Mshitakiwa

Mshitakiwa

Kuna kitu hapa sikielewi.

Kama Aboud Jumbe alijiuzulu mwaka 1984 na JK Nyerere aliacha Urais mwaka 1985, ilikuwaje Maalim Seif aibe faili Ikulu kwa Nyerere na kulipeleka Butiama ambako ni kijijini kwoa Nyerere. Kwa nini Nyerere asiagize tu walilete hilo faili?

Au kuna mtu kaelewa zaidi anifafanulie nyie GT?

Ikulu unayozungumzwa hapo ni Ikulu ya mnazi mmoja Zanzibar sio Magogoni Dar.
 
Rais wakati huo alikuwa nani wengine ndo tunajifunza history humu

Huyu bana ni Aboud Jumbe, huyu jamaa nataka kweli kujuwa habari zake, unajuwa huyu jamaa anashikiliwa mateka huko Tanganyika mpaka leo, nasikia haoni na ni mzee sana.
Huyu ndo chanzo cha jina la kijiji kimoja huko Tanganyika, eneo la Kigamboni kinaitwa MJI MWEMA.
Kijiji kiliitwa mjimwema sababu ilikuwa full ulinzi. Hamna cha kibaka wala nini!
Sijawahi kumwona tena katika picha wala sherehe za muungano tangu alipokamatwa mateka

Huyu ndo aliyekuwa rais wa awamu ya pili Zanzibar.

Nafikiri hata sura yake vijana wengi wa JF hawaijuwi.
Nahisi huyu akiwekwa hadharani atatuachia wosia Mzuri sana kuhusu Muungano.
 
Ikulu unayozungumzwa hapo ni Ikulu ya mnazi mmoja Zanzibar sio Magogoni Dar.

Huyu Sikonge sjuwi vipi!
Hapa tukiamua kuijadili hii ishu ya Jumbe nape atajuta kwanini karopoka anadhani kamkomoa Maalimu, hajuwi
ishu ya Jumbe ndo jini linaloitafuna nyinyiemu.
Wamemweka Mzee wa watu mateka miaka dahali!
 
(makala hii imeandikwa na Dr. Mohammed Seif Khatibu)

MWAKA 1984, mkoani Dodoma ndani ya ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulikuwepo kesi kubwa. Kesi ya kiongozi wa juu wa serikali ya Zanzibar. Alishitakiwa kwa kosa la kwenda kinyume cha Òhati za MuunganoÓ uliosainiwa na Abeid Amani Karume na Julius Nyerere.

Mtuhumiwa, Rais wa Zanzibar, hakuwahi kujiandaa vyema na kufikisha hoja yake mbele ya mamlaka ya Chama chake. Marafiki zake wa karibu walimuendea kinyume na kuiba waraka muhimu wa mashitaka katika shubaka la Ikulu.

Bila shaka wale waliohusika walifanya wizi huu kwa siri kubwa kwani waraka wenyewe uliibiwa na kutolewa nakala na kurejeshwa ulipochukuliwa bila wahusika kujulikana. Waraka huo ukapelekwa Butiama kwa Mwalimu kwa ndege ya kukodi.

Njama hizo za kumwangamiza na kumtosa kiongozi huyo wa Zanzibar katika majanga ilikuwa ajali kubwa ya kisiasa na ya kihistoria kutokea katika taifa letu. Mipango ikapangwa kesi ikadhihirishwa katika kikao cha Chama na kuwa kama mahakama. Mshitakiwa ni Rais wa Zanzibar. Akasomewa mashitaka yake yote mbele ya viongozi wenzake katika ukumbi wa Chuo cha CBE huko Dodoma.

Mwendesha mashitaka dhidi ya Rais wa Zanzibar alijitokeza kwa haraka na kuona kama vile amepata bahati ya pekee. Sio mwingine ila alikuwa Maalim Seif. Akasimama kidete mbele ya hadhara na kuelezea kwa nini kiongozi huyo wa Zanzibar amefanya kosa na dhambi kubwa ya kutaka kuubadilisha muundo wa Muungano badala ya kuwa wa serikali mbili alitaka uwe wa serikali tatu kinyume na sera za Chama.

Mwendesha mashitaka huyu kwa jasiri alijenga hoja zake za kutosha za kuonesha uzuri wa Muungano, tija ya Muungano wa Serikali mbili na kwa nini kiongozi huyo wa juu wa Zanzibar inapaswa achukuliwe hatua kali sana bila huruma!

Mwendesha mashitaka huyo akaungwa mkono sana na wafuasi wake akiwamo marehemu Shaaban Mloo. Mwendesha mashitaka huyo baadaye ikaonekana kuwa yeye ndiye aliyehusika mapema kuiba waraka huo katika shubaka au suraka ya huko Ikulu.
Hivyo, basi alifanya kazi mbili za kuiba waraka na kumkabidhi Nyerere na kusimama kama mwendesha mashitaka namba moja dhidi ya Rais wake huyo. Mshitakiwa, Rais wa Zanzibar, kwa unyonge alikubali adhabu ya kujiuzulu kwa nafasi zake zote tatu. urais wa Zanzibar, makamu wa rais wa Tanzania na umakamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

Hakuruhusiwa kuishi Zanzibar. Viongozi wenzake wa karibu, wote wakafuata nyayo zake za kujiuzulu akiwemo waziri kiongozi wake. Viongozi wake waandamizi wakawekwa katika vifungo vya nyumbani katika mikoa kadhaa ya Tanzania Bara.

Matokeo yote hayo, mabaya kwa Rais wa Zanzibar na wenzake ni kazi ÒnzuriÓ ya kuiba nyaraka Ikulu na kusimamia kidete Mwendesha Mashitaka huyu stadi, bingwa, mahiri na jasiri - Maalim Seif. Ni bahati mbaya kuwa mwendesha mashitaka huyo ni mwanafunzi wa mshitakiwa katika Chuo cha Lumumba.

Pia ni bahati mbaya mwendesha mashitaka alipewa nafasi ya masomo ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mshitakiwa. Ni bahati mbaya mwendesha mashitaka huyu alipewa kazi serikalini baada ya masomo na kumwingiza katika siasa na yeye mshitakiwa pia hata kufika nafasi aliyonayo sasa.

Hiyo ndio fadhila yake? Hiyo ndio ahsante yake? Ni bahati mbaya kuwa mwendesha mashitaka hivi sasa hayupo kizimbani kwa kutenda kosa na dhambi ileile aliyoifanya Rais wa Zanzibar aliyejiuzulu.

Mwendesha mashitaka huyu aliyetetea Muungano wa serikali mbili kwa uchungu na hoja, leo amegeuka. Huyo ndiye leo anaongea hadharani kuwa sio tu anakataa serikali mbili bali anataka Muungano huo adhimu uliomfikisha leo hapo alipo uvunjwe kabisa.

Yeye kama kiongozi wa juu na mtendaji mkuu wa chama chake anakwenda kinyume pia na sera ya Chama chake ya Muungano wa serikali tatu.

Hivi mwendesha mashitaka huyu wa kesi kama hii kwa nini na yeye asishitakiwe na chama chake? Uadilifu wake uko wapi? Ukweli wake uko wapi? Sheria si msumeno? Unafiki na uzandiki umemtawala. Mwendesha mashitaka ni mshitakiwa, afikishwe kizimbani. Anayo kesi ya kujibu.

We nape kichaaa kabisa!
 
Wote hao ni "system", wanaoneana wivu tu, "kwanini yeye si mimi?".

Kwani hayo huyajui Nape Nnauye?

"Nyani haoni kundule.." yeye naye si mmoja wa walio asisi CCJ huku akiwa bado CCM, je huu nao si unafiki, usaliti na uzandiki usiovumilika? Nape akae akiomba kila siku isije tokea Leigwanani mkuu akachukua uenyekiti wa Chama, atatatamani ardhi ipasuke immeze kuliko kushuhudia litakalo mpata!
 
