Msimamizi wa uchaguzi Arumeru anastahili

Msimamizi wa uchaguzi Arumeru anastahili

Ritts

Senior Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
136
Reaction score
33
Huyu ni Trasias kagenzi,Alisimamia uchaguzi mdogo tarime mwaka 2008 ivyo kuonyesha kuwa ana uzoefu usiotiliwa shaka.CCM mkimkataa huyu basi mnakimbia kivuli chenu.
 
huyu mkurugenzi ni mmojawapo ya wakurugenzi mahiri,wapole na wapenda haki lakini hila za ccm zinaweza kumfanya atoe maamuzi ambayo si sahihi.kama una kumbukumbu jiulize baada ya uchagui wa huo wa tarime nini kilimtokea?nina uhakika kuwa wananchi wa meru wanamkubali sana tu na maamuzi yake yataakisi mahitaji ya wanameru na hayataathiriwa na itikadi za chama
 
kwani alifanywaje baada ya uchaguzi mdogo tarime? Halafu hakufanya mizengwe uchaguzi wa 2010? Isije ikawa ni mbwamwitu mwenye sura ya kondoo!
 
Hakuna hata Jimbo moja ambalo CCM wamewahi kulalamikia utendaji wa msimamizi wa uchaguzi. Siku zote ni wapinzani ndio huwa watu wa kulalaka lalamika.
 
Kengemaji rudisha kumbukumbu nyuma,ccm walalamishi wakuu wakipigwa bao
 
kwani alifanywaje baada ya uchaguzi mdogo tarime? Halafu hakufanya mizengwe uchaguzi wa 2010? Isije ikawa ni mbwamwitu mwenye sura ya kondoo!

Swali zuri sana Jackbour hebu tupe jibu.
 
Hakuna hata Jimbo moja ambalo CCM wamewahi kulalamikia utendaji wa msimamizi wa uchaguzi. Siku zote ni wapinzani ndio huwa watu wa kulalaka lalamika.

Huwa hawalalamiki wazi wazi ila wanajua jinsi ya kumshughulikia muhusika. Ila walishawahi kulalamika mwaka 1995 wakati wa Salmini. Kuna mtu mmoja anaitwa Ally Ameir ndiye aliyelalamika lakini wanajua matokeo wlivyoyafanya
 
hakuna hata jimbo moja ambalo ccm wamewahi kulalamikia utendaji wa msimamizi wa uchaguzi. Siku zote ni wapinzani ndio huwa watu wa kulalaka lalamika.

we mgonjwa hata habari za hii nchi huna!kaa kimya!
 
Hakuna hata Jimbo moja ambalo CCM wamewahi kulalamikia utendaji wa msimamizi wa uchaguzi. Siku zote ni wapinzani ndio huwa watu wa kulalaka lalamika.
Wacha ushabiki, kwani nini kipo pale Arusha?
 
Hakuna hata Jimbo moja ambalo CCM wamewahi kulalamikia utendaji wa msimamizi wa uchaguzi. Siku zote ni wapinzani ndio huwa watu wa kulalaka lalamika.

ccm watakuwa wehu kama watalalamikia wasimamizi wa uchaguzi waliowaweka wenyewe!!tume yao wasimamizi wanateuliwa na ccm sasa walalamikie nini tena??
 
Ajali mbaya iliyobeba roho ya mpendwa wetu Chacha Wangwe ili ilazimu tume ya uchaguzi kuitisha uchaguzi mdogo kuziba pengo la marehemu.Mapambano yalianza kama ilivyo sas katika jimbo la Arumeru.Tuache maneno mengi ngoja nikupe yaliyotokea wakati wa matokeo ya mwisho.

Ilikuwa hivi matokeo yalikuwa yanaonyesha CHADEMA imeshinda, lakin Mh(mume wa mwana mama machachari mbunge pale Bungen) alimtishia Mkurugenzi wa wakati huo na kumlazimisha aseme CCM imeshinda na kama atatangaza CHADEMA imeshinda Mkurugenzi atapoteza kazi.Kweli Mkurugenzi alisimamia msimamo wake wa kusimamia ukweli na haki na alitangaza CHADEMA kuwa mshindi.

Baada ya muda mkurugenzi huyo aliletewa barua yakusimamishwa kazi, kwa vile aliamini Mungu yu pamoja nae alifungua kesi mahakaman ambayo baada ya muda ilionekana hana hati na kurudishwa kazini,ila tu alihamishwa kituo na kupelekwa ARUMERU MASHARIKI ambapo ndio anasimamia uchaguzi mdogo.

Nikiripoti kutoka hapa Usa River mji mkuu wa jimbo letu tukufu ni mim Sunguratope wa jeifuuuuuuuuuuuuuu.
 
Kama ni kweli anaweza kuhamishwa kabla ya uchaguzi.
 
nina uhakika atasimamia haki kama walimfukuza na akaenda mahakamani akarudishwa kazini. huyo sio mnyonge anajua anachofanya.
 
...huyo ni mtu hatari sana kwa M.A.G.A.M.B.A na ni rafiki mkubwa wa HAKI,labda kama baada ya kuamia huko Arumeru alimwacha Mungu huko Tarime...
 
Magamba hawampendi mtu anayesimamia haki. Unayakumbuka ya Kenya kati ya Kivuitu na Kibaki?. Tuwe makini yasije yakatokea na hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom