Msigwa ajadili bajeti ITV, Asema UKAWA wanaunga mkono mafao ya wabunge kukatwa kodi

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Anasema mabalozi wa nchi yetu wameenda nje kuangalia interest za CCM badala ya maslahi ya kiuchumi za taifa.

Anasema viwanda havitatukuta tunazozana huku bila kutuma vijana wakasome nchi nyingine.

Anasema wabunge wa CCM hawawezi kufikiria nje ya muda wa utawala wao, wanadhani watatawala milele.

Anasema leo tuna serikali ambayo huwezi kuikosoa ndani ya bunge au hata nje ya bunge maana serikali imezuia mikutano.

Amesema wananchi wampuuze Lusinde maana wameona jinsi wabunge wasivyoweza kujadili bajeti badala ya watu.

Amsema watasubiri hata akikaa miaka mitano.

Anasema wao hawakufuata posho bungeni maana waliacha milioni 30 kila mmoja kwenye bunge la katiba. Anaunga mkono kiinua mgongo kukatwa lakini akikumbusha kukata cha viongozi wote wa kisiasa wakiwemo marais.
 
Anasema mabalozi wa nchi yetu wameenda nje kuangalia interest za Ccm badala ya maslahi ya kiuchumi za taifa
Anasema viwanda havitatukuta tunazozana huku bila kutuma vijana wakasome nchi nyingine
Anasema wabunge wa Ccm hawawezi kufikiria nje ya muda wa utawala wao, wanadhani watatawala milele
Anasema leo tuna serikali ambayo huwezi kuikosoa ndani ya bunge au hata nje ya bunge maana serikali imezuia mikutano.

Amesema wananchi wampuuze Lusinde maana wameona jinsi wabunge wasivyoweza kujadili bajeti badala ya watu.
Anasema labda Naibu spika anavaa pampas maana huwa hatoki kukojoa. Amsema watasubiri hata akikaa miaka mitano

ANATAPATAPA TUUUUUUUUUUU HAPA HAMNA ANCHOONGEA CHA MAANA, ANAONGEA HILI ANA RUKIA LILE,
BE SERIOUS WAJAMAN,
 
Akichambua bajeti ITV Mbunge makini Mch.Msingwa anasisitiza kuwa wao UKAWA wanaunga mkono kukatwa kodi kwa kiinua mgongo cha wabunge.

Anaulizwa kipi kizuri katika bajeti hii anasema Kukata kodi kiinua mgongo cha wabunge.Pamoja na hilo amesema bunge liende mbali zaidi hadi kwenye pensheni za maspika,waziri mkuu,rais nk!

Pia amesema watu wakumbuke UKAWA walishaacha posho za mamilioni Bunge la Katiba,yote haya ni ilikuwa kuwapigania wananchi kupata katiba bor.

Mtangazaji Godwin Gondwe ameonekana wazi wazi kufurahishwa na msimamo wa Mch.Msingwa
 
Ila kiujumla naibu spika ni mzigo. Nimesikia kaagizwa ahakikishe anaongoza vikao vyote mpaka bajeti ipitishwe ili kuepuka hoja nzito toka ukawa dhidi ya bajeti.
 
Halafu anajiita Mchungaji! Mchungaji gani hana lugha ya staha? Mchungaji wa kweli lugha akiongea unajua huyu mchungaji.Pia asivyojua mambo hajui kuwa bajeti yeye kama mbunge anatakiwa aijadili bungeni siyo vichochoroni.Wapiga kura wake wamemtuma bungeni akawakilishe mambo yao bungeni yeye anaenda kuyajadili vijiweni.Poleni wapiga kura wa Iringa mjini

Huyu anayejiita mchungaji Mimi simshangai ana mambo yake mcheki hapa akiwa marekani

_DSC8604.JPG
 
Kila mtu alipe kodi.Nashangaa kuna mtu anahamasisha watu wengine walipe kodi hadi kwa matangazo ya TV lakini halipi.Anahamasisha hadi povu linamtoka kumbe yeye hana tofauti na wakwepa kodi

Cha ajabu atasingizia sheria inamzuia ndo yenye matatizo

Hakuna nchi serious yenye maadili inayoweza kuruhusu mtu asilipe kodi
 
Halafu anajiita Mchungaji! Mchungaji gani hana lugha ya staha? Mchungaji wa kweli lugha akiongea unajua huyu mchungaji.Pia asivyojua mambo hajui kuwa bajeti yeye kama mbunge anatakiwa aijadili bungeni siyo vichochoroni.Wapiga kura wake wamemtuma bungeni akawakilishe mambo yao bungeni yeye anaenda kuyajadili vijiweni.Poleni wapiga kura wa Iringa mjini

Huyu anayejiita mchungaji Mimi simshangai ana mambo yake mcheki hapa akiwa marekani

_DSC8604.JPG
hivi mkuu huyu na mchungaji kwajima nani zaidi? ni swali tu la kichokozi...
 
Wabunge wengine ni mizigo sana. Kauli gani hiyo iliyokosa busara za utu uzima? Yani ITV wamepoteza mda kuleta mtu anayeongea upuuzi mtupu.

Mkuu mbunge kama msigwa ni mzigo tena sio mdogo.Hayo ndio walikuwa wakililia TV kuonyeshwa LIVE..
 
ANATAPATAPA TUUUUUUUUUUU HAPA HAMNA ANCHOONGEA CHA MAANA, ANAONGEA HILI ANA RUKIA LILE,
BE SERIOUS WAJAMAN,

Ili asionekane anatapatapa unapendekeza aongee nini? Mimi nafikiri ni katika kuchagua mambo muhimu katika mengi aliyo nayo na ambayo angeyasema kama muda ungeruhusu. Kwa muda mfupi uliopo ni lazima awe makini katika mambo anayoyasema ili kufikisha ujumbe.
 
hili la pampas msigwa kateleza. ila kiujumla naibu spika ni mzigo. nimesikia kaagizwa ahakikishe anaongoza vikao vyote mpaka bajeti ipitishwe ili kuepuka hoja nzito toka ukawa dhidi ya bajeti.

Kaka hiyo ni siasa. Mbona lowasa walisema kanyea mkuu na akaendelea na siasa zake tu?? Tena ni kina msukuma ndo alimwita ivo. So thats a politics and infacts is a bad game. If don know to play it just be aside
 
hivi mkuu huyu na mchungaji kwajima nani zaidi? ni swali tu la kichokozi...

Wote wawili kwa kuporomosha matusi hawajambo mwingine anamporomoshea matusi pengo mwingine anaporomoshea matusi Naibu Spika.Kanisa limeingiliwa na wachungaji koko
 
Ha ha ha! Eti sheria inamzuia kulipa kodi. Sheria inayozuia mtu/watu kufanya jambo jema hiyo ni null and void. Inatakiwa kufutiliwa mbali mara moja unless tuambiwe baadhi ya watu kulipa kodi ni jambo baya.
 
Anasema mabalozi wa nchi yetu wameenda nje kuangalia interest za Ccm badala ya maslahi ya kiuchumi za taifa
Anasema viwanda havitatukuta tunazozana huku bila kutuma vijana wakasome nchi nyingine
Anasema wabunge wa Ccm hawawezi kufikiria nje ya muda wa utawala wao, wanadhani watatawala milele
Anasema leo tuna serikali ambayo huwezi kuikosoa ndani ya bunge au hata nje ya bunge maana serikali imezuia mikutano.

Amesema wananchi wampuuze Lusinde maana wameona jinsi wabunge wasivyoweza kujadili bajeti badala ya watu.
Anasema labda Naibu spika anavaa pampas maana huwa hatoki kukojoa. Amsema watasubiri hata akikaa miaka mitano
Anasema wao hawakufuata posho bungeni maana waliacha milioni 30 kila mmoja kwenye bunge la katiba. Anaunga mkono kiinua mgongo kukatwa lakini akikumbusha kukata cha viongozi wote wa kisiasa wakiwemo marais
kama serikali haifichi kitu nn
mbona bunge lililo pita alikuwa anaendesha zungu leo hii wanaona hawez hau hawawataki ndio mana wamemkazania tulia busara inaitajika mtu anajadiliwa na kamat lakin bado anakalia kiti ikitokea kashindwa watasema je
 
Kama wastaafu hawalipi kodi basi Kuna kodi kubwa sana kwenye pensheni za wastaafu: Mawaziri Wakuu wastaafu....! Rais wastaafu na VP wastaafu!!!
 
Wanaosema Msigwa amesema matusi hawajawasikia wabunge wa Ccm wasivyojadili bajeti bali matusi kwa wapinzani. Amepata nafasi ya kuwajibu akatupa kombora na likatua bara bara
 
Back
Top Bottom