Msichana Witness Obedi aliyefariki na kuzikwa atokea nyumbani kwake na kusimulia mkasa

Usipotoshe watu, mambo ya kishirikina haluna ni uhuni tuu, hata wewe ukijificha tu mwezi familia yako inaelekea itakimbilia kwa waganga

Watakimbia wasichokijau, siri ni moja tu, upate ila ya kuwaona mchezo umeisha, ni mazingaombwe ya kutuficha macho tusiwaone ndicho mchezo mzima. Inapotokea watu kuambiwa kadondoka or what ever ukweli ni kwamba madawa yao yana masharti na muda, kimoja kikikosewa basi matokeo ndio hayo.
 
View attachment 160991Witness Obedi aliyefariki View attachment 160992Kaburi lake View attachment 160993Akiwa na wazazi kisha tukio View attachment 160994Majirani walioomboleza msiba wake wafika kushangaa tuko hilo

Tukio la pekee ambalo linaonekana ni la kishirikina huko Arumeru/Arusha ni pale msichana Witness Obed ambaye inaelezwa alifariki na kuzikwa mara mbili ametokea nyumbani akiwa hai kwa wazazi wake na kisha kusimulia mkasa wa tukio ulivyomtokea. Mkasa huo ulitokea baada ya binti huyo kurudi toka chuo na kufika nyumbani saa mbili jioni akiwa amechelewa ndiyo iliyokuwa sababu ya kugombezwa na familia yake hasa babake mzazi.

Mzazi wake anasema alimgombeza, hivyo binti akatoroka. Binti huyo hakurudi na siku iliyofuata wakatoa tangazo la kumtafuta kupitia vyombo mbalimbali vya habari na sheria. Baadaye walisikia katika kijiji kingine walimwokota msichana aliyefariki. Walipoenda kuuliza waliambiwa alishazikwa.

Wakaenda kuomba kibali polisi cha kufukua kaburi ili kubaini kama ni binti yao, baada ya kupata kibali na kufukua kaburi waliitambua maiti kutokana na alama ambazo aliwa nazo wakati akiwa hai. Wakauchukua mwili huo na kwenda kufanya matanga kwao na kuuzika upya kwenye kaburi jingine.

Baada ya kuondoka alifika kwenye nyumba moja na kumkuta mama mmoja, aliomba maji ya kunywa. Alipewa na alipokuwa anakunywa mama yule alikuwa anamsimamia, lakini alipoonja na kuona machungu alikataa, lakini mama yule alimlazimisha kwa kumnywesha hadi akamaliza kisha akapoteza fahamu na hakujua nini kinaendelea na wapi aliko hakujitambua.

Anasema baadaye hajitambui amefikaje nyumbani, na mama yake alipomwona mara ya kwanza akifika alikimbia kufikiria anaona mzuka. Lakini baadaye alijipiga moyo konde na kumjongea binti yake.

Kuna matukio kadhaa yametokea siku za karibu huko kanda ya Ziwa na kwingineko kwa matuko kama haya, kuna kila dalili ya mchezo wa kishirikia.

Polisi wamesema wanataarifa juu ya tukio hilo na wanalifanyia uchunguzi wa kina.

Source: Global Publishers.

Uchawi wa Geita sasa umeingia Arumeru!
 
Habari hizi ni za kweli ingawa mwandishi ameongeza chumvi ila tukio limetokea maeneo ya moshono arusha, na baba wa marehemu ni mwinjilisti wa makanisa ya KKKT usharika wa Mara. wakati binti huyu amepotea kulikuwa na mvua kubwa sana zikinyesha mkoani Arusha na binti huyu alikuwa ni mlokole na alipenda sana kwenda kwenye maombi radio safina kwa wale wakazi wa arusha na moshi wanafahamu, kutokana na tatizo lake la kurukwa na akili muda mwingine alitoka safina na kwenda kwa ndugu zake maeneo ya nduruma na wakati akirudi akaendele na safari zake hakufika nyumbani hali ilioinua taharuki kubwa nyumbani kwao. baada ya kutomuona kwa muda wa siku nne wakaamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola na ndipo walipopata taarifa kuwa kuna maiti maeneo ya nduruma ya msichana imekutwa mtoni na ikiwa imeharibika na wakazi wa huko hawaitambui na hakuna mtu kapotea maeneo hayo, baada ya kusikia hayo familia ya binti huyo iliamua kufunga safari mpaka huko na kukuta wakazi wa nduruma wameshaizika kwenye mfuko wa sulphate(kwa wakazi wa arusha na moshi) na kuoma ifukuliwe na polisi waliwaonyesha picha wakiwa wameitoa maiti hiyo ndani ya maji baba mzazi wa binti huyokutokana na binti yake kutoonekana kwa muda mrefu na taarifa kwamba binti yae alienda nduruma moja kwa moja alisema huyu ni binti yangu ingawaje mama alikataa na kusema binti yangu sio mnene hivi baba akasema kwa sababu imekaaa kwenye maji mda mrefu imevimba. kilichofuatia ni kuifukua maiti na kuiweka kwenye jeneza ikiwa kwenye mfuko wa huo wa sulphate na kwenda kijiji cha moshono kwa mazishi. Habari hizi si za kishirikina ila ni makosa tu yalifanyika na mpaka so watu waache kupotosha.mto nduruma ni mto mkubwa sio mferegi so maiti hiyo huenda imetoka mbali sana coz mpaka sasa hivi hakuna mtu mkoani arusha ameripoti kupotelewa na ndugu na polisi wanaendelea na uchunguzi kwa kuwasiliana na mikoa mingine.kaburi limeng'olewa tu msalaba na kuachwa kama lilivyo mpaka hapo uchunguzi wa polisi utakapo kamilika ila ndugu wa baba wa binti wanasema walisawazishe coz ni mkosi.source ni mimi mwenyewe coz nlikuwa mpaka eneo la tukio.
Ahsante sana Kiongozi,kwa kunitoa tongo tongo.
 
Mambo haya yasikieni kwa wengine, nimeamua kutoa maoni kuhusiana na huyu binti kwa saba namjua na hata wazazi wake nawajua vyema hususani baba yake Mwinjilisti Obedi. Tarehe 5 mwezi wa 6 mwaka 2023 nilikutana naye maeneo ya fulani katikati ya jiji la Arusha, akiwa amekaa na mama mmoja anachoma mahindi na nilipomwona ndipo kumbukumbu za tukio lake zikanijia na kujiuliza anafanya nini maeneo yale mida ya usiku? Hapo nikamfuata nikamwuliza unanijua akasema hanijui nami nikamwambia nakujua vizuri tu. Akaomba nimnunulie muhindi nikafanya hivyo na kumwambia aagize na uji kabisa.
 
Baada ya hapo nikamwuliza unakaa wapi? Akajibu nilipomkuta ndipo anapoishi siku zote. Nikamwomba anipe historia kamili ya maisha yake na hapo ndipo akanieleza yaliyomsibu toka apatwe na maswahibu yaliyokuwa na utata. Kwa maelezo yake ni kwamba shida ilianzia pale alipopata kipaimara, alipatwa na hali ya kupata ugonjwa wa kukakamaa mwili mara kwa mara na haikujulikana ugonjwa huo ulitokana na nini kwani hata madaktari walipomfanyia vipi hakukuonekana ugonjwa au viashiria vyovyote vya kuwa na magonjwa aina ya dege dege. Kwa maelezo yake alianza kwenda maombi ya kiimani sehemu mbali mbali mojawapo ni Safina.
 
Anaeleza kuwa kuna siku alikwenda kumtembelea shangazi yake na hapo ndipo taarifa za yeye kufariki na kuzikwa zilianza kuenezwa na kwa maelezo anadai hakuwa amefariki bali alikuwa amewekwa kama msukule na shangazi yake (dada wa baba yake Mwinjil Obedi), na maiti iliyozikwa na kufukuliwa haikuwa yake bali ni ya mtu mwingine. Anadai kuwa mama yake hakuamini kuwa mwanae amefariki ila baba mzazi alikubali kuwa mwili uliofukuliwa ni wa mwanae na akauchukua kwenda kuzika upya.
 
Namna alivyorudi uraini anasema ilikuwa ni siku ambayo familia, ndg na marafiki walipokwenda kutoa shukrani kanisani baada ya kumaliza shughuli ya kumzika kupita salama. Shangazi yake (aliyemchukua msukule) na yeye aliungana na ndg wengine kwenda kutoa shukrani. Na kwa maelezo yake ni kuwa siku hiyo huyo shangazi alijisahau akaucha mlango wazi na hapo yeye akapata upenyo wa kutoka na kuanza kuzurura, ikumbukwe Baba yake ni mtu maarufu Kata ya Moshono na wanajua huyu binti alikwisha fariki. Kuonekana hadharani kukazua taharuki kuwa marehemu amefufuka na taarifa zikasambaa hadi kule kanisani wanafamilia walipokwenda kutoa shukrani. Ndipo wanafamilia na jamii mbio mbio wakaja kuhakiki na kweli wakakuta ni yeye. Wakamwuliza ulikuwa wapi na kuwajibu kuwa alikuwa amefungiwa na shangazi yake..
 
Habari hizi ni za kweli ingawa mwandishi ameongeza chumvi ila tukio limetokea maeneo ya moshono arusha, na baba wa marehemu ni mwinjilisti wa makanisa ya KKKT usharika wa Mara. wakati binti huyu amepotea kulikuwa na mvua kubwa sana zikinyesha mkoani Arusha na binti huyu alikuwa ni mlokole na alipenda sana kwenda kwenye maombi radio safina kwa wale wakazi wa arusha na moshi wanafahamu, kutokana na tatizo lake la kurukwa na akili muda mwingine alitoka safina na kwenda kwa ndugu zake maeneo ya nduruma na wakati akirudi akaendele na safari zake hakufika nyumbani hali ilioinua taharuki kubwa nyumbani kwao. baada ya kutomuona kwa muda wa siku nne wakaamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola na ndipo walipopata taarifa kuwa kuna maiti maeneo ya nduruma ya msichana imekutwa mtoni na ikiwa imeharibika na wakazi wa huko hawaitambui na hakuna mtu kapotea maeneo hayo, baada ya kusikia hayo familia ya binti huyo iliamua kufunga safari mpaka huko na kukuta wakazi wa nduruma wameshaizika kwenye mfuko wa sulphate(kwa wakazi wa arusha na moshi) na kuoma ifukuliwe na polisi waliwaonyesha picha wakiwa wameitoa maiti hiyo ndani ya maji baba mzazi wa binti huyokutokana na binti yake kutoonekana kwa muda mrefu na taarifa kwamba binti yae alienda nduruma moja kwa moja alisema huyu ni binti yangu ingawaje mama alikataa na kusema binti yangu sio mnene hivi baba akasema kwa sababu imekaaa kwenye maji mda mrefu imevimba. kilichofuatia ni kuifukua maiti na kuiweka kwenye jeneza ikiwa kwenye mfuko wa huo wa sulphate na kwenda kijiji cha moshono kwa mazishi. Habari hizi si za kishirikina ila ni makosa tu yalifanyika na mpaka so watu waache kupotosha.mto nduruma ni mto mkubwa sio mferegi so maiti hiyo huenda imetoka mbali sana coz mpaka sasa hivi hakuna mtu mkoani arusha ameripoti kupotelewa na ndugu na polisi wanaendelea na uchunguzi kwa kuwasiliana na mikoa mingine.kaburi limeng'olewa tu msalaba na kuachwa kama lilivyo mpaka hapo uchunguzi wa polisi utakapo kamilika ila ndugu wa baba wa binti wanasema walisawazishe coz ni mkosi.source ni mimi mwenyewe coz nlikuwa mpaka eneo la tukio.
hii ndo comment yenye utimamu katika taarifa.
Sijui kwanin watu wengi hasa waafrica huwai kuamini kuelekea ushirikina.
Ni kama hatuko tayar kufikiri nje ya box.
Ndo maana suluhisho nyingi tunalazimika kuzikopa kwa wanaofikiri vizur.
Nikiangalia vipindi vya waganga namna vinasettiwa, hDi vyombo na taasisi zinaingizwa humo, hadi profesa anapigwa nachoka.
Mf ni kisa cha moto kuwaka wenyewe musoma wakati najua mchezo unakuwa kwa chemical reactions tu, naishia kusema duh, makolo ni wengi.
 
Baada ya hapo aliendelea na maisha kama kawaida, japo tatizo lake la kukakamaa halikuondoka. Anaeleza kuwa kilipita kipindi kifupi tokea mkasa ule umpate na hapo tatizo jingine likazaliwa.. Alianza kusumbuliwa na jicho moja likawa linamsumbua sana na walipompeleka hospitali ugonjwa haukuonekana na kadiri siku zilivyozidi kusogea ndipo ghafla alipo paralyse upande mmoja wa kushoto kuanzia lile jicho hadi mguu wa kushoto.
 