Duu, sikuwa nimeunganisha Dots hiyo. Thanks Mkuu kwa ufafanuzi ambao ni mfupi ila unaeleweka bila lugha mbovu. Pamoja sana.
Ikulu unayozungumzwa hapo ni Ikulu ya mnazi mmoja Zanzibar sio Magogoni Dar.
 
Kweli Sijui vipi.... Niliandika kuwa sijaelewa na Eddie kanifafanulia, sasa wewe hujui nini?

Ukitaka kujadili, wewe jadili tu mie huko wala simo ila ntakuwa Msomaji wenu.
Huyu Sikonge sjuwi vipi!
Hapa tukiamua kuijadili hii ishu ya Jumbe nape atajuta kwanini karopoka anadhani kamkomoa Maalimu, hajuwi
ishu ya Jumbe ndo jini linaloitafuna nyinyiemu.
Wamemweka Mzee wa watu mateka miaka dahali!
 
Last edited by a moderator:
mnamtesa tuu mzee Aboud Jumbe kwa kifungo cha nyumbani na uroho wa madaraka,kwani kuhoji muungano au sura ya muungano huyu mzee Aboud Jumbe hakua na haki hiyo kama raia wa tanzania???huo ulikua ni ufashisti wa Nyerere
 
Kumbe wee Kinyozi? Ntakuletea Bibi mmoja kutoka Dodoma umnyowe.

Ngoja nijiwahie Mwarabu wangu leo jioni tukajirushe na wimbo wa Salt Shaker...... Wee baki Kinyozi

Umenichekesha sana!

Real JF Nice one!!!!!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
(makala hii imeandikwa na Dr. Mohammed Seif Khatibu)

Pia ni bahati mbaya mwendesha mashitaka alipewa nafasi ya masomo ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mshitakiwa. Ni bahati mbaya mwendesha mashitaka huyu alipewa kazi serikalini baada ya masomo na kumwingiza katika siasa na yeye mshitakiwa pia hata kufika nafasi aliyonayo sasa.

Hiyo ndio fadhila yake? Hiyo ndio ahsante yake? Ni bahati mbaya kuwa mwendesha mashitaka hivi sasa hayupo kizimbani kwa kutenda kosa na dhambi ileile aliyoifanya Rais wa Zanzibar aliyejiuzulu.

Mwendesha mashitaka huyu aliyetetea Muungano wa serikali mbili kwa uchungu na hoja, leo amegeuka. Huyo ndiye leo anaongea hadharani kuwa sio tu anakataa serikali mbili bali anataka Muungano huo adhimu uliomfikisha leo hapo alipo uvunjwe kabisa.

Yeye kama kiongozi wa juu na mtendaji mkuu wa chama chake anakwenda kinyume pia na sera ya Chama chake ya Muungano wa serikali tatu.

Hivi mwendesha mashitaka huyu wa kesi kama hii kwa nini na yeye asishitakiwe na chama chake? Uadilifu wake uko wapi? Ukweli wake uko wapi? Sheria si msumeno? Unafiki na uzandiki umemtawala. Mwendesha mashitaka ni mshitakiwa, afikishwe kizimbani. Anayo kesi ya kujibu.

Ndugu na kiongozi wetu katika chama naomba nishereheshe pia mawazo yangu katika sehemu nilizoweka Red.
1. kupewa nafasi (Yeyote ile) - Kinachofahamika ni kuwa watanzania wengi hupata nafasi mbali mbali kulingana na sifa japo wapo wachache kama unavyodhihirisha katika ujumbe wako huu kwa kuwema kupewa ukiimanisha hawakuwa na sifa bali ilikuwa ni upendeleo. Hii ndio dhana ambayo watanzania tunatakiwa kuipinga na kuitokomeza kwani kama itaendelezwa ni dhahiri kuwa watoto wa viongozi na wenye nafasi pekee ndio watakaonufaika na fursa mbali mbali kwa upendeleo. Japo hili kwa sasa linazidi kuota mizizi ndio maana kuna watoto wengi wanaojadiliwa kila siku kuwa ni wa vigogo na hata wanapofanya vibaya hakuna wa kuwaadhibu.

