Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 59,020
- 103,416
Hizi ni porojo kama porojo zingine tu,ilimradi siku zinakwenda,litaibuka lingine,hili litapita,namshauri katibu mkuu wa ccm kwamba siasa za majikwaani haziepukiki,awe makini na kauli zake,kuna kundi kubwa la wanasiasa linaishi kwa kuvizia matamko,yaani watafuta kiki,atachokonolewa sana,hii ni mwanzo tu,kila tafsiri ya kauli zake itapatikana kwa mtazamo wa kila mmoja achukuliavyo
Mkuu sio kuwa makini na kauli zake, sema asiseme ukweli. Huyo Bashiru ukimwangalia ni muisilamu safi, na hajawahi kujihusisha na siasa za ulaghai. Magufuli alimpa cheo kikubwa akidhani kila mtu huwa anashiriki uovu. Kwa bahati mbaya huyo Bashiru sio mwanasiasa wa kufumbia macho ouvu kutokana na ucha Mungu wake, hivyo hicho kinachoendelea kwenye box la kura ambalo yeye anaamini linatoa kiongozi halali anaona dhahiri linachezewa na chama ambacho yeye ni kiongozi. Hili linaitesa dhamiri yake.
Kila mara huwa nasema hapa ccm imechokwa na hiyo ni kawaida ya binadamu yoyote. Magufuli kuamua kutumia madaraka yake vibaya kuihujumu cdm ni kwakuwa anajua kabisa cdm ndio inayopendwa kutokana na wakati, hivyo anawatumia tiss, vyombo vya dola na tume ya uchaguzi kuipa uhai ccm kitu ambacho hawezi na hatokaa aweze. Ukitaka kujua binam huchoka angalia ccm inafanya mikutano yenyewe, inatangaza maendeleo, inawahujumu cdm na kuwadhalilisha lakini bado haipati mvuto. Na sasa watu kudhihirisha wameichoka ccm wanatumia njia ya amani ya kususia uchaguzi. Na hawa akina Bashiru ni watu wanaosoma nyakati na ndio maana anajikuta automatic anaongea ukweli. Hiyo ni nature, kwamba wakati ni ukuta.