Ajali mbaya iliyobeba roho ya mpendwa wetu Chacha Wangwe ili ilazimu tume ya uchaguzi kuitisha uchaguzi mdogo kuziba pengo la marehemu.Mapambano yalianza kama ilivyo sas katika jimbo la Arumeru.Tuache maneno mengi ngoja nikupe yaliyotokea wakati wa matokeo ya mwisho.
Ilikuwa hivi matokeo yalikuwa yanaonyesha CHADEMA imeshinda, lakin Mh(mume wa mwana mama machachari mbunge pale Bungen) alimtishia Mkurugenzi wa wakati huo na kumlazimisha aseme CCM imeshinda na kama atatangaza CHADEMA imeshinda Mkurugenzi atapoteza kazi.Kweli Mkurugenzi alisimamia msimamo wake wa kusimamia ukweli na haki na alitangaza CHADEMA kuwa mshindi.
Baada ya muda mkurugenzi huyo aliletewa barua yakusimamishwa kazi, kwa vile aliamini Mungu yu pamoja nae alifungua kesi mahakaman ambayo baada ya muda ilionekana hana hati na kurudishwa kazini,ila tu alihamishwa kituo na kupelekwa ARUMERU MASHARIKI ambapo ndio anasimamia uchaguzi mdogo.
Nikiripoti kutoka hapa Usa River mji mkuu wa jimbo letu tukufu ni mim Sunguratope wa jeifuuuuuuuuuuuuuu.