Meljons
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 3,085
- 1,360
Habari hizi ni za kweli ingawa mwandishi ameongeza chumvi ila tukio limetokea maeneo ya moshono arusha, na baba wa marehemu ni mwinjilisti wa makanisa ya KKKT usharika wa Mara. wakati binti huyu amepotea kulikuwa na mvua kubwa sana zikinyesha mkoani Arusha na binti huyu alikuwa ni mlokole na alipenda sana kwenda kwenye maombi radio safina kwa wale wakazi wa arusha na moshi wanafahamu, kutokana na tatizo lake la kurukwa na akili muda mwingine alitoka safina na kwenda kwa ndugu zake maeneo ya nduruma na wakati akirudi akaendele na safari zake hakufika nyumbani hali ilioinua taharuki kubwa nyumbani kwao. baada ya kutomuona kwa muda wa siku nne wakaamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola na ndipo walipopata taarifa kuwa kuna maiti maeneo ya nduruma ya msichana imekutwa mtoni na ikiwa imeharibika na wakazi wa huko hawaitambui na hakuna mtu kapotea maeneo hayo, baada ya kusikia hayo familia ya binti huyo iliamua kufunga safari mpaka huko na kukuta wakazi wa nduruma wameshaizika kwenye mfuko wa sulphate(kwa wakazi wa arusha na moshi) na kuoma ifukuliwe na polisi waliwaonyesha picha wakiwa wameitoa maiti hiyo ndani ya maji baba mzazi wa binti huyokutokana na binti yake kutoonekana kwa muda mrefu na taarifa kwamba binti yae alienda nduruma moja kwa moja alisema huyu ni binti yangu ingawaje mama alikataa na kusema binti yangu sio mnene hivi baba akasema kwa sababu imekaaa kwenye maji mda mrefu imevimba. kilichofuatia ni kuifukua maiti na kuiweka kwenye jeneza ikiwa kwenye mfuko wa huo wa sulphate na kwenda kijiji cha moshono kwa mazishi. Habari hizi si za kishirikina ila ni makosa tu yalifanyika na mpaka so watu waache kupotosha.mto nduruma ni mto mkubwa sio mferegi so maiti hiyo huenda imetoka mbali sana coz mpaka sasa hivi hakuna mtu mkoani arusha ameripoti kupotelewa na ndugu na polisi wanaendelea na uchunguzi kwa kuwasiliana na mikoa mingine.kaburi limeng'olewa tu msalaba na kuachwa kama lilivyo mpaka hapo uchunguzi wa polisi utakapo kamilika ila ndugu wa baba wa binti wanasema walisawazishe coz ni mkosi.source ni mimi mwenyewe coz nlikuwa mpaka eneo la tukio.
duu hii inatisha pia. hiyo maiti nayo kupatikana tu kipindi cha kutoweka huyo binti...