Hana tofauti na Yuda Iskarioti, alisema "Yule nitakaye msalimia kwa kumbusu ndiye Yesu mkamateni"
Maalim Seif Sharif Hamad anahasira kwani alitarajia kwamba Mwl angemteua yeye kuwa Rais wa Zanzibar kwa kufanya kazi nzuri ya unafiki. Kumbe principles za Mwl ni kwamba "huyu aliyemsaliti mwenzie leo, kesho atakusaliti wewe"
Umenikumbusha dada mmoja alikuwa anafanya kazi kwenye shirika fulani la wazungu halafu yeye akawa anawapeleleza Watz wenzake na kupeleka taarifa zao kwao. Kweli wale waliopelezwa walifukuzwa kazi lakini na yeye baada ya muda alifukuzwa kwa kuwa ilionekana asingeweza kuwa msaliti kwa Watz wenzake halafu akawa mwanifu sana kwako. ndiyo maana wanasema 'He who gossps to yuou will gossip about you'. Hata kama mtu anakuwa fundi wa kutoa siri za chama fulani kwa kingine kwa kepewa fedha eventually wale wanaopewa zile siri watamtenga kwa kuwa hawatajua ni lini atapewa fedha nyingi zaidi na kusema siri zao. Uaminifu na uadilifu ni bora kuliko usaliti.