Msiba wa Musiba: When you become public enermy

Unapogeuka kuwa adui wa hadhira ni kheri ufe kuliko kuendelea kuwa hai...hakuna gundu baya kama kuchukiwa na hadhira.. Fikiria kila roho ikupe laana yake.. Huo ni msiba mara saba kama roho tisa za paka

Unajua tuna watu wengi sana wamesoma lakini hawajaelimika
Haijalishi umesoma mabuku mangapi
Haijalishi umemaliza vyuo vingapi
Haijalishi umefaulu mitihani mingapi
Haijalishi umetunukiwa shahada ngapi
Swali muhimu... Je umeelimika?

Tuna watu wengi tu wenye uelewa kimo cha mbilikimo pamoja na kutumikia muda mwingi kwenye elimu, wamefaulu darasani wamefeli mitaani...
Chuo halisi cha kufaulu ni chuo cha maisha halisi
Musiba ana misiba mingi sijui ataanza na upi na kumaliza na upi
Ana msiba wa maadui aliojitengenezea
Ana msiba wa wale wote aliowatukana na kuwakejeli
Ana msiba wa wale wote aliowazushia tuhuma mbalimbali
Ana msiba wa kesi zilizoko mahakamani
Ana msiba wa wale wote ambao kupitia matamshi na matendo yake waliumia na kuumizwa kwa namna moja ama nyingine
Ana msiba wa hatima yake
Juu ya yote ana msiba wa mbeleko, mfadhili na mlinzi wake...!!!

Madhila yake yatakuwa ni bandika bandua..
Kila jambo lina nyakati zake
Kuna wakati wa kulia na kuna wakati wa kucheka
Ukilia leo kesho utacheka na kinyume chake!!!
View attachment 1745614
Sema unamchukia ww! Wengine tunampenda na kumuheshimu!
By the way huyo HK anaganya n8n8 tenaaa! Hii tiba imethibitishwa na wataalam gani wa ulaya, mbona ametulia hivišŸ¤£šŸ˜‚šŸ¤£!
 
Utateseka mwenyewe! Musiba ni shujaa wa Tz, kubali kataa, ukweli ndio huo! Stay blessed my brother MusibašŸ™!
Na JK Gang sasaiv litawashugulikia wote kimya kimya mliokuwa mnamtukana. Na kazi imeshaanza. Piga mchungaji na kondoo watasambaratika
 
Hii picha ya kweli au yakupikwa mbona huyo Ni Kama doctor au
Ni Dokta mwenyewe huyo! Mwanasayansi mnafiki na kigeugeu! Leo anamponda Bosi wake kwa kuanzisha Nyungu pale Muhimbili, na wakati hapo kabla akiwa Waziri wa Utalii na Maliasili alitaka hizo Nyungu ziwepo huko kwenye vituo vya utalii kama moja ya njia za kumuunga mkono Bosi wake!

Hapo pichani alikuwa eti anazindikwa na Wazee wa Kimila! Yaani na Udaktari wake, bado anaamini katika uchawi na ushirikina!!!
 
serikali ya watu wa twitter chini ya "bwana fulani" imeapa kuendelea kumpiga spana na kumsagia kunguni mpaka pale Mungu atakapo mpenda zaidi

binafsi nimejifunza jambo kuhusu musiba. tuache tabia ya unafiki, uchawa na kujipendekeza kwa watu wenye madaraka au wenye kipato kikubwa.

huyo unayefanya uchawa kwake siku akifa, kupoteza madaraka au kufilisika unabaki peke yako ukiwa huna wa kukutetea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema unamchukia ww! Wengine tunampenda na kumuheshimu!
By the way huyo HK anaganya n8n8 tenaaa! Hii tiba imethibitishwa na wataalam gani wa ulaya, mbona ametulia hivi!
 
Funzo ni kwamba tumsitegemee mwanadamu kama nguzo yetu maana naye ni mwanadamu tu na siku zake si nyingi. Kitabu cha Mungu kinasema katika Jeremiah 17:5-8 kama ifuatavyo:-
5 BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake
Na moyoni mwake amemwacha BWANA.
6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto;
Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi;
Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.
 
Atakuwa anajifungia mashambani huko siku hizi.
IMG-20210407-WA0008.jpg
 
Unapogeuka kuwa adui wa hadhira ni kheri ufe kuliko kuendelea kuwa hai...hakuna gundu baya kama kuchukiwa na hadhira.. Fikiria kila roho ikupe laana yake.. Huo ni msiba mara saba kama roho tisa za paka

Unajua tuna watu wengi sana wamesoma lakini hawajaelimika
Haijalishi umesoma mabuku mangapi
Haijalishi umemaliza vyuo vingapi
Haijalishi umefaulu mitihani mingapi
Haijalishi umetunukiwa shahada ngapi
Swali muhimu... Je umeelimika?

Tuna watu wengi tu wenye uelewa kimo cha mbilikimo pamoja na kutumikia muda mwingi kwenye elimu, wamefaulu darasani wamefeli mitaani...
Chuo halisi cha kufaulu ni chuo cha maisha halisi
Musiba ana misiba mingi sijui ataanza na upi na kumaliza na upi
Ana msiba wa maadui aliojitengenezea
Ana msiba wa wale wote aliowatukana na kuwakejeli
Ana msiba wa wale wote aliowazushia tuhuma mbalimbali
Ana msiba wa kesi zilizoko mahakamani
Ana msiba wa wale wote ambao kupitia matamshi na matendo yake waliumia na kuumizwa kwa namna moja ama nyingine
Ana msiba wa hatima yake
Juu ya yote ana msiba wa mbeleko, mfadhili na mlinzi wake...!!!

Madhila yake yatakuwa ni bandika bandua..
Kila jambo lina nyakati zake
Kuna wakati wa kulia na kuna wakati wa kucheka
Ukilia leo kesho utacheka na kinyume chake!!!
View attachment 1745614
we nae huwa hujitambui kama kichaa fulani hivi, Haya kama Musiba ameudhi wengi je Kigogo2014 na Mange wameudhi wangapi? acha chuki zako binafsi na Musiba endelea na kazi yako ya uganga wa kienyeji, ndio maana Umekimbia Dar ukahamia mkoani kutibu watu kwa mitishamba, kufilisika kubaya sana
 
Back
Top Bottom