2. KUlipa fadhila - Ninachojiuliza ni kuwa baada ya kupata ujuzi fulani na kukabidhiwa madaraka, hapo tena hakuna undugu na mtu aliyekupa nafasi hiyo bali ni misingi, sheria na taratibu za kazi ndizo zinazotumika. Ukichukulia hivyo ningeanza kupingana nawe kwa kauli zako kadhaa juu ya wale uliowaambia wavue magamba kama taratibu za chama zilivyohitaji. Lakini ukikumbuka miaka michache tu uliposimama na kugombea cheo fulani, Baada ya kukosa uliahidiwa mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kupewa U-DC na baadae cheo ulichonacho sasa. Kama ungefuata ujomba na ushangazi Usingedhubutu kuwaambia wavue magamba hali ya kuwa moja ya jitihada zao ndio hizo ulizonazo sasa. Japo kuwa hiyo kauli yako sasa imedhihiri ilikuwa ni ya kisiasa na sio kiutendaji ndio maana leo muda uliotolewa na chama umeisha na magamba bado wako tena wanazidi kuwa na nguvu.
Jamani, tuacheni tabia hii ya kulipa fadhila hata pale kiongozi anapopotoka. Kama tunatumia fadhila Sheria na kanuni tuliziweka za nini? Basi kama moja ya kiongozi toa kauli ya kufuta sheria na kanuni zisitubane ili tutekeleze vizuri u-fadhila.

3. aliyetetea muungano na sasa anakwenda kinyume na kanuni za chama - Ni sasa kabisa alichofanya huyo kiongozi. Kwa wakati ule muungano na serikali mbili ndio ilikuwa moto wa chama na serikali. hivyo aliyekwenda kinyume na agizo hilo alikuwa anvunja sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa. Hivyo alipaswa kuchukuliwa hatua. Lakini hakuna kitu kinachodumu milele. Ndio maana tunakuwa na mipango kazi mingi kila mwaka na kuiipitia chini ya miaka 10 utakuta tayari kuna mingine inakinzana. Mfano:- Katika serikail yetu Kuna waziri alifuta michezo mashuleni kitu ambacho leo kimerejeshwa, Kuna waziri aliungangisha baadhi ya msomo na kufuta mengine katika level ya sekondari na leo yamerudishwa kama yalivyokuwa mwanzo, Serikali na Baraza la Mitihani tanzania lilitangaza kubadili muda wa kufanya mitihani ya taifa kwa kidato cha tano na sita (Kidato cha tano toka November kwenda ........., Na A-level toka May kenda February) lakini kwa tangazo la sasa linarudisha muda ule ule uliokuwepo awali, Kuna majengo mengi hata ya serikali yaliyojengwa katika maeneo ambayo kwa leo inaonekana haifai na mengine yanavunja sheria. Hivyo ukiangalia utendaji wa viongozi wetu wale waliotetea mifumo ya mwanzo na wale walioivunja na kuanzisha mipya na leo wamekuja wengine na kuirudisha ile ile ya mwanzo. Unataka kusema pia wote hao wana kesi ya kujibu na wanatakiwa kuadhibiwa?. Ni ukweli usiopingika kuwa kuna wengine wanatakiwa kuchukuliwa hatua na kuna wengine hawastahili kutokana na muundo na jinsi jamii ya sasa inavyotakiwa kuishi (Utandawazi).
Muungano kwa kipindi kile ilikuwa ni hot cake, Lakini kwa sasa nina imani kama CCM itaamua kufanya uwamuzi mgumu wa kuwaruhusu wananchi kutoa maoni yao na yakaheshimiwa naamini muungano unavunjika kwani wananchi wengi hawaoni faida yake wala umuhimu wake kwa sasa. Kiegezo cha kipindi kile sio kiegezo tena sasa ndio maana hata serikali inagwaya kusema kinagaubaga faida na hasara za muungano zaidi ya kuishia kusema una faida lakini hazitajwi.

