Msigwa amvaa Paul Chacha kuhusu sakata la Nchimbi

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
400
Reaction score
1,024
Peter Msigwa amemjibu Paul Chacha kufuatia kauli yake kwamba wakati akiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jukumu lake lilikuwa kushika simu za Dkt. Emmanuel Nchimbi, akikanusha madai hayo na kusema hajawahi kufanya kazi hiyo.

Msigwa amesema hakuna kazi halali inayomvunjia mtu heshima, hata kama angekuwa akifanya kazi hiyo, lakini amesisitiza kuwa kinachopaswa kukemewa ni kutumia madai yasiyo ya kweli kwa lengo la kumdhalilisha mtu mwingine.

Katika majibu yake, Msigwa ameeleza kushangazwa na hatua ya Chacha kuendelea kumhusisha Nchimbi katika kauli zinazomlenga yeye, akijiuliza kwa nini jina la Kiongozi huyo linaendelea kuingizwa kwenye mjadala wakati CCM ilishamfukuza, ameondoka katika Uongozi wa Serikali na kutangaza kustaafu siasa.

Amesema kama Chacha ana jambo la kumkosoa, anapaswa kulielekeza kwake badala ya kumhusisha mtu mwingine ambaye hayupo kwenye mjadala wao. Hata hivyo, amesisitiza kuwa hana nia ya kumsemea Nchimbi wala kujificha nyuma yake, kwa kuwa anawajibika mwenyewe kwa historia na maamuzi yake ya kisiasa.

Msigwa amekumbusha kuwa alipoona hawezi kuendelea kusimama na mambo ambayo dhamiri yake haikuyakubali, aliamua kuondoka CCM na baadaye kuomba msamaha hadharani. Hata hivyo, amesema hatua hiyo haimaanishi amepoteza haki ya kujitetea dhidi ya kile alichokiita madai yasiyo ya kweli.

Aidha, ameelekeza mjadala kwenye masuala mapana ya kisiasa, akitaja umuhimu wa kujadili Katiba Mpya, uhuru wa Mahakama, haki za wananchi na mipaka kati ya chama tawala, Serikali na vyombo vya dola.

Katika hatua nyingine, Msigwa amemtaka Chacha kufafanua kauli yake kwamba vyombo vya ulinzi na usalama ni mali ya CCM, akisema suala hilo lina uzito mkubwa katika mjadala kuhusu nafasi na wajibu wa taasisi hizo.

Amehitimisha kwa kusema yuko tayari kujadili historia yake ya kisiasa, lakini hatakubali historia hiyo kuwasilishwa kwa madai anayoyapinga, huku akisisitiza kuwa kumwondoa mtu kwenye nafasi ni jambo moja, lakini kuendelea kupambana na kivuli chake ni jambo jingine.
 
mchungaji Msigwa anajaribu kukana na kukataa jukumu alilokua nalo wakati akiwa CCM sio? :pedroP:
 
Ila msigwa alijivua nguo hadharani,
Namshauri akae kimya maana lolote analoongea sasahivi ni sawa na kutingisha chululu na kende baada ya kujivua nguo
 
Back
Top Bottom