Msigwa: Kabla ya kuzungumzia mfumo wa uchaguzi, Bashiru na Magufuli wakifufue kwanza kile chama cha siasa kilichokuwa kinaitwa CCM

Nimemsikia Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM. Kauli yake inajaribu kujenga dhana potofu kuwa CCM imekuwa ikishinda kihalali lakini kwa kura kidogo, kwasababu eti wananchi hawana imani na mfumo wa uchaguzi.

Ukweli ni kwamba CCM ya Bashiru na Magufuli haijawahi kushinda kihalali katika uchaguzi wowote ule.Si wa kura kidogo wala kwa kura nyingi, CCM ya Bashiru na Magufuli haijawahi kushinda popote kihalali.

Wakati CCM ya kina Kikwete na Kinana, ilihangaika kutafuta ushindi kwa kutumia rushwa na wizi wa kura;CCM ya Magufuli na Bashiru hata kwa kutumia rushwa na wizi wa kura, bado haina uwezo wa kupata ushindi! Ni CCM iliyofikia kilele cha juu kabisa cha kuchokwa na kukataliwa na umma!

Kitu pekee ambacho CCM ya Magufuli na Bashiru inafanya ni kuitumia Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi kuzuia mawakala wa Chadema wasiingie vituoni kwa wakati, kujijazia kura kwenye masanduku, kujiandikia matokeo ya kughushi kwenye fomu za matokeo na kuhakikisha kuna mitutu ya bunduki ya kutosha ya kuwawezesha Wakurugenzi wa Halmashauri (Wateule wa Magufuli) kutangaza ushindi feki.

Kwa maneno mengine, ushindani uliopo hivi sasa, si baina ya vyama vya upinzani na CCM kama ilivyozoeleka huko nyuma; bali ni baina vyama vya upinzani na vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na wengineo waliokubali kuchukua nafasi ya CCM iliyoshindwa siasa.

Kwa hiyo, kimsingi, CCM anayoizungumzia Bashiru hata haipo.Ni kweli mfumo wetu wa uchaguzi una mapungufu na dosari nyingi. Lakini kabla ya kuzungumzia mfumo, namshauri Bashiru na Magufuli watafute namna ya kufufua kile "chama cha siasa" kilichokuwa kinaitwa "CCM", ili tushindane kwa sera na mikakati, na sio kwa mitutu ya bunduki.

Mfumo wa uchaguzi upo kwaajili ya vyama vya siasa, na si kwaajili ya Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola vilivyojipa kazi ya kuisaidia CCM iliyokufa.

Na hata maboresho yoyote yanayohitaji kufanyika katika mfumo wetu wa uchaguzi yanapaswa kulenga vyama halali vya kisiasa vinavyoshindana na sio majeshi ya nchi.

Rev. Peter Msigwa the MP for iringa Urban.

My take:
Niliwahi andika hapa JF hivi:

BM aliitoa "sisiem" mtaani akaipeleka hospitali (wodini). Jk, kwa upande wake, aliitoa wodini na kuipeleka ICU, na JPM anaitoa wodini na kuipeleka mortuary (kaburini).
Hakuna hoja wala.majibu yoyote kutoka CCM hata Magufuli mwenyewe kama mwenyekiti wa chama anayeweza kupinga ukweli huu. Hakuna mwenye majibu si polisi wala usalama.
Rev. peter Msigwa umegongelea msumali kwenye kovu.
 
Safi sana Bashiru!
Bashiru amezusha mjadala mpya ndani na nje ya ccm, nimesikia Bashiru akijadiliwa leo katika medani za siasa DW.

Hofu imeanza kutanda kama kweli Maneno ya Bashiru ni ya chama au ilikuwa msimamo wake mwwnyewe? Na je Atasalimika mbele ya malaika feki Jiwe??
 
Hizi ni porojo kama porojo zingine tu,ilimradi siku zinakwenda,litaibuka lingine,hili litapita,namshauri katibu mkuu wa ccm kwamba siasa za majikwaani haziepukiki,awe makini na kauli zake,kuna kundi kubwa la wanasiasa linaishi kwa kuvizia matamko,yaani watafuta kiki,atachokonolewa sana,hii ni mwanzo tu,kila tafsiri ya kauli zake itapatikana kwa mtazamo wa kila mmoja achukuliavyo
Wewe na Bashiru nani lofa??
 
Mimi nafikiri akili zako ndo za kihayawani,kwa siku uaandika threads zisizopungua 5,zote ni useless,ni kama umefungwa motor matakoni,huna hoja ,wajinga wezako ndo watatembea na ujinga wako,sioni jipya
Kaka hizi hasira zote zinatokana na Tamko la Bashiru kukinanga chama chake?? Mwanzo wa mtifuano ndani ya chama.
 
Nimemsikia Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM. Kauli yake inajaribu kujenga dhana potofu kuwa CCM imekuwa ikishinda kihalali lakini kwa kura kidogo, kwasababu eti wananchi hawana imani na mfumo wa uchaguzi.

Ukweli ni kwamba CCM ya Bashiru na Magufuli haijawahi kushinda kihalali katika uchaguzi wowote ule.Si wa kura kidogo wala kwa kura nyingi, CCM ya Bashiru na Magufuli haijawahi kushinda popote kihalali.

Wakati CCM ya kina Kikwete na Kinana, ilihangaika kutafuta ushindi kwa kutumia rushwa na wizi wa kura;CCM ya Magufuli na Bashiru hata kwa kutumia rushwa na wizi wa kura, bado haina uwezo wa kupata ushindi! Ni CCM iliyofikia kilele cha juu kabisa cha kuchokwa na kukataliwa na umma!

Kitu pekee ambacho CCM ya Magufuli na Bashiru inafanya ni kuitumia Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi kuzuia mawakala wa Chadema wasiingie vituoni kwa wakati, kujijazia kura kwenye masanduku, kujiandikia matokeo ya kughushi kwenye fomu za matokeo na kuhakikisha kuna mitutu ya bunduki ya kutosha ya kuwawezesha Wakurugenzi wa Halmashauri (Wateule wa Magufuli) kutangaza ushindi feki.

Kwa maneno mengine, ushindani uliopo hivi sasa, si baina ya vyama vya upinzani na CCM kama ilivyozoeleka huko nyuma; bali ni baina vyama vya upinzani na vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na wengineo waliokubali kuchukua nafasi ya CCM iliyoshindwa siasa.

Kwa hiyo, kimsingi, CCM anayoizungumzia Bashiru hata haipo.Ni kweli mfumo wetu wa uchaguzi una mapungufu na dosari nyingi. Lakini kabla ya kuzungumzia mfumo, namshauri Bashiru na Magufuli watafute namna ya kufufua kile "chama cha siasa" kilichokuwa kinaitwa "CCM", ili tushindane kwa sera na mikakati, na sio kwa mitutu ya bunduki.

Mfumo wa uchaguzi upo kwaajili ya vyama vya siasa, na si kwaajili ya Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola vilivyojipa kazi ya kuisaidia CCM iliyokufa.

Na hata maboresho yoyote yanayohitaji kufanyika katika mfumo wetu wa uchaguzi yanapaswa kulenga vyama halali vya kisiasa vinavyoshindana na sio majeshi ya nchi.

Rev. Peter Msigwa the MP for iringa Urban.

My take:
Niliwahi andika hapa JF hivi:

BM aliitoa "sisiem" mtaani akaipeleka hospitali (wodini). Jk, kwa upande wake, aliitoa wodini na kuipeleka ICU, na JPM anaitoa wodini na kuipeleka mortuary (kaburini).
Hata yesu alikufa na siku ya tatu akafufuka na amekaa kuume(kulia) kwa baba yake!
CCM DAIMA MILELE!
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Ukweli mtupu ambao police, usalama wa taifa, na tume ya uchaguzi wanaukubali kabisa bila kupepesa
Kwa sasa hamna chama kinachoitwa ccm bali kuna police na tume ya uchaguzi
 
Ndiyo maana Bashiru anajua na voters turn out ya 30 % wakati NEC wanakupa over 70 %.
Hata hivuo nashangaa nini kinawauma watu kama akina Bashiru na Nape ikiwa lengo la cxm ni kuwa madarakani na kweli kiko madarakani??
 
Sijaona mahali amegusia sera mpya waliyozindua juzi kwa mbwembwe..au wameitupa kapuni tayari baada ya kuona nayo haijawapa kiki??
 
Back
Top Bottom