Ndugu Nape nakuasa kama kiongozi wetu, kwa heshima na taadhima kubwa kuwa.
1. Kumbukeni uongozi ni dhamana ipo siku utastafu / utaachia mdaraka. Jiulize je utaishije na jamii hii?
2. Acheni kuongoza watanzania kwa matwaka yenu binafsi, tumieni njia sahihi za ushirikishwaji wa jamii na heshimuni matakwa na mawazo ya wananchi. Hii itawasaidia ninyi kuwa na "Rapport" nzuri katika jamii na pia kuepusha uvunjifu wa amani usio wa msingi.

3. Tekelezeni miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi na acheni kutekeleza kwa kuzuga "Kutuliza akili za watanzania". Kuna faida gani ya kuwashikilia wawekezaji na kuwaachia wakiondoka na mali za watanzania huku wakiachwa masikini?. Huenda ninyi viongozi wa juu mnanufaika ndio maana ufisadi umekuwa kitu cha kawaida Tanzania na hakuna wa kumchukulia mwenzio hatua na badala yake mnaishi kwa kulindana lindana tu. Pamoja na kuwa na fedha nyingi huko nje ya nchi kwa viongozi bado faida ni ndogo kwani zinawanyima uhuru hata wa kuzitumia. Kuna faida gani kununua Gari yako nzuri kwa kuwa unauwezo lakini unapopita hakuna barabara inayoendana na hadhi ya gari hiyo?, Unakuwa na nyumba nzuri lakini jirani zako wanalala na njaa, Ukiugua mpaka ukimbilie nje ya nchi badala ya kutibiwa hapa nchini, N.k. Tuboreshe maendeleo yetu watanzania yatawasaidia nanyi viongozi.

4. Tukumbuke kuwa hapa duniani binadamu ni kiumbe wa kupita, Mungu ameelekeza mengi sana katika uhai baada ya dunia na kinachotakiwa. Je tujiulizeni ni bora maidha haya ya duniani yenye udhalili na ubanifu wa kushindwa hata kuongea na jirani pia kwa mungu tukiwa hatujaandaa chochote cha kutusaidia?. Hakuna imani ya dini hata moja inayoruhusu kudanganya, kulaghai, kuchukua kisicho chako, kutoutumikia uongozi wako kiuadilifu, kutoa rushwa n.k.

5. Ndugu Nape jitambue na Uwe wa kwanza kuwaongoza watanzania kwa uadilifu na kama huwezi sio vibaya ukakiri na kuachia nafasi hiyo ambayo siku ya mwisho ndio kitakuwa kitu cha kwanza kuulizwa na muumba wako.
 
(makala hii imeandikwa na Dr. Mohammed Seif Khatibu)

MWAKA 1984, mkoani Dodoma ndani ya ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulikuwepo kesi kubwa. Kesi ya kiongozi wa juu wa serikali ya Zanzibar. Alishitakiwa kwa kosa la kwenda kinyume cha Òhati za MuunganoÓ uliosainiwa na Abeid Amani Karume na Julius Nyerere.

Mtuhumiwa, Rais wa Zanzibar, hakuwahi kujiandaa vyema na kufikisha hoja yake mbele ya mamlaka ya Chama chake. Marafiki zake wa karibu walimuendea kinyume na kuiba waraka muhimu wa mashitaka katika shubaka la Ikulu.

Bila shaka wale waliohusika walifanya wizi huu kwa siri kubwa kwani waraka wenyewe uliibiwa na kutolewa nakala na kurejeshwa ulipochukuliwa bila wahusika kujulikana. Waraka huo ukapelekwa Butiama kwa Mwalimu kwa ndege ya kukodi.

Njama hizo za kumwangamiza na kumtosa kiongozi huyo wa Zanzibar katika majanga ilikuwa ajali kubwa ya kisiasa na ya kihistoria kutokea katika taifa letu. Mipango ikapangwa kesi ikadhihirishwa katika kikao cha Chama na kuwa kama mahakama. Mshitakiwa ni Rais wa Zanzibar. Akasomewa mashitaka yake yote mbele ya viongozi wenzake katika ukumbi wa Chuo cha CBE huko Dodoma.

Mwendesha mashitaka dhidi ya Rais wa Zanzibar alijitokeza kwa haraka na kuona kama vile amepata bahati ya pekee. Sio mwingine ila alikuwa Maalim Seif. Akasimama kidete mbele ya hadhara na kuelezea kwa nini kiongozi huyo wa Zanzibar amefanya kosa na dhambi kubwa ya kutaka kuubadilisha muundo wa Muungano badala ya kuwa wa serikali mbili alitaka uwe wa serikali tatu kinyume na sera za Chama.

Mwendesha mashitaka huyu kwa jasiri alijenga hoja zake za kutosha za kuonesha uzuri wa Muungano, tija ya Muungano wa Serikali mbili na kwa nini kiongozi huyo wa juu wa Zanzibar inapaswa achukuliwe hatua kali sana bila huruma!

Mwendesha mashitaka huyo akaungwa mkono sana na wafuasi wake akiwamo marehemu Shaaban Mloo. Mwendesha mashitaka huyo baadaye ikaonekana kuwa yeye ndiye aliyehusika mapema kuiba waraka huo katika shubaka au suraka ya huko Ikulu.
Hivyo, basi alifanya kazi mbili za kuiba waraka na kumkabidhi Nyerere na kusimama kama mwendesha mashitaka namba moja dhidi ya Rais wake huyo. Mshitakiwa, Rais wa Zanzibar, kwa unyonge alikubali adhabu ya kujiuzulu kwa nafasi zake zote tatu. urais wa Zanzibar, makamu wa rais wa Tanzania na umakamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

Hakuruhusiwa kuishi Zanzibar. Viongozi wenzake wa karibu, wote wakafuata nyayo zake za kujiuzulu akiwemo waziri kiongozi wake. Viongozi wake waandamizi wakawekwa katika vifungo vya nyumbani katika mikoa kadhaa ya Tanzania Bara.

Matokeo yote hayo, mabaya kwa Rais wa Zanzibar na wenzake ni kazi ÒnzuriÓ ya kuiba nyaraka Ikulu na kusimamia kidete Mwendesha Mashitaka huyu stadi, bingwa, mahiri na jasiri - Maalim Seif. Ni bahati mbaya kuwa mwendesha mashitaka huyo ni mwanafunzi wa mshitakiwa katika Chuo cha Lumumba.

Pia ni bahati mbaya mwendesha mashitaka alipewa nafasi ya masomo ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mshitakiwa. Ni bahati mbaya mwendesha mashitaka huyu alipewa kazi serikalini baada ya masomo na kumwingiza katika siasa na yeye mshitakiwa pia hata kufika nafasi aliyonayo sasa.

Hiyo ndio fadhila yake? Hiyo ndio ahsante yake? Ni bahati mbaya kuwa mwendesha mashitaka hivi sasa hayupo kizimbani kwa kutenda kosa na dhambi ileile aliyoifanya Rais wa Zanzibar aliyejiuzulu.

Mwendesha mashitaka huyu aliyetetea Muungano wa serikali mbili kwa uchungu na hoja, leo amegeuka. Huyo ndiye leo anaongea hadharani kuwa sio tu anakataa serikali mbili bali anataka Muungano huo adhimu uliomfikisha leo hapo alipo uvunjwe kabisa.

Yeye kama kiongozi wa juu na mtendaji mkuu wa chama chake anakwenda kinyume pia na sera ya Chama chake ya Muungano wa serikali tatu.

Hivi mwendesha mashitaka huyu wa kesi kama hii kwa nini na yeye asishitakiwe na chama chake? Uadilifu wake uko wapi? Ukweli wake uko wapi? Sheria si msumeno? Unafiki na uzandiki umemtawala. Mwendesha mashitaka ni mshitakiwa, afikishwe kizimbani. Anayo kesi ya kujibu.
Umenena Kaka, naikumbuka sana kesi hii
 
Hii inatukumbusha kuwa wanaotaka muungano uvunjike, ama kutaka serikali tatu; ni kwa sababu wanajua nafasi za uongozi zitaongezeka na watakuwa na nafasi ya kufanya madudu yao kwa uhuru bila kukabwa. Maskini wazenj....
 
Asante Mh Nape kwa kuleta maada yenye ukweli na mafundisho kama hii.
 
Back
Top Bottom