Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,283
- 9,913
Ilianzia katika mvutano wa kisheria kati ya jumuia ya Kiislamu na Kanisa la Waadventista wa Sabato (SDA) kuhusu umiliki wa ardhi.
Mvutano huo uliokuwepo kwa miongo kadhaa, ulimalizika mwezi Oktoba mwaka huu na Mahakama ya Mazingira mjini Kisumu iliamua kuwa ardhi hiyo ni milki ya Jamii ya Kiislamu.
Katika jitihada za kujenga daraja la mahusiano kati ya jamii ya Kiislamu na kanisa, imechagua jina la msikiti ambalo limevuta hisia za wengi katika mitandao ya kijamii.
Msikiti ambao umejengwa kwenye ardhi iliyokuwa kwenye mgogo eneo la Kaloleni katika Kaunti ya Kisumu unaitwa 'Msikiti wa Yesu Kristo mwana wa Maria ( The Mosque of Jesus Christ the son of Mary)
Lakini kwa nini jina hili la kipekee?
Abdul Rashid ni Mwadhini ameliambia gazeti la The Standard la Kenya kuwa '' Tumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu ardhi na hii ni moja ya sababu zilizotufanya kuchagua jina hili. Sisi hatuna uadui na Wakristo,'' alisema.
Amesema kuwa Waislamu pia wanaamini Yesu na kuwa alikuwa sambamba na manabii wanne akiwemo Mtume Muhamad (S.A.W).
''Waislamu wanaamini katika Yesu Kristo . Uchaguzi wa jina pia ni shukrani ya Yesu Kristo ambaye tunaamini atarudi tena," Rashid aliliambia gazeti la The Standard.
Hatua hii imegusa hisia za watu nchini Kenya wengine wakihoji je, huu ni Msikiti na Kanisa kwa wakati mmoja? Wengine wameifurahia hatua hiyo
BBC.
Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app