Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,800
Ni ndoto za wanaume wengi kuoa mwanamke mrembo na mwenye kipato ili wasaidiane kutengeneza familia bora ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba nzuri, kusomesha watoto kwenye shule bora n.k Hapo ndipo baadhi ya vijana hufikiria kuoa wanawake wasomi wenzao wenye kazi nzuri. Lakini kabla ya kufikiria kuoa mke msomi na mwajiriwa( hasa serikalini) ni vema ukajua faida na hasara zake.
Tukianza na faida
1. Mke mwajiriwa atakusaidia kuongeza kipato kwa maendeleo ya familia.
2. Pili,km hali yako ya kiuchumi ikiyumba,familia inaweza isiathirike na kama itaathirika basi ni kidogo.
3. Kazi/cheo cha mkeo kinaweza kuleta heshima fulani ndani ya familia.
Hasara zake:-
1. Kuna baadhi ya wanawake akichangia hela yake kununua kitu mfano kiwanja usishangae siku mkikosana akakudhalilisha kwamba kiwanja kanunua yeye au nyumba kajenga yeye.
2. Wanawake waliosoma na wenye kazi wengi wao (SI WOTE ) huwa si watiifu kwa waume zao hasa ikitokea kipato chake ni kikubwa kuliko mme.
3. Jiandae na mivutano ya haki sawa. Kuna baadhi ya wanawake wasomi huigeuza ndoa kuwa sehemu ya kufanya uanaharakati. Hali hii inaweza kuibua mivutano ya mara kwa mara.
4. Ndoa kuongozwa na vichwa 2. Maandiko yanasema, "Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe" Efeso 5:23.
Kuna baadhi wanawake wakishasoma na kuwa na ajira nzuri hujipa mamlaka ndani ya nyumba. Badala ya mume kuwa sauti ya mwisho kimaamuzi atataka yeye awe msemaji wa mwisho. "In nature"wanaume hatuko tayari kutawaliwa na mwanamke hapo inaweza kuwa chanzo cha ndoa yenu kusambaratika.
5. Ndugu wa mke kukudharau/ kutokupa heshima unayostahili hasa km familia yao ni ya kishua na wasomi.Hebu fikiria mkeo ni mkuu wa kitengo muhimu aafu wewe Mwalimu wa shule ya msingi( mfano tu), Usishangae kwa baadhi ya matukio ukawa wa mwisho kupewa taarifa. Tena usiombe iwe familia ya Kihaya( kidding).
6. Watoto wakigundua mama yao ana pesa nyingi kuliko baba heshima yao kwako inaweza shuka na usishangae kuona shida zao nyingi wanamalizana na mama yao. Hapa usipokuwa makini unaweza jikuta kama umetengwa ndani ya nyumba yako.
Kuna afande ni rafiki angu hiki kimemkuta, watoto hawana time nae kabisa.
7. Usitegemee neno pole na kazi au kupokewa mzigo utokapo kazini. Mwanamke mwenye kazi anajiona hata yeye ni mtafutaji. Hivyo anaweza asione sababu ya kukupokea kwani hata yeye katoka kutafuta huo mkate.
8. Kuna wakati "Stress"za kazini anaweza kuzihamishia nyumbani. Hapo ndo hatari maana anaweza kukosa hata hamu ya kukupa unyumba.
9.Kuleta ubosi kitandani. Wanawake wengi wenye kazi na mabosi hujisahau na kuleta ubosi wao hadi nyumbani. Hivyo mkiwa faragha usishangae kauli za kibabe na wengi wao hawawezi kuwa romantic.
Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo mengi nimejifunza kwa brother yangu aliyeoa Daktari mwenzake mwenye cheo kikubwa kuliko yeye na kwa baadhi ya wafanyakazi wenzangu.
NB: Niko tayari kurekebishwa.
Pia soma hoja hii ilivyojibiwa: Kamgomoli: Mwanamke wa Miaka ile sio Mwanamke wa leo