Sheikh Mwaipopo ni Musiba wa kipindi cha Samia?

Dr Restart

JF-Expert Member
Jul 15, 2021
3,298
17,155
Wasalaam.

Kupitia wimbi la Ubinafsishwaji wa Bandari, kumeibuka na makundi kadhaa. Lakini kuna huyu anayejiita Sheikh Mwaipopo.

Kwanza, wakati wa uongozi wa awamu ya tano kuna mtu aliyejiita Mwanaharakati Musiba. Mtu huyu kwa mwamvuli alitumia vyombo vyake vya habari (online tv na magazeti) kuwavamia na kuwatusi wale wote wenye mawazo kinzani na yale ya Boss wake, Magufuli.

Hivi majuzi Sheikh Mwaipopo, chini ya Ukatibu wa Baraza la Habari la Waislamu Tanzania (BAHAKITA), pamoja na kutumia mwamvuli wake wa dini ya Kiislamu kutetea Sakata la Bandari na Rais Samia kwa ujumla.

Juzi alimshambulia na kumuonya Prof Shivji kuwa hajawahi kuunga mkono mambo yote yanayofanywa na serikali. Nipo hapa kujiuliza, je tunalazimishwa kuunga juhudi mambo yote ya serikali. Uhalali wa kukosoa ni mpaka uwe ulishasapoti hapo kabla?

Amemkejeli zaidi kwa ubaguzi wake na kuita amepata upendeleo wa makusudi kwa sababu ya Uhindi wake. Na wala si kwa sababu ya utaalam wake.

Musiba alianza kidogo kidogo na baadae akawa dubwana kubwa. Lakini, ya kheri yeye alitumia vyombo vyake na wala hajajivika ngozi ya udini.

Je, dini ya Kiislamu kwa ujumla wake imeridhia hatua hizo (kubagua na kukejeli) anazochukua Sheikh Mwaipopo? Kwa kuwa anaongea kwa niaba ya vyombo vya habari vya dini husika?

Sheikh Mwaipopo asimame yeye pekee yake. Asitumie Mwamvuli wa dini yake katika kufanikisha ushwetwani. Na kama ataendelea basi itambulike ni kwa niaba ya dini nzima ya Kiislamu.

Musiba ana kesi kede kede mahakamani. Akihitajika kulipa Mabillion ya fedha, ujeuri wote umepukutika baada ya Boss wake kufariki.

Sheikh aenende kwa kunyata. Siku Samia atafariki, atapelekwa mahakamani na kulipishwa kiwango kikubwa cha fedha. Je, waislamu mtamchangia?
 
Sheikh njaa yule sijui kapata wapi guts za kumsema shivji

Ila najua ataitwa na ataonywa
 
Asipewe airtime huyo Mbwiga hakuna sheikh hapo zaidi ya muhuni muhuni tu mjaza utumbo mpana.
 
Ana elimu ya aina gani? Isije kuwa qualification yake kapata kwa kutukana na kushambulia dini za watu.
Ukisikiliza anachoongea, unaelewa fika amejaa ujinga mwingi na uwezo wake kiakili ni mdogo sana.
Tumsamehe bure
 
Back
Top Bottom