Msichana Witness Obedi aliyefariki na kuzikwa atokea nyumbani kwake na kusimulia mkasa

Si vema kukubaliana na hoja yako ya utetezi ambayo haionyeshi ufundi katika kutuhabarisha kwa kuchukua jukumu la kufanya utafiti wa kina kutoka kwa msichana husika, wazazi, majrani, makaburi na vyombo vya usalama kama polisi.

Ungefanya hivyo ningekuwa upande wako, lakini umekuja na habari za vijiweni zisizohakikiwa, kwa mtazamo wa jumla unaweza ukawa ni mmoja katika kundi wa hawa washirikina na hivyo unajaribu kujenga utetezi wa kuwalinda washirikina kashfa hii kwa vile wachawi kwa wachawi hawawezi kushikana uchawi.

wewe ndo mshirikina maana unapenda hbr za.kichawi kuliko hbr za ukweli
 
Huyo binti abanwe atasema alikuwa wapi....Huyo binti siku anagombezwa kuchelewa kurudi, alikuwa ametoka kwa mwanaume wake....

Akibanwa vizuri na mtu asiye amini mambo ya Uchawi hakika atasema alikokuwa........

Ila kwakuwa jamii yetu imegubikwa na Imani za kichawi hawatambana mpaka aseme alipokuwa...
 
wewe ndo mshirikina maana unapenda hbr za.kichawi kuliko hbr za ukweli
hahahahaaa chaUkucha, sisi si wachawi bali tunataka kuanzia walipoishia wengine, hatutaki kubaki gizani, kwa mfano tungependa kujua nini kilitokea tangu siku anapotea mpaka anapatikana, alikuwa wapi anafanya nin, alikuwa anakula nini? yani maswali ni mengi na wengi wetu hatutaki kujishughulisha nayo hivyo tunabaki palepale

Umeona chanzo cha habari si blabla kama zako, wameleta uthibitisho wa:

  1. Tukio zima tangu mwanzo hadi mwisho
  2. Mhusika mkuu wa tukio/mwathirika
  3. Wazazi
  4. Mazingira ya tukio
  5. Majirani
  6. Mamlaka ya usalama ya serikali
  7. Serikali ya mitaa
  8. Picha kadhaa za kuonyesha mazingira ya tukio kama ifutavyo;

  • Picha ya mwathirika
  • Picha ya Mama yake mzazi
  • Picha ya kaburi alilozikwa mara ya pili
  • Picha ya majirani

Kwa dondoo hizo zinathibitisha chombo kilicholeta habari ambako nimetohoa na kuileta hapa kimefanya utafiti wa kina tofauti na wewe unayeleta maneno yasiyo na utafiti wa kina ila blabla tu.
 
Hivyo ndivyo GPL walipaswa kufanya uchunguzi na kuandika ukweli halisi wa tukio lenyewe, kwa maelezo haya hakuna maajabu yeyote kuhusu kufariki na kuonekana akiwa hai.
Habari hizi ni za kweli ingawa mwandishi ameongeza chumvi ila tukio limetokea maeneo ya moshono arusha, na baba wa marehemu ni mwinjilisti wa makanisa ya KKKT usharika wa Mara. wakati binti huyu amepotea kulikuwa na mvua kubwa sana zikinyesha mkoani Arusha na binti huyu alikuwa ni mlokole na alipenda sana kwenda kwenye maombi radio safina kwa wale wakazi wa arusha na moshi wanafahamu, kutokana na tatizo lake la kurukwa na akili muda mwingine alitoka safina na kwenda kwa ndugu zake maeneo ya nduruma na wakati akirudi akaendele na safari zake hakufika nyumbani hali ilioinua taharuki kubwa nyumbani kwao. baada ya kutomuona kwa muda wa siku nne wakaamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola na ndipo walipopata taarifa kuwa kuna maiti maeneo ya nduruma ya msichana imekutwa mtoni na ikiwa imeharibika na wakazi wa huko hawaitambui na hakuna mtu kapotea maeneo hayo, baada ya kusikia hayo familia ya binti huyo iliamua kufunga safari mpaka huko na kukuta wakazi wa nduruma wameshaizika kwenye mfuko wa sulphate(kwa wakazi wa arusha na moshi) na kuoma ifukuliwe na polisi waliwaonyesha picha wakiwa wameitoa maiti hiyo ndani ya maji baba mzazi wa binti huyokutokana na binti yake kutoonekana kwa muda mrefu na taarifa kwamba binti yae alienda nduruma moja kwa moja alisema huyu ni binti yangu ingawaje mama alikataa na kusema binti yangu sio mnene hivi baba akasema kwa sababu imekaaa kwenye maji mda mrefu imevimba. kilichofuatia ni kuifukua maiti na kuiweka kwenye jeneza ikiwa kwenye mfuko wa huo wa sulphate na kwenda kijiji cha moshono kwa mazishi. Habari hizi si za kishirikina ila ni makosa tu yalifanyika na mpaka so watu waache kupotosha.mto nduruma ni mto mkubwa sio mferegi so maiti hiyo huenda imetoka mbali sana coz mpaka sasa hivi hakuna mtu mkoani arusha ameripoti kupotelewa na ndugu na polisi wanaendelea na uchunguzi kwa kuwasiliana na mikoa mingine.kaburi limeng'olewa tu msalaba na kuachwa kama lilivyo mpaka hapo uchunguzi wa polisi utakapo kamilika ila ndugu wa baba wa binti wanasema walisawazishe coz ni mkosi.source ni mimi mwenyewe coz nlikuwa mpaka eneo la tukio.
 
Concrete umekomelea msumali wa imani yangu ya kutosoma haya magazeti. Mmejione wenyewe huyo mwandishi alivyogeuza habari. Sijui shigongo na waandishi wake analipeleka wapi Taifa letu.... na wajinga wengi huyapenda haya magazeti... na yeye anazidi kuwasukumia gizani na kuwajaza hofu. Shindwa shigongo na kunasiku utalipa.
 
Maelezo binafsi yasiyojitosheleza yanatafsirika kama ni ya kutoholewa vijiweni kwa sababu maelezo yako hayajawa published kwa utaratibu wa vyombo vya public media, na umeshindwa kuleta ushahidi wa uchunguzi wako kama walivyoleta hawa waandishi ilikochukuliwa source ya habari hii. Sina kawaida ya kukubali maelezo ya mtu binafsi bila uthibitisho wa kinga ya public publication, hivyo naweza kudiriki kukuambia you are seriously wrong kwa vile hujaleta uthibitisho wa utafiti, kwamba unaishi karibu utatuthibitishaje kama si mtu unayejaribu kusafisha ukweli wa tukio hili?

Umeona chanzo cha habari si blabla kama zako, wameleta uthibitisho wa:
  1. Tukio zima tangu mwanzo hadi mwisho
  2. Mhusika mkuu wa tukio/mwathirika
  3. Wazazi
  4. Mazingira ya tukio
  5. Majirani
  6. Mamlaka ya usalama ya serikali
  7. Serikali ya mitaa
  8. Picha kadhaa za kuonyesha mazingira ya tukio kama ifutavyo;

  • [*=1]Picha ya mwathirika
    [*=1]Picha ya Mama yake mzazi
    [*=1]Picha ya kaburi alilozikwa mara ya pili
    [*=1]Picha ya majirani
Kwa dondoo hizo zinathibitisha chombo kilicholeta habari ambako nimetohoa na kuileta hapa kimefanya utafiti wa kina tofauti na wewe unayeleta maneno yasiyo na utafiti wa kina ila blabla tu.

Ndugu Candid Scope, wewe umepewa taarifa, mwenzio ni jirani ya sehemu ya tukio, kwa nini ushabikie uchawi? kwani amesema hakuna kaburi wala wazazi? Anachokataa ni kuhusisha ushirikina. Nadhani na wewe kama ni serious writer ungefanya upenguzi yakinifu na kubaini nani ni mwongo badala ya kushabikia kama unavyofanya sasa. Story ya Concentrate15 inanunulika ya kwako ina gaps kuna sehemu unakatika na hakuna uelekeo mzuri. Chunguza sana ndugu yangu maana si yote yaletwayo kama story ni ya kweli. Bila shaka wananchi wengi na hasa katika hali za UJIMA wangefurahi kununua magazeti yanayosema juu ya UCHAWI na haya yanafanywa ili matoleo ya GBL nyasomeke, kama nia ni hiyo HONGERA. Alamsiki
 
Habari hizi ni za kweli ingawa mwandishi ameongeza chumvi ila tukio limetokea maeneo ya moshono arusha, na baba wa marehemu ni mwinjilisti wa makanisa ya KKKT usharika wa Mara. wakati binti huyu amepotea kulikuwa na mvua kubwa sana zikinyesha mkoani Arusha na binti huyu alikuwa ni mlokole na alipenda sana kwenda kwenye maombi radio safina kwa wale wakazi wa arusha na moshi wanafahamu, kutokana na tatizo lake la kurukwa na akili muda mwingine alitoka safina na kwenda kwa ndugu zake maeneo ya nduruma na wakati akirudi akaendele na safari zake hakufika nyumbani hali ilioinua taharuki kubwa nyumbani kwao. baada ya kutomuona kwa muda wa siku nne wakaamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola na ndipo walipopata taarifa kuwa kuna maiti maeneo ya nduruma ya msichana imekutwa mtoni na ikiwa imeharibika na wakazi wa huko hawaitambui na hakuna mtu kapotea maeneo hayo, baada ya kusikia hayo familia ya binti huyo iliamua kufunga safari mpaka huko na kukuta wakazi wa nduruma wameshaizika kwenye mfuko wa sulphate(kwa wakazi wa arusha na moshi) na kuoma ifukuliwe na polisi waliwaonyesha picha wakiwa wameitoa maiti hiyo ndani ya maji baba mzazi wa binti huyokutokana na binti yake kutoonekana kwa muda mrefu na taarifa kwamba binti yae alienda nduruma moja kwa moja alisema huyu ni binti yangu ingawaje mama alikataa na kusema binti yangu sio mnene hivi baba akasema kwa sababu imekaaa kwenye maji mda mrefu imevimba. kilichofuatia ni kuifukua maiti na kuiweka kwenye jeneza ikiwa kwenye mfuko wa huo wa sulphate na kwenda kijiji cha moshono kwa mazishi. Habari hizi si za kishirikina ila ni makosa tu yalifanyika na mpaka so watu waache kupotosha.mto nduruma ni mto mkubwa sio mferegi so maiti hiyo huenda imetoka mbali sana coz mpaka sasa hivi hakuna mtu mkoani arusha ameripoti kupotelewa na ndugu na polisi wanaendelea na uchunguzi kwa kuwasiliana na mikoa mingine.kaburi limeng'olewa tu msalaba na kuachwa kama lilivyo mpaka hapo uchunguzi wa polisi utakapo kamilika ila ndugu wa baba wa binti wanasema walisawazishe coz ni mkosi.source ni mimi mwenyewe coz nlikuwa mpaka eneo la tukio.
Mkuu wewe ndo umeeleza ukweli! Ni vigumu sana kuijua sura ya mtu au alama zake aliyekufa siku 4,huyo hakuwa amekufa!
 
Matukio kama hayo si kwa Tanzania tu, nimewahi kushuhudia kwenye vyombo vya habari matukio mawili ya aina hiyo nilipokuwa nchini Marekani, ingawa huko watoto waliopotea na kisha kufika nyumbani wakiwa wamepoteza uwezo wa ufahamu na utambuzi baada ya miaka mitatu au minne hadi walipopelekwa hospitalini kwa matibabu, lakini mazingira ni yayo hayo. Mhusika alishikwa na sijui baadaye kilichoendelea. Mambo haya yapo tusijaribu kutelezesha ukweli.

Hapooo ndipo nilitaka uchunguze maana hapa umesema mwenyewe "Mhusika alishikwa na sijui baadaye kilichoendelea" hakuna kilichoendelea kwa kuwa ilikuwa porojo za kuuza matoleo yao. Uelewe ndugu. Alamsiki
 
inabidi tumtanguliize mungu katikaa kila jambo letu na kila siku ya maisha yetu binafsi najua kama uchawi upo ila siupi nafasi hata kidogo katika maisha yangu only God will protect me
 
Hili tukio sio la kishirikina. Wala lisihusishwe na ushirikina kabisa. Huyu binti alitoka kwa mvulana wake na baba yake alipomfokea akakasirika akarudi huko kwa jamaa yake. Sasa suala la kuchukuliwa msukule sijui linatoka wapi.
Ni ubishi tu wa huyo Mwinjilisti Obedi. Watu walimshauri kama hana uhakika na mwanaye bora asizike asubiri kwanza. Yeye akasema roho wa mungu amemuongoza. Kumbe mwanaye yuko hai.
 
Ndugu Candid Scope, wewe umepewa taarifa, mwenzio ni jirani ya sehemu ya tukio, kwa nini ushabikie uchawi? kwani amesema hakuna kaburi wala wazazi? Anachokataa ni kuhusisha ushirikina. Nadhani na wewe kama ni serious writer ungefanya upenguzi yakinifu na kubaini nani ni mwongo badala ya kushabikia kama unavyofanya sasa. Story ya Concentrate15 inanunulika ya kwako ina gaps kuna sehemu unakatika na hakuna uelekeo mzuri. Chunguza sana ndugu yangu maana si yote yaletwayo kama story ni ya kweli. Bila shaka wananchi wengi na hasa katika hali za UJIMA wangefurahi kununua magazeti yanayosema juu ya UCHAWI na haya yanafanywa ili matoleo ya GBL nyasomeke, kama nia ni hiyo HONGERA. Alamsiki

Nani mkweli mropokani na public media?
 
