Msigwa: Kabla ya kuzungumzia mfumo wa uchaguzi, Bashiru na Magufuli wakifufue kwanza kile chama cha siasa kilichokuwa kinaitwa CCM

Mimi siyo mwanasiasa lakini kauli ya Bashiru kwa nafasi yake ktk chama chake ni damage kubwa kwa NEC na serikali nzima. Nani atacontrol hii damage ni yeye mwenyewe au chama au itaachwa ipite kama upepo?
Huyu msigwa si mbobevu ktk analysis, hapa mtu angetegemea opposition coalition waje na press conference ya nguvu kulingana na kauli ya Bashiru as reference
 
CHADEMA wamechanganyikiwa. Badala ya kujadili Chama chenunaanza kuijadili CCM.
Kwahiyo msigwa siku hizi amekuwa msemaji wa CCM!?
"chenunaanza" ndo nini mkuu achakuchafua kiswahili jaziba haifai jibu hoja.
 
Mimi nafikiri akili zako ndo za kihayawani,kwa siku uaandika threads zisizopungua 5,zote ni useless,ni kama umefungwa motor matakoni,huna hoja ,wajinga wezako ndo watatembea na ujinga wako,sioni jipya
Mkuu matusi ya nn jenga hoja.
 
Nimemsikia Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM. Kauli yake inajaribu kujenga dhana potofu kuwa CCM imekuwa ikishinda kihalali lakini kwa kura kidogo, kwasababu eti wananchi hawana imani na mfumo wa uchaguzi.

Ukweli ni kwamba CCM ya Bashiru na Magufuli haijawahi kushinda kihalali katika uchaguzi wowote ule.Si wa kura kidogo wala kwa kura nyingi, CCM ya Bashiru na Magufuli haijawahi kushinda popote kihalali.

Wakati CCM ya kina Kikwete na Kinana, ilihangaika kutafuta ushindi kwa kutumia rushwa na wizi wa kura;CCM ya Magufuli na Bashiru hata kwa kutumia rushwa na wizi wa kura, bado haina uwezo wa kupata ushindi! Ni CCM iliyofikia kilele cha juu kabisa cha kuchokwa na kukataliwa na umma!

Kitu pekee ambacho CCM ya Magufuli na Bashiru inafanya ni kuitumia Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi kuzuia mawakala wa Chadema wasiingie vituoni kwa wakati, kujijazia kura kwenye masanduku, kujiandikia matokeo ya kughushi kwenye fomu za matokeo na kuhakikisha kuna mitutu ya bunduki ya kutosha ya kuwawezesha Wakurugenzi wa Halmashauri (Wateule wa Magufuli) kutangaza ushindi feki.

Kwa maneno mengine, ushindani uliopo hivi sasa, si baina ya vyama vya upinzani na CCM kama ilivyozoeleka huko nyuma; bali ni baina vyama vya upinzani na vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na wengineo waliokubali kuchukua nafasi ya CCM iliyoshindwa siasa.

Kwa hiyo, kimsingi, CCM anayoizungumzia Bashiru hata haipo.Ni kweli mfumo wetu wa uchaguzi una mapungufu na dosari nyingi. Lakini kabla ya kuzungumzia mfumo, namshauri Bashiru na Magufuli watafute namna ya kufufua kile "chama cha siasa" kilichokuwa kinaitwa "CCM", ili tushindane kwa sera na mikakati, na sio kwa mitutu ya bunduki.

Mfumo wa uchaguzi upo kwaajili ya vyama vya siasa, na si kwaajili ya Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola vilivyojipa kazi ya kuisaidia CCM iliyokufa.

Na hata maboresho yoyote yanayohitaji kufanyika katika mfumo wetu wa uchaguzi yanapaswa kulenga vyama halali vya kisiasa vinavyoshindana na sio majeshi ya nchi.

Rev. Peter Msigwa the MP for iringa Urban.

My take:
Niliwahi andika hapa JF hivi:

BM aliitoa "sisiem" mtaani akaipeleka hospitali (wodini). Jk, kwa upande wake, aliitoa wodini na kuipeleka ICU, na JPM anaitoa wodini na kuipeleka mortuary (kaburini).
Na mbowe anaipelekaje chadema, kundulo, nyani haoni.
 
In fact CCM ilianza kufa taratibu pale Nyerere alipokifanya ccm kuwa chama dola.

Ukweli umekuchoma mkuu
Hizi ni porojo kama porojo zingine tu,ilimradi siku zinakwenda,litaibuka lingine,hili litapita,namshauri katibu mkuu wa ccm kwamba siasa za majikwaani haziepukiki,awe makini na kauli zake,kuna kundi kubwa la wanasiasa linaishi kwa kuvizia matamko,yaani watafuta kiki,atachokonolewa sana,hii ni mwanzo tu,kila tafsiri ya kauli zake itapatikana kwa mtazamo wa kila mmoja achukuliavyo
 
Watanzania tumewechoka mkuu tuachieni nchi yetu, mwende na CCM yenu...

Back
Top Bottom