Mshitakiwa

Makala imemu expose Seif Shariff vibaya.Inamuonyesha ni mtu kigeugeu na mwenye roho ya usaliti kwa tamaa ya madraka.Na pia imemuonyesha kuwa ni mnafiki na mtu asiyeaminika.
 
Kama ni kauli na vitendo tafauti hebu tuyaanze na kauli zake huyu kijana Nape, ile dhana ya kujivua gamba imefikia wapi? wale aliowanadi ati wezi na mafisadi si ndio hao hao anaokumbatiana nao na kucheka nao..jee yuko credible kuwajadili wengine wakati yeye mwenyewe amekosa standard na werevu wa siasa za kweli, haki na uadilifu. Kuna siku alisisimama Zanzibar na kuwaambia vijana wa CCM kuwashughulikia kwanza wale wote wanaowapinga halafu ndio waachiwe vyombo vya sharia vifanye kazi. Hana uhalali wa kuwasema wengine ikiwa yeye mwenyewe ni hypocrite mkubwa..
 
si unajuwa tena media zetu ni kama hakuna tu?hadi sasa kungetakiwa kuwepo na kipindi ambacho kinazungumzia,hata kwa dk moja tu,kuwa leo ni siku let's say ya mia mbili toka ccm wawape muda magamba ambao ndo wenye nguvu hivi sasa kwenye chama.
 
Nape hivi kuwadharau Watanganyika wezio ni moja ya ufahari kwako ?kwa kipindi kirefu hapa Jf watanganyika au tuseme waTanzania wamekuwa wakikuhoji mambo kadhaa yayotokea ndani ya nchi yanayohusu chama chako na Raia wasio na hatia, lakini umekuwa Du kimnya leo umezuka na (mambo ya Arba fogo wali pesa mbili) ili yale wanyoyataka jaamaa zako kujibiwa usijibu au usiyatolee ufafanuzi ,lakini kumbuka kifo cha nyani kinapofika miti yote huteleza, pia kumbuka watanganyiaka wa leo sio wale waliokuwa wakipelekwa Geza ulole kwenye vijiji vya ujamaa.
 
kumbe ukitulia zina chaji..... Uchambuzi mzuri sana!! Sas kwa kuwa hicho chama ni mshirika wa chama chako kinachotetea muungano si muamrishe chama hicho kimchukulie hatua asiendelee kuwavuruga.
Kumbuka muungano ukivunjika mmeenda na maji maana huko zenji ndo mnakzoa kura......!!!!!
 


Siasa kweli mchezo mchafu! Tangia Blaise Compaore aliposhiriki kumuua Thomas Sankara mimi nikasema siasa basi siitaki! Leo uko hivi kesho uko vile ili mradi upate mamlaka.
 
kwani mkuu wewe hujui Nape Nnauye anatumika na wakati mwingine anaongea tuuu, iko wapi falsafa ya kujivua gamba?? sijui imeishia wapi, kwenye kikao cha CCM mkoa nikiwa mjumbe nimewahi kuuliza bila kupata majibu...

Hizi falsafa huwa zinaenda kama fashen, zinakwenda na kurudi, wala hilo lisikupe shida.

Hilo la kutumika, najuwa kuwa yeye ana ajira pale CCM na ndipo anapopatumikia, au unamaanisha nini?
 
Hawa CCM wanfanya mambo ya ajabu sana....

Kwa nini awe mtuhumiwa leo wakati kosa lilifanyika miaka hiyo ya themanini na jamaa alionekana shujaa?

Why now?
 


haaaa Bora wewe umedadavua
Basi mie nilikuwa najiuliza ni nani huyu?
 
Ukitaka kujua kwamba mleta mada ni mpuuzi, check topic information....
Mleta mada hayumo kuchangia mada yake!
NEPI aaaaah, NAPE bwana!
 
hizo ni zama hizo na mzee nyerere saizi hii ni dunia ingine.....mkajipange tena alafu mrudi hapa na mshtakiwa na mwendasha mashtaka
 

Da form 3 nilikutana na ii kitu..umenikumbusha mbali sana
 
Huyu Maalim Seif kwa Usaliti aliomfanyia mwenzake hafai kabisa kuwa kiongozi Mkubwa, anaweza kuisaliti na kuiuza nchi huyu Bwana..
 
Enyi kizazi cha nyoka, mtu akikubeba sio tiketi ya kumfichia maovu yake, hii ndio inaiua ccm sasa watu wamebebwa na wanaendelea kubebana na kufichiana maovu. Nape Nnauye ulitaka Seif alipe fadhila gani kwa mouvu au atoe asante gani? Ukitetea uovu utaendelea kuwa mtumwa wa uovu Nape.

Nape Nnauye sasa hivi hatuzungumzii sera za chama tunazungumzia katiba ya nchi, unafahamu kwamba katiba ni sheria ya mama, sera za chama haziwezi ku influence mawaza ya mtu juu ya rasimu ya katiba. Kama ndio hivyo tungechukua sera za chako ndio ziwe katiba ya nchi.
 
Last edited by a moderator:
Huyu Maalim Seif kwa Usaliti aliomfanyia mwenzake hafai kabisa kuwa kiongozi Mkubwa, anaweza kuisaliti na kuiuza nchi huyu Bwana..

Kikwete pia kauza nchi kwa obama na mafisadi je atashitakiwa lini?
 
Huyu Maalim Seif kwa Usaliti aliomfanyia mwenzake hafai kabisa kuwa kiongozi Mkubwa, anaweza kuisaliti na kuiuza nchi huyu Bwana..

Hapa Msaliti alikuwa nani Seif au Abood, kwa mtazamo wangu Abood ndio alikuwa anafanya njama za chinichini ili aue muungano na ndio alikuwa msaliti na alistahili kupata adhabu kali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…