Msikiti wa posta na ubaguzi??

Utaje huo msikiti, nikiujua nitaenda Ku volunteer kuzuia vibaka wanaoenda misikitini kuiba matalawanda na makubasi
 
Logical consistence inakujaje? usichoelewa ni kuwa having power to do smething hailazimishi kufanya kitu hicho. kuna several reasons behind doing or not doing s.thing, is not just a matter of power. uwe unaleta facts sio fallacies, sawa?
 
Msikiti wa Manyema kuna mtu aliwahi kurusha ngumi pale, kuna watu wa familia flani weupe walishajiwekea kuwa swafu ya mbele ni ya kwao, so wewe kanjangaz ukifika pale unatakiwa ukae ya pili hata kama ya kwanza haijajaa...

Uislamu hauruhusu kufanya "reservation" ya mstari wa kusimana katika ibada.

Huku Asia, Waislamu wa kike wanafanya ibada na full make up, kama wanakwenda harusini.
Nilipowauliza, wakajibu, kama unakwenda kuonana na Mola wako, lazima upendeze saa zote.

Huko Afrika, kutumia manukato/ perfume ni mwiko kwa wengi. Vinuka Vikwapa vinakata stimu ya kusali kwa kweli.

Sababu moja naswali msikiti wa Kishiia badala wa Kisunni ni kuwa kuna vinuka vikwapa wachache sana katika msikiti wa Kishiia.

Labda hao jamaa hawataki kusali na vinuka vikwapa, japo hairuhusiwi kidini kubagua.
 
Nijuavyo mimi Posta kule kuna Msikiti wa Ngazija na Ocean Road (nisahihishwe), ni upi kati ya hiyo!
 
Wewe sio katika imani ! Unajua mtume wetu ametuamlisha mini?
 
Msikiti wa Manyema kuna mtu aliwahi kurusha ngumi pale, kuna watu wa familia flani weupe walishajiwekea kuwa swafu ya mbele ni ya kwao, so wewe kanjangaz ukifika pale unatakiwa ukae ya pili hata kama ya kwanza haijajaa...
Innalillah!Waislam tumefikia stage hii?
Wanasali nini hao watu wa hiyo familia?
Aiseee siku nikiingia msikiti wa aina hiyo nami lazima nizirushe...
 
Yote nina haki ya kuswali tatizo Huduma wanatoa kibaguzi, hawasemi bali matendo tu
Labda ulitaka kunyakuwa Micro-phone utoe khutuba... au ulitaka kuiba viatu ?!!? maana kila msikitini nchini unao utaratibu wake na Viongozi walioteuliwa na Chama tawala na kuwapa masharti ya kuto ruhusu mgeni yeyote kujipenyeza na kushawishi waUmini....
Msikiti ina Muadhini na Imamu kama una hoja/shaka/maulizo/shida/ onana nao hao !!
 
Innalillah!Waislam tumefikia stage hii?
Wanasali nini hao watu wa hiyo familia?
Aiseee siku nikiingia msikiti wa aina hiyo nami lazima nizirushe...
Mmmh !! dadngu usiamini maneno hayo ya Patience123 acha uongo !! HAKUNA,HAKUNA, NO no kwanza hakuna Wamanyema waeupe, hilo ni uongo !! pili inapo adhiniwa tu wa kwanza hutakiwa akaSwali mbele apendavyo !! safu hutimia tammati ndipo Swala husimama !!!
 
Taja jina LA mckiti

Huyo ni muongo,pengine ukute hata sio muislamu,kaamua tu kuleta huu ushuzi wake hapa kuona watu wata react vipi,kwani anajua masuala ya kiimani huwa yanajadiliwa kwa jazba na yeye anapenda kuona watu wakikwaruzana kwa mitazamo ya kiimani,angekuwa anachokisema ni kitu anachokifahamu fika ingekuwa ni rahisi kwake kutaja jina la msikiti unaofanya mambo hayo,lakini hajataja na hatotaja kwa kuwa si kweli,kwani hayo mambo misikitini ni ya kufikirika sana.
 
Wandugu wote......nawaomba hii mada ya ubaguzi msikitini muiache.
Maeneo ya posta kuna misikiti mitatu.
Msikiti wa Shia....Bohora na Ngazija.
Uislam hauna ubaguzi kabisa...angalia ibada ya Hijja.Mimi ni mweusi na siyo bohora lakini naweza ingia msikiti wao nikaswali kulingana na dhehebu langu.HAKUNA UBAGUZI KATIKA KUABUDU......
 
Wewe kama ni Muislam ungeingia kuswali katika huo msikiti halafu uone kama utabaguliwa ama vipi kuliko kuja kupost vitu vya kudhania na kufikirika. Inawezekana maeneo yaliko huo msikiti hao wasio weusi ni wengi zaidi lakini msikiti wowote hanyimwi tu kwenda kuswali, ni uchaguzi wako tu
 

Usinanganie dini za watu, km wewe Ni mweusi fuata dini za asili yako, labda wao wanawangaa !!!!
 
SalaamAleykum W W..
Nakuamkia kwa Salaam za muumba Rehema zake ziwe juu yetu !!
kwa heshima na taadhima nachambua kauli uliyotujuza kuwa Huko Asia na huku barani Africa !!
Wanazuoni wengi husema "ihtilafu za MaUlamaa ni rehema" yaani kuna Madrasa (mafundisho) mbali mbali za ilmu ya dini.... japo wapo wanaokubalina na upamabaji (urembo,maukato kwa "ke" hizo) na wapo wanaopingana nao na wapo waiitayo makruhu (kero) !!Sasa yategemea mtumiaji huyo anafuata MADRASA ipi ...
Makazi mema na kila lenye kheri nawe...
 
Punguza Mawazo mleta mada,kama ni shia weusi wapo unachotakiwa uswali kama wanavyoswali wao. Dhuhuri na alasiri wanaunga pamoja na maghribi na isha wanaziunga pamoja jioni.

Sasa kama wewe ni suni utaratibu wako hauko hivyo kwanini uende ukaswali hapo?
 
Inawezekana alumina mwizi wa viatu katimuliwa ndio akaona awatangazie ubaguzi baking msikiti wenye ubaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…