Msiba wa Kijana Abas

Pole sana dear...
Aliniambia jinsi ulivyokuwa unaenda
Kumuona mara kwa mara, jinsi mlivyokuwa
Mnacheka, na pale ulipofikisha ile michango
Ya wana JF..

Mara ya mwisho nlivyoongea nae aliniambia
Afadhali hajavimba mdomo ili aweze
kupiga porojo na kutuchekesha.. na aliniambia nisimuonee huruma bali nimuombee na niwe na imani..

Kwa kweli Abbasi alikuwa kijana wa aina yaki
Pekee.. na nimejifunza mengi kutoka kwake.
I will miss you my dear friend ..
Pole sana sweetie! Mipango ya Mungu haina makosa!
 
Pole sana dear...
Aliniambia jinsi ulivyokuwa unaenda
Kumuona mara kwa mara, jinsi mlivyokuwa
Mnacheka, na pale ulipofikisha ile michango
Ya wana JF..

Mara ya mwisho nlivyoongea nae aliniambia
Afadhali hajavimba mdomo ili aweze
kupiga porojo na kutuchekesha.. na aliniambia nisimuonee huruma bali nimuombee na niwe na imani..

Kwa kweli Abbasi alikuwa kijana wa aina yaki
Pekee.. na nimejifunza mengi kutoka kwake.
I will miss you my dear friend ..

AD unayosema ni kweli........alikuwa mcheshi sana ukienda kumwona hutamani kuondoka..... alifurahi sana alipopata michango toka JF japokuwa alikuwa hajui JF ni nini , nilimweleza na akafurahi akasema akipona atajiunga na kuwasalimu wote
 
ad unayosema ni kweli........alikuwa mcheshi sana ukienda kumwona hutamani kuondoka..... Alifurahi sana alipopata michango toka jf japokuwa alikuwa hajui jf ni nini , nilimweleza na akafurahi akasema akipona atajiunga na kuwasalimu wote
poleni sana dada zangu mliokuwa mnaenda kumuona ... I realy know how you feel right now
 
ina lilah wainailahii raj'uun Allah akulaze mahala pema Abas
 
Aliyevimba mguu afariki *Send to a friend
Thursday, 13 October 2011 20:24
0
digg

Daniel Mjema,Moshi
MGONJWA Abbas Abdallah, mkazi wa Kiru Ndogo, wilayani Babati mkoani Manyara, aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, kufuatia kuvimba mguu wake mmoja, amefariki dunia.Abbas alifariki dunia dunia saa 4:00 usiku wa juzi akiwa katika chumba cha* wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu, baada ya madaktari kumfanyia upasuaji wa mguu wake.
*
Habari zilisema Abbas, alifariki saa 13 baada ya jopo la madaktari wa KCMC kumfanyia upasuaji ulioambatana na* kukata nyama zilizokuwa zimevimba.Baba mzazi wa marehemu, Abdallah Juma na kaka mkubwa wa marehemu, Seleman Abdalah, walilithibitishia Mwananchi jana kuhusu kufariki kwa kijana huyo.

“Ni kweli kwamba amefariki dunia na sasa ndio tumepata gari tunajaribu kama Mungu akipenda tuweze kumsafirisha leo (jana),* kwenda Kiru Ndogo kwa mazishi kesho (leo),”alisema baba yake.

Mzazi huyo alisema mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya Hood, Mohamed Hood, ambaye ni mmoja wa wafadhili wakuu wa marehemu, ametoa gari la kumsafirisha hadi kijijini kwao kwa mazishi.Kaka wa marehemu, Seleman ambaye alikuwa akimuuguza marehemu, alisema mdogo wake walichukuliwa saa 3:00 asubuhi juzi na kupelekwa chumba cha upasuaji.

“Baada ya upasuaji ambao nilielezwa na wauguzi kuwa madaktari walimkata mguu ili kupunguza nyama, alipelekwa ICU ambako hakuna mtu anaruhusiwa kuingia,”alisema.“Ilipofika saa 1:00 usiku jana (juzi) nilikwenda nikamuona kupitia* vioo akiwa na mashine na moja iliyokuwa akipiga sana alarm (sauti),ikuelewa nikabaki kumuomba Mungu”.

Seleman alifafanua kuwa baadaye alipitiwa na usingizi na alishtuliwa na muuguzi mmoja ambaye alimwamsha na kumuuliza kama alikuwa amekwenda kumuona tena mgonjwa.

Kwa mujibu wa Seleman, muuguzi huyo ambaye hamfahamu kwa jina, alimwambia kuwa alipaswa kwenda tena kumuangalia mdogo wake ili kujua hali yake.

*“Nilikwenda ICU nikagonga mlango muuguzi akaja nikamwambia mgonjwa wangu anaendeleaje akaniambia kuna tatizo kidogo madaktari wanahangaika nalo,”alisema.

Alisema akiwa amesimama nje ya ICU aliona kitoroli kinachotumika kutoa maiti wodini kikiingizwa katika wodi hiyo na hapo ndipo aliposhuku kuwa mdogo wake hayupo tena duniani.“Baada ya muda mfupi kidogo akaja muuguzi mwingine akaniambia naitwa ndani na ndio wakaniambia mdogo wangu amefariki na wakanifunulia nikauona mwili wake,”alisema.

Siku moja kabla ya kufanyiwa upasuaji huo, Abbas akisema anaamini baada ya upasuaji huo angerejea katika hali yake ya kawaida na kuwa kama binadamu wengine.

“Kama sio Mwananchi* ningefia kijijini lakini nawashukuru wameandika habari zangu na nimepata wasamaria wema akiwemo Hood ambaye ni msaada mkubwa kwangu,”alisema kaka yake akimkariri mdogo wake.

Kwa mujibu wa ndugu, huyo mdogo wake aliwahi kusema kuwa haelewi cha kumlipa Hood ambaye amegharamia chakula na gharama za matibabu ikiwamo sh7 milioni ambazo alisema ni gharama kwa ajili ya upasuaji huo.

Alisema tangu ugonjwa huo umtokee mwaka 2005 ulipoanza kama uvimbe mdogo wa kawaida, hajawahi kupata msaada kama alioupata baada ya Mwananchi kutoa habari zake.Lakini pamoja na matarajio ya Abbas kurejea katika hali ya kawaida ya binadamu, ndoto yake imeyeyuka kama mshumaa wakati madaktari wakijaribu kufanya ndoto yake kutimia.

Kufikishwa hospitalini kwa marehemu, kulitokana na jitihada kubwa zilizofanywa na kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), kuandika habari za Abbas.

Baadaye MCL kwa kushirikiana na Benki ya CRDB Limited, walimfunguliwa akaunti Abbas katika Tawi la Moshi ambayo ilitumiwa na wasamaria wema kupitishia fedha za msaada.

Katika kufungua akaunti hiyo,CRDB walilegeza* masharti ya kufungua akaunti yanayotaka mteja kufika mwenyewe benki na ikatoa msaada wa sh150,000 za kufungulia akaunti.
 
Hii stori kwenye gazeti la mwananchi imeniumiza sana .... Leo ningekuwa msichana ningelia sana .... Rip boy.....
Poleni sana blaki , Afro d na wengine mlioguswa kwa ukaribu
 
Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu, apumzike kwa amani! Amen!
 
Mungu amjaalie makazi mema ya milele.

Pole kwa wote walioguswa na hili kwa namna moja au nyengine
 
RIP mpendwa Abas,

hii imekuwa ndiyo siku yako. sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu, tumetoka kwake na kwake siku moja tutarejea.

amina
 
Hii habari imenisikitisha saana... Amefariki huyu kijana.

Namshukuru saana Vikwazo kwa kuweka Uzi wa taarifa
za ugonjwa wa Marehemu... Namshukuru AfroDenzi kwa
jitihada zake za kukusanya chochote toka kwa JF members
Nashukuru Pia ushirikiano wa Maxence katika issue yoote..
Na nakushukuru pia Blacki Woman kwa moyo wako wa upendo
na from the post i see kua ulikua nae karibu... Mungu awabarik
saana awezeshe kukuza Mioyo ya Upendo mlo nayo.

REST IN PEACE ABBASI...
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom