Faida na hasara za kuoa mwanamke msomi na mwenye kazi na kipato kizuri

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Kumekuwa na maoni mbalimbali toka kwa wadau juu ya mada hii:

Je, kuoa mwanamke mwenye elimu nzuri na kazi nzuri au mwanamke asiye na elimu kubwa na mama wa nyumbani - ni lipi jambo sahihi?

Maoni ya wanaume wengi yana mitizamo tofauti na pengine ni kupitia mjadala huu hata wanawake pia watatoa maoni yao kueleza mtizamo wao na hata kuweza kupata mjadala wenye tija kwa wadau mbalimbali wanaotaka kufanya maamuzi kabla ya kuoa/olewa.

Karibuni kwa mjadala!
 
Eti jamaa mmoja anasema heri kuoa ambaye hajasoma maana hatamtesa, anadai kwamba wasomi wana majidai, majigambo na najidai kujua sana. Kwa upande wangu naona ukipata msomi na mwenye ufahamu mpana mtasaidiana katika mengi na hatakutegemea wewe tu kwa kila kitu, nimsaidieje huyu jamaa ili anielewe?
 
mwambie afumbe macho na achague. kwani mtu unaweza kumwambia mtu ampende nani, si asikilize moyo wake?
 
mwambie afumbe macho na achague. kwani mtu unaweza kumwambia mtu ampende nani, si asikilize moyo wake?

Huwezi jua,labda kaenda kwao porini kakuta wame pangwa hapo,..
mmoja msomi,mwengine sio msomi so anatakiwa achague.....
 
maswali mengine bana....unajua wapo walioacha wasomi wakenda kuoa wasio wasomi wakawaendeleza wakawa mwiba mchungu sana baada ya kupata elimu na kupata maisha bora....mimi nasema,mke mwema mtu hupewa na Mungu,achukue muda awasome wote wawili...aamue mwenyewe kwa kufahamu yupi anampenda zaidi na yupi kati ya hao wasichana anampenda yeye zaidi......!! ningekuwa mwanaume ningeoa msomi anayenipenda kweli na ninayempenda!
 
Muombe mungu akupe mke mwema!

I love that,hahahaha!
Hauhitaji kurusha shilingi juu ili ujue nani ata kufaa,Mungu atakuonesha nani atakua mke mwema!
Najua wengi watakimbilia kusema kua msomi ndo anafaa,...
ila yawezekana huyo msomi akafanya uishi kama uko ahera na hujafa,..
Huyo asiye msomi anaweza kua anakupenda kwa dhati,na kama unataka awe msomi ukaweza kumuendeleza kielimu vile vile!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom