Mshkaji wa Ghetto akaharibu mbaya…!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
swanga2.JPG

Nilikuwa maarufu kijijini kuliko kawaida...(Picha haihusiani na habari hii)

Ilikuwa ni mwaka 1999 baada ya kumaliza masomo yangu ya kidato cha nne na kuangukia pua ndipo nilipokuja mjini na kufikia kwa shangazi yangu maeneo ya Temeke Mikoroshini Kwa Mpelumbe. Baada ya kusota bila kazi kwa muda mrefu kidogo, niliamua kuhamia ghetto kwa washkaji zangu na kuanza kubangaiza na biashara ndogo ndogo za kimachinga.

Nilimudu kidogo kujikusanyia fedha na kila ninapoenda kijijini nilikuwa najipiga viwalo vya mitumba na kutamba kwamba mimi ni mfanya biashara mkubwa hapa jijini Dar. Kwa kuwa nilikuwa natembeza nguo za Mitumba, ilikuwa rahisi kwangu kupiga pamba za nguvu hivyo kuweka mazingira ya kuaminika kwamba kweli mimi ni mfanyabiashara mkubwa. Kwa hiyo kila ninapoenda kijijini najitahidi kuwaonyesha wanakijiji kuwa mambo yangu sio mabaya. Hata hivyo kwenye familia yetu walikuwa wanaujua ukweli kwamba nilikuwa choka mbaya.

Siku moja nikiwa kijijini nikiwa nawanunulia jamaa zangu pale kijijini bia nilikuwa natamba sana kwamba huku jijini Dar ninamiliki maduka ya kuuza spea za magari na wapo niliowaahidi kuwapa ajira. Kutokana na kutamba kwangu na kumwaga kwangu ofa, nilijikuta nikiwa nimezungukwa na wapambe kibao, huku totoz kama kawa zikiwa nazo hazichezi mbali. Nilikuwa nawabadilisha mabinti kama nguo kwani walikuwa wakinizimikia kutokana na maujiko yangu.

Wakati bado nikiendelea kumwaga ofa za bia huku nikiendelea kujimwagia maujiko mara akaja jamaa mmoja. ‘Duh, umekuja mshkaji, mimi niko hapa tangu wiki jana.' Alisema yule jamaa.

Huyu jamaa tulikuwa tunabangaiza wote mjini na tulikuwa tunaishi ghetto moja tukiwa tumelundikana kama watu sita katika chumba kimoja. Ukweli ni kwamba sikujua kwamba mshkaji naye ni mwanakijiji wa pale kijijini kwetu, ingawa najua ni mwenyeji wa wilaya yetu. Ni kweli wiki mbili zilizopita alituaga kwamba angesafiri kumuona mama yake….‘siku hizi na mimi ni mwanakijiji hapa, mama ameolewa hapa na mzee… Alimtaja mzee fulani.

‘Sasa mzee lete habari maana ngalambe zetu mjini tunazijua wenyewe…'Alianza kusema na nilianza kuhisi hatari ikija.

Halafu aliendelea… ‘Wazee huyu ni jamaa yangu kabisa. Wiki iliyopita tu tulikuwa tunakabiliana na mama mwenye nyumba tunayoishi. Tumepewa notisi kuhama kwenye ghetto yetu, si mnajua maisha ya Bongo yalivyo, mtu sita chumba kimoja, mambo magumu washkaji msije mjini…'

Kila nikimzuia asizungumze, naona mwenzangu anachanja mbuga tu kutoa siri za maisha yetu ya Dar. Mwisho wake wapambe wangu wakaanza kuhoji kuhusu anachosema yule jamaa. Jamaa naye bila ajizi aliendelea kusema ukweli kuhusu maisha yetu mjini. Nilipoona vile kwa sababu namjua kuwa ni mgomvi, niliona bora niondoke badala ya kubishana naye.

Kwa kweli kesho yake nikakuta taarifa zile zimeenea kijiji kizima kwamba, huko Dar niliko nabangaiza tu na sina maduka ya spea za magari wala nini. Ilibidi niondoke siku hiyo hiyo na kwenda kulala kijiji kingine cha jirani na kusafiri siku iliyofuata kurudi Dar.
Lakini nashukuru, jamaa alinisaidia. Kwani baada ya pale niliamua kuwa mkweli. Leo hii hata hivyo maisha yangu yamebadilika na yamekuwa mazuri kiasi cha kutosha. Lakini siku zote nakuwa mkweli sitaki kupanda zaidi ya nilivyo katika hali halisi….
 
Yaani katika watu waJF ambao naweza kutoa chochote ili niwaone ni wewe, yaani huwa nashindwa kukuimagine. Hauna nafasi ya muhudumu kwenye Mtambuzi pub?

Vimini ndio nguo nizipendazo, hivyo usihofu kuhusu qualification. LOL
 
Ndugu yangu Mtambuzi a.k.a mzee wa Ununio naona umeibuka tena kutokea Temeke mikoroshini....lol
Kiukweli uongo ni uongo tu na hata uupambe vipi kuna siku unaumbuka mtu mzima..Inatokea hata katika ya maisha mapenzi watu wanaingia na gia za udanganyifu wanasahau yatakapobumbuluka wanakosa mwana na maji ya moto...
My take: Always be yourself!!
 
Last edited by a moderator:
Umu wapo wengi wanaohitaji kubadirika-Ukweli mda mwengine una saidia

Mda mwengine inabidi tuwe kama tulivyo
 
Yaani katika watu waJF ambao naweza kutoa chochote ili niwaone ni wewe, yaani huwa nashindwa kukuimagine. Hauna nafasi ya muhudumu kwenye Mtambuzi pub?

Vimini ndio nguo nizipendazo, hivyo usihofu kuhusu qualification. LOL

Ha ha ha ha ha haaaaaa Kaunga bwana....
Mimi ni Invisible kwa hiyo siku ukimuona Invisible ujue umemuona Mzee Mtambuzi..... LOL
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaa! Mtaaaaa! Kimjinimjini mtu unamiliki Black Berry, I phone 4s, I pad na vingine  vya kuuzia sura ila unakoishi ambako umepanga ni USWAAAAAA ile mbayaaaa! Watu mujini hatukaribishani majumbani, kitu BAR bwanaa hadi utokee MSIBA! Mashauzi yana Gharama Sana!!!!!! Unakuta jitu lina 27 bado lipo home kwa wazee kula kulaa na kazi anayo!
 
Ndugu yangu Mtambuzi a.k.a mzee wa Ununio naona umeibuka tena kutokea Temeke mikoroshini....lol
Kiukweli uongo ni uongo tu na hata uupambe vipi kuna siku unaumbuka mtu mzima..Inatokea hata katika ya maisha mapenzi watu wanaingia na gia za udanganyifu wanasahau yatakapobumbuluka wanakosa mwana na maji ya moto...
My take: Always be yourself!!
Mkuu SnowBall unayosema ni kweli, lakini kwa wadada wa siku hizi nao ukiwa mkweli sana unakuwa husomeki, inashauriwa uwe na kauwongo kidogo ili ku-lubricate mazingira ya kukubaliwa, la sivyo utaisoma namba, ila ni vyema ukilamba mzigo ndio useme ukweli lakini uwe makini usije ukamwagiwa tindikali, mabinti wa siku hizi wamepinda ile mbaya....LOL
 
Mtambuzi sikatai ni kweli kabisa..kwa faida za muda mfupi uongo unaweza kulipa..meaning kwamba unaweza kupata unachokitaka..but in a long run inaweza kukucost vibaya braza.....Nakumbuka once a time niliwahi kumdanganya mtu flani hivi kwamba nina gari na kweli alikuwa ananiona nadrive..siku ilivokuja kubackfire na kugundulika kuwa lile gari ni la mshkaji na mimi sina hata baiskeli..nilitamani kuwa mdogo kama piriton aisee..Kifupi uongo au show up sio nzuri!!....
 
Last edited by a moderator:
Mbinu kama hizo huwa tunazitumia kwenye short term mission hasa kwa watu ambao ukiwaambia ukweli hawataki.
 
Mtambuzi sikatai ni kweli kabisa..kwa faida za muda mfupi uongo unaweza kulipa..meaning kwamba unaweza kupata unachokitaka..but in a long run inaweza kukucost vibaya braza.....Nakumbuka once a time niliwahi kumdanganya mtu flani hivi kwamba nina gari na kweli alikuwa ananiona nadrive..siku ilivokuja kubackfire na kugundulika kuwa lile gari ni la mshkaji na mimi sina hata baiskeli..nilitamani kuwa mdogo kama piriton aisee..Kifupi uongo au show up sio nzuri!!....

Kuanzia leo itabidi nianze kusema kwamba hili gari ninaloendesha sio lakwangu ni la Muhindi tajiri yangu, kumbe huwa ina backfire eh...! Ahsante kwa kunipa maujanja...LOL
 
Huwa natamani haya mafunzo yangekuwa yanawafikia wale wanaopenda kijitutumua, nimeshuhudia jambo kama hili wiki mbili zimepita japo mhusika hakuumbuka. Jamaa namfahamu ni mhudumu wa mgahawa mmoja ambao mara nyingi huwa nafika hapo, sasa cku moja nikamwona yupo ktk mji mwingine tofauti na huo anaofanyia kazi maongezi yake, tembea yake, vaa n.k vililenga aonekane km m2 fulani alienazo. Hapo alipokuwa anajitutumua ni kwenye bar na bila shaka alikuwa anamtega binti mmoja aliponiona niliona uso wa wasiwasi na mimi nikampotezea tu.

Mi nafikiri ni bora ukawa wewe(jinsi ulivyo) katika mazingira yoyote ili uwe na amani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom