bado bila bila ex darling, hapa nina mpango wa ku-update niongezee misimamo zaidi maana naonana hiyo ilikuwa michache, ikifika 20 itapendeza.
sidanganyiki.

Hapo umeamka kunyonyesha baby wako, then saa tisa tena utaamka. Bado chako ni chako tu? Isije kuwa mshahara wako jamaa ndio anauchukua kupangia matumizi ya home
 
Back
Top Bottom