Hapooo ndipo nilitaka uchunguze maana hapa umesema mwenyewe "Mhusika alishikwa na sijui baadaye kilichoendelea" hakuna kilichoendelea kwa kuwa ilikuwa porojo za kuuza matoleo yao. Uelewe ndugu. Alamsiki

Msichana anaeleza mkasa yaliyompata siku ahaondoka na kilichotokea kupoteza uelewa aliko hadi siku anafika nyumbani, sasa utetezi wenu ujajengeka kwenye hoja ipi?
 
inabidi tumtanguliize mungu katikaa kila jambo letu na kila siku ya maisha yetu binafsi najua kama uchawi upo ila siupi nafasi hata kidogo katika maisha yangu only God will protect me

Kumbuka kuna ufalme wa ibilisi ambao ni nguvu za gizani na utawala wa Mungu wenye nguvu za mwangani.
 
View attachment 160991Witness Obedi aliyefariki View attachment 160992Kaburi lake View attachment 160993Akiwa na wazazi kisha tukio View attachment 160994Majirani walioomboleza msiba wake wafika kushangaa tuko hilo

Tukio la pekee ambalo linaonekana ni la kishirikina huko Arumeru/Arusha ni pale msichana Witness Obed ambaye inaelezwa alifariki na kuzikwa mara mbili ametokea nyumbani akiwa hai kwa wazazi wake na kisha kusimulia mkasa wa tukio ulivyomtokea. Mkasa huo ulitokea baada ya binti huyo kurudi toka chuo na kufika nyumbani saa mbili jioni akiwa amechelewa ndiyo iliyokuwa sababu ya kugombezwa na familia yake hasa babake mzazi.

Mzazi wake anasema alimgombeza, hivyo binti akatoroka. Binti huyo hakurudi na siku iliyofuata wakatoa tangazo la kumtafuta kupitia vyombo mbalimbali vya habari na sheria. Baadaye walisikia katika kijiji kingine walimwokota msichana aliyefariki. Walipoenda kuuliza waliambiwa alishazikwa.

Wakaenda kuomba kibali polisi cha kufukua kaburi ili kubaini kama ni binti yao, baada ya kupata kibali na kufukua kaburi waliitambua maiti kutokana na alama ambazo aliwa nazo wakati akiwa hai. Wakauchukua mwili huo na kwenda kufanya matanga kwao na kuuzika upya kwenye kaburi jingine.

Baada ya kuondoka alifika kwenye nyumba moja na kumkuta mama mmoja, aliomba maji ya kunywa. Alipewa na alipokuwa anakunywa mama yule alikuwa anamsimamia, lakini alipoonja na kuona machungu alikataa, lakini mama yule alimlazimisha kwa kumnywesha hadi akamaliza kisha akapoteza fahamu na hakujua nini kinaendelea na wapi aliko hakujitambua.

Anasema baadaye hajitambui amefikaje nyumbani, na mama yake alipomwona mara ya kwanza akifika alikimbia kufikiria anaona mzuka. Lakini baadaye alijipiga moyo konde na kumjongea binti yake.

Kuna matukio kadhaa yametokea siku za karibu huko kanda ya Ziwa na kwingineko kwa matuko kama haya, kuna kila dalili ya mchezo wa kishirikia.

Polisi wamesema wanataarifa juu ya tukio hilo na wanalifanyia uchunguzi wa kina.

Source: Global Publishers.

JamiiForums,Acheni uzushi,ndani ya futi 6 chini ya udoongo,hakuna anayeweza kutoka humo,atausukumaje huo udongo,na hilo jeneza atalifunguaje??!!Acheni upotoshaji huu!!!Au mna ka-interest?
 
JamiiForums,Acheni uzushi,ndani ya futi 6 chini ya udoongo,hakuna anayeweza kutoka humo,atausukumaje huo udongo,na hilo jeneza atalifunguaje??!!Acheni upotoshaji huu!!!Au mna ka-interest?

Ukiamua kubaki ndani ya box we endelea. Vigumu kuuelewa utawala wa ibilisi ambao ni nguvu za giza.
 
Back
Top Bottom