Msiba niliouhudhuria leo...

Msiba niliouhudhuria leo...

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,442
Leo majira ya mchana nimepigiwa simu na rafiki yangu akinijulisha msiba uliompata mdogo wake kutokana na hizi mvua zinazoendelea kunyesha hapa jijini Dar.

Mdogo wa huyu rafiki yangu amempoteza mkewe na watoto wake wawili. Wa kike mwenye umri wa miaka 7 na wa kiume mwenye miaka 5, ambao walifariki jana alfajiri kwa kuangukiwa na ukuta huko Kimara Temboni. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, na wanatarajia kusafirisha maiti hao kwenda Kilimanjaro kwa mazishi kesho mchana.

Nilibahatika kuzungumza na mume wa marehemu hao, ingawa tukio hilo limemchanganya, lakini alimudu kunisimulia mkasa mzima ulioikumba familia yake. Siku hiyo ya jana yeye na mkewe waliamka alfajiri kama kawaida yao wakaswali swala ya asubuhi, na kisha akajiandaa kwenda kazini, lakini wakati anataka kuondoka mkewe akamzuia asiondoke na mvua, hivyo akaamua kukaa sebuleni. Wakati huo huo mkewe akawachukua watoto wake wawili na mtoto mmoja wa wifi yake ambaye amekuja likizo kuwatembelea na kuwahamishia chumbani kwao. Ghafla mume akasikia kishindo kikubwa akiwa hapo sebuleni, akadhani ni radi.Lakini akajiwa na wazo achungulie chumbani, alipofunua pazia akakuta ukuta umemuangukia mkewe na watoto pale kitandani, aliwahi kumuokoa mtoto wa dada yake tu kwani yeye hakubanwa sana na ule ukuta lakini akashindwa kumuokoa mkewe na hao wanae wawili kutokana na ukuta ule kuwa na kufusi. Alinieleza kwamba chanzo cha ukuta huo kuanguka ni kutokana na ngema kukatika na kuuangukia ukuta wa nyumba yake na hivyo kusababisha kazi ya uokoaji kuwa ngumu.

Nimeguswa sana na msiba huu kwa sababu nimekuwa karibu sana na familia hii………Mwenye enzi Mungu aziweke roho za marehemu hawa mahali pema peponi…………… Amina.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pole Mtambuzi na mfikishie rafiki yako salamu zangu za pole kwa kupata msiba huo mzito. Ni vigumu kuamini kama mvua hii imeleta maafa kiasi hichi. Wapumzike kwa amani....Amina
 
Pole sana wafiwa ma mungu azilaze roho za marehem mahala pema peponi, Amina.
 
Pole Mtambuzi na mfikishie rafiki yako salamu zangu za pole kwa kupata msiba huo mzito. Ni vigumu kuamini kama mvua hii imeleta maafa kiasi hichi. Wapumzike kwa amani....Amina

Ni kweli ni msiba mzito kwa huyu kijana, yaani we acha tu.......... nilijikuta nikitokwa na machozi pale alipokuwa analia kwa uchungu akimtaja mkewe na wanae kuwa wamemuacha mkiwa asijue la kufanya..........................ni jambo la kusikitisha kwamba analazimika kuanza maisha mapya bila familia ambayo aliizoea.
 
Pole sana. Nafikiri hizi namba tunazopewa na serikali (waliofariki) ni ndogo sana kulinganisha na iadi ya kweli.
 
pole mtambuzi jitahidi kumfariji huyo rafiki hilo ni pigo kubwa maishani kulistahimili
 
mhh jamani inasikitisha sana. Poleni sana wafiwa

RIP wote waliotangulia mbele ya haki
 
ni story inayohuzunisha mno,Mungu awalaze mahali pema peponi..amen
 
Innalillah wainna ilayh rajiun. Mungu atampa subra rafk yako Inshaallah. Mpe pole zetu kwa niaba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom