msichana wa sura nzuri
Lady doctor
kitu gani kinakufanya usiolewe
elimu unayo ya kutosha
hata ng'ambo ukaenda ukarudi
msichana wa urembo kama wewe
Lady doctor
uonyeshe mapenzi kwa vijana kama
Chimbuvu
ukionyesha majivuno kwa vijana kama
manoah
utazeeka ukiwa nyumbani kwenu
ooh baby, miaka yaenda mbio sana
na sura yako nayo ikichuchuka
ooh baby, miaka yaenda mbio sana
na sura yako nayo ikichuchuka
pengine tabia zako ndizo mbaya
awali kweli dada ulijivuna
kwanza
Arushaone alitaka akuoe
ukaringa ati hana masomo babu
Bishanga ndio rika lako
ooh baby, ona watoto wa nyuma yako
Passion Lady,
mimisa
wameolewa wamekuwacha ukihangaika
ooh baby, ona watoto wa nyuma yako
wameolewa wamekuwacha ukihangaika
msichana wa sura nzuri
kitu gani kinakufanya usiolewe
elimu unayo ya kutosha
hata ng'ambo ukaenda ukarudi