Msimamizi wa uchaguzi Arumeru anastahili

Nimemuona mkurugenzi wa Arumeru na msimamizi mkuu TBC Akisisitiza watu watawanyike baada ya kupiga kura.
Sheria ya uchaguzi zinasema watu wakae umbali wa mita miamoja.
Hivi hili la kulazimika kwenda nyumbani kalitolea wapi?
Wapo wanaosema wakae umbali wa mita miambili hili ni kwasheria ipi?.
Nasisitiza wananchi wote wanahaki ya kujua kinachoendelea katika vituo vya kupiga kura na usalama wa kurazao. Sheria ilitambua hilo ndiomaana ilisema watu wakae kwa utulivu umbali wa mita mia. kwanini wanaotoa kauli za kupinga sheria halali za uchaguzi wasishitakiwe?. Na imefika wakati tume ya uchaguzi iwe na wafanyakazi wake kama taasi na si kutumia wakurunzi wa wilaya.
 
Nimemuona mkurugenzi wa Arumeru na msimamizi mkuu TBC
Akisisitiza watu watawanyike baada ya kupiga kura.
Sheria ya uchaguzi zinasema watu wakae umbali wa mita miamoja.
Hivi hili la kulazimika kwenda nyumbani kalitolea wapi?
Wapo wanaosema wakae umbali wa mita miambili hili ni kwasheria ipi?.
Nasisitiza wananchi wote wanahaki ya kujua kinachoendelea katika vituo
vya kupiga kura na usalama wa kurazao. Sheria ilitambua hilo ndiomaana
ilisema watu wakae kwa utulivu umbali wa mita mia. kwanini wanaotoa
kauli za kupinga sheria halali za uchaguzi wasishitakiwe?. Na imefika
wakati tume ya uchaguzi iwe na wafanyakazi wake kama taasi na si
kutumia wakurunzi wa wilaya.

kuna vingine ni swala la kutumia common sense tu. hivi kila anaepiga kura akibaki kituoni patatosha?
 
Hii inanikumbusha mwaka 2008 katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime ambapo Mkurugenzi huyuhuyu Bwana Kagenzi alimtangaza Charles Nyanguru Mwera wa Chadema kuwa mshindi dhidi ya Christopher Ryoba Kangoye wa CCM. Na sasa ni Nassari dhidi ya Sioi wa CCM. Inawezekana jamaa ana msimamo au ni coincidence tu?
 
Huyo mkurugenzi kuhojiwa na Magic FM akasema "huku mambo shwari kabisa"
 
Bw. Kagenzi ni msimamia Haki. Baada ya Uchaguzi wa Tarime; Kagenzi alizushiwa kesi na kusimamishwa kazi. Mahakama ilimrejesha kazini. Baadaye akahamishiwa Arusha. Sasa sijui itakuwaje kwa kosa hili la kutangaza CDM washindi. Tumuombee Mungu amzidishie ujasiri.
 
Wakimuonea huyo mtu kwa kutangaza haki patachimbika CDM inatakiwa tuwahakikishie ulinzi watu kama kagenzi dhidi ya mafisadi.
 
  • Thanks
Reactions: TKO
Kagenzi aliishi na Tarime na akajifunza tabia ya kutopindisha mambo, jambo ambalo wengi wetu tuliowahi kufanya kazi huko tumejifunza pia. kule mbwai mbwai! kijiko ni kijiko na sepetu ni sepetu!! kama hutaki sio juu yao. Sasa sijui na huku pia watamzushia kesi sijui wampeleke wapi!? niliwaambia jamaa zangu kuwa wasitarajie Kagenzi angekubali kuchakachua kitu.
 
Mkweli siku zote atasimamia ukweli anaouamini pasipo shaka. Ccm kwa chuki hawajambo, si unamkumbuka yule mkurugenzi wa Arusha mjini (Mbunda) baada ya kumtangaza Lema mshindi wa uchaguzi jimbo la Arusha mjini sasa hv huyu jamaa yupo kwetu NAMTUMBO analima karanga.
 
Sawa wanafikiri kwa kumpeleka Mbunda Namtumbo wanamuadhibu kume ndio wanampeleka karibu na nyumbani!!
 
Trasias Kagenzi ameendelea kujizolea sifa kwa kusimamia chaguzi ndogo mbili bila kukipendelea chama tawala. Mwaka 2008 alikuwa msimamizi mkuu huko Tarime, CHADEMA kikashinda. Akahamishiwa Arumeru, uchaguzi mdogo umefanyika na CHADEMA wameshinda tena.

Ninavyoona, na ninavyojua fitina za chama tawala, Kagenzi hatahamishwa tena kwa kuhofia kuwa atakapohamishiwa uchaguzi mdogo utaitishwa na CHADEMA kitashinda.

Bravo Kagenzi kwa kusimamia haki.
 
Na akawe chachu kwa NEC nzima!
 
Bravo wakazi wa Arumeru kwa kujitokeza kupiga kura na kulinda kura zao!

Hiyo ndio ilikuwa success story!!
 
Nilianza kuwa naimani na Kagenzi mapema kwani alipotakiwa kuhojiwa na waandishi hakuwa na papara za wizi kam yule wa Igunga kagenzi ni mwanamapinduzi aliye katika utawala dhalimu.
 
Kilichotokea hapa ni kwamba CCM wamepigwa kwa Knock out, so isingewezekana kuwabeba hata kwa mbeleko ya chuma.
 
Hakutaka damu imwagike kwa kubadili mambo ndivyo sivyo, Haki ya aliye na haki yeye huitoa bila upendeleo.
 
Back
Top Bottom