Kwa maelezo yake walimpeleka sehemu mbali mbali lakini hakuna waliojua chanzo cha tatizo, alilala zaidi ya miaka 3 hospitalini Muhimbili kama sijakosea, hadi siku moja anaeleza kuwa walipita watumishi wale wanaotoa huduma kwa kuombea wagonjwa mahospitalini na walipokuwa wanaomba kwenye kitanda alichokuwa amelala, anadai kuna kitu kilijivua na pale pale aliinuka na kuanza kutembea mwenyewe na kuongea na lile jicho likawa zima kabisa. Anadai huo ulikuwa ni muujiza kwake.
 
Habari hizi ni za kweli ingawa mwandishi ameongeza chumvi ila tukio limetokea maeneo ya moshono arusha, na baba wa marehemu ni mwinjilisti wa makanisa ya KKKT usharika wa Mara. wakati binti huyu amepotea kulikuwa na mvua kubwa sana zikinyesha mkoani Arusha na binti huyu alikuwa ni mlokole na alipenda sana kwenda kwenye maombi radio safina kwa wale wakazi wa arusha na moshi wanafahamu, kutokana na tatizo lake la kurukwa na akili muda mwingine alitoka safina na kwenda kwa ndugu zake maeneo ya nduruma na wakati akirudi akaendele na safari zake hakufika nyumbani hali ilioinua taharuki kubwa nyumbani kwao. baada ya kutomuona kwa muda wa siku nne wakaamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola na ndipo walipopata taarifa kuwa kuna maiti maeneo ya nduruma ya msichana imekutwa mtoni na ikiwa imeharibika na wakazi wa huko hawaitambui na hakuna mtu kapotea maeneo hayo, baada ya kusikia hayo familia ya binti huyo iliamua kufunga safari mpaka huko na kukuta wakazi wa nduruma wameshaizika kwenye mfuko wa sulphate(kwa wakazi wa arusha na moshi) na kuoma ifukuliwe na polisi waliwaonyesha picha wakiwa wameitoa maiti hiyo ndani ya maji baba mzazi wa binti huyokutokana na binti yake kutoonekana kwa muda mrefu na taarifa kwamba binti yae alienda nduruma moja kwa moja alisema huyu ni binti yangu ingawaje mama alikataa na kusema binti yangu sio mnene hivi baba akasema kwa sababu imekaaa kwenye maji mda mrefu imevimba. kilichofuatia ni kuifukua maiti na kuiweka kwenye jeneza ikiwa kwenye mfuko wa huo wa sulphate na kwenda kijiji cha moshono kwa mazishi. Habari hizi si za kishirikina ila ni makosa tu yalifanyika na mpaka so watu waache kupotosha.mto nduruma ni mto mkubwa sio mferegi so maiti hiyo huenda imetoka mbali sana coz mpaka sasa hivi hakuna mtu mkoani arusha ameripoti kupotelewa na ndugu na polisi wanaendelea na uchunguzi kwa kuwasiliana na mikoa mingine.kaburi limeng'olewa tu msalaba na kuachwa kama lilivyo mpaka hapo uchunguzi wa polisi utakapo kamilika ila ndugu wa baba wa binti wanasema walisawazishe coz ni mkosi.source ni mimi mwenyewe coz nlikuwa mpaka eneo la tukio.
Wewe ndio umeelezea vizuri. Unaona jinsi haya makanjanja dizaini ya Global yanavyoposha watu kwa makusudi. Watu wenye upeo mdogo hapa walishasema ni ushirikina.
 
Aliugua kimiujiza na akapona kimiujiza, na kwa sasa anaendelea na maisha yake japo hana marafiki anadai wamemtenga kwa sababu ya changamoto alizowahi kupitishwa na walimwengu. Hapaswi kulala usingizi kwa mgongo na akijisahau lazima apatwe na changamoto ya kukakamaa. Amefanikiwa kupata mtoto mmoja na anaishi kwa bibi na babu yake.
 
Je yy mzee obedi na dada yake walimalizana vp?
Asante
 
Wamasai wanakawaida zao za kuitishana vikao vya kupatanisha, tofauti na hapo hakuna kingine zaidi ya visasi na ukifa usije kwenye msiba basi.. Ila bado Witness Obedi anaishi maisha yenye kutia huruma na ni amejikatia tamaa ya maisha.. Bila huyo shangazi yake kufa hatokaa awe wa kawaida kamwe.
 
Back
Top Bottom