Mshikaji wangu alivyotapeliwa na Mnyarwanda pesa ya kununua coaster 2, sasa hivi hana hamu tena

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Mshikaji wangu alivyotapeliwa na kuingizwa chaka na mnyarwanda sahivi hana hamu tena.

Leo nawapa kisa cha mshkaji wangu ambaye kaingizwa chaka na Mnyarwanda.

Mambo yalianza hivi, mungu si athumani mshikaji wangu akachaguliwa kupata kazi fulani hivi,ili kuwaaminisha hata watumishi wenzake kwamba anafanya kazi miezi miwili ya mwanzo kazini alifanya kazi kwa bidii akawa kakusanya vihela vyake ili ajipange maana jamaa aliona mbali.

Ghafla kapata rafiki mpya kutoka Rwanda wakawa mabest kinoma jamaa yetu alikua na mpango wa kununua costa za kubebea abiria ili walau apate kipato.

Aisee mnyarwanda akamshauri jamaa anunue macosta ili aweze kuongeza kipato hayawi hayawi jamaa akanunua costa mbili bila hata kushauriana na sisi ndugu zake, masela zake aka wana.

Basi ubest friend wao na mnyarwanda ukanoga mnyarwanda akamshauri jamaa anunue costa zaidi!lakini nikamuuliza mshkaji kwamba angeacha kwanza hizo mbili kwa kua ndo kaanza kubeba abiria ili aone kama zinaingiza faida au la. Mshkaji akanijibu kuwa hapangiwi.

Akaongeza costa nyingine kwa kumsikiliza huyo rafiki yake mnyarwanda, sasa issue ikaja kuwa kwamba jamaa akaagiza costa nyingine huko nje aisee masuala ya hapa na pale kumbe alikua na kesi fulani hivi na manzi wa kizungu ile costa ikabidi ikamatwe jamaa alihaha sana na ile kesi.

Mambo yakaja kupoa sasa jamaa kuepusha shari mshikaji wa kigali akamwambia atamsaidia kununua costa nyingine mbili kupitia jina lake, yaani atamsaidia jamaa kununua kupitia jina lake huyo mnyarwanda ili zisikamatwe mzigo utatua kigali then atamkabidhi utakuja bongo.

Jamaa akaingia kichwa kichwa akamkabidhi mnyarwanda pesa mamilioni yale ilikua ni hela ya kununua costa mbili mpya.

Aisee mnyarwanda akasepa na mkwanja zikaanza "excuse nyingi" mara kesho mara naenda kununua mara hivi mara vile, mnyarwanda kasepa na hela yote kamtapeli jamaa kibaya zaidi hiyo pesa kumbe alichukua kazini wakaguzi ofisini wanasema pesa hainekani kwa kitabu cha mahesabu na mnyarwanda kasepa na mkwanja wote na hawezi kumdai maana tayari walikabidhiana kisirisiri behind the scene halaf jamaa lenyewe anamwambia jamaa niguse ninuke.

Sahivi mshikaji kanywea kinyama maana hana namna jamaa alituficha sisi washikaji zake kila kitu kumbe kuna kiwanja alinunua arusha maeneo ya Kia kilikua na kokoto nyingi sana huyo rafiki yake mpya kutoka rwanda kaja kang'ang'ania eti apewe kijisehemu alime maana kiwanja kile ni hekari kumi jamaa akampa kama hekari 4, mnyarwanda kakomba kokote zote shambani.

Alitutenga sisi marafiki zake akaamini mtu mwingine kuliko sisi tena akatuita wasaliti tusiomtakia mema na eti tunamuonea wivu, mnyarwanda akadai kwa jamaa kwamba asimuulize ulize ujinga "kwani si nilikupa hadi sungusungu?si nilikupa hadi kundi langu likaja kuwashughulikia wale waliokua wanataka kukunyang'anya tonge lako kazini, jamaa akatoa sababu kibao.

Sahivi mshkaji wetu kanywea kimyama, juzi October 28 ilikua ni birthday yake, sikuhizi hata chalii wa rwanda hata salam hakuna.

Juzi mshkaji namuona kapata rafiki mpya sisi marafiki zake katusahau kabisa hajajifunza kwa chalii wa kigali alomtapeli pesa za costa sahivi kapata rafiki mpya msela flan wa kitaa cha kule Makerere Uganda.Huyo ndo mshkaji wake muda wote wapo pamoja hadi kwenye kubet wanakua pamoja katusahau sisi marafiki zake wa mtaa mmoja.

Wakuu ni juzi tu nimeonana na mama yake alikua analia sana akiva kavaa nguo ya rangi nne, maza analia sana anasema jamaa ni mtoto wake wa tano amezaa sana lakini huyu mtoto wake wa tano ni wa hovyo,ana kiburi toka apate kazi, ana visasi, ni mwizi kazini lakini anajificha kwenye kivuli cha uaminifu kumbe mwizi,ni mnafiki na anajifanya ni mtu wa dini sana, anapenda wenzie wateseke,ana husda,kijicho,wivu,mropokaji tamaa hapendi mwenzie apate ni mzandiki wa kutupwa anapenda kunyenyekewa hadi na mke wake, ni mtesaji na mkatili sana lakini akiwa hadharani hujifanya mwema, mama analia sana aisee,mama yake analia sana jinsi mwanae anavyofanya.

Nilichomwambia mama ni kuwa asilie ipo siku tu mwanae huyo atafunzwa na ulimwengu.

#HITIMISHO
 
Niliposoma mwanzoni nikaanza muona jamaa mbona fala anafurahia rafiki yake kupigwa, halafu anataka aambiwe kila kitu kwani yeye mkewe.

Ila nilipofika kwenye shamba arusha na kokoto nikajua anajaribu kuzungumzia kitu kingine kabisa wala siyo rafiki yake wala nini.
Ila najaribu kuunga dots kuhusu anayozungumza sijapata fununu ya kagame kumpiga magu. Over
 
Niliposoma mwanzoni nikaanza muona jamaa mbona fala anafurahia rafiki yake kupigwa, halafu anataka aambiwe kila kitu kwani yeye mkewe.
Ila nilipofika kwenye shamba arusha na kokoto nikajua anajaribu kuzungumzia kitu kingine kabisa wala siyo rafiki yake wala nini.
Ila najaribu kuunga dots kuhusu anayozungumza sijapata fununu ya kagame kumpiga magu. over
Bombardier nasikia tulipigwa mkwanja mrefu na Kagame.
 
Daaah Tunashukuru leo kinachodaiwa "Utawala Dhalimu Wa Israel" hakijatajwa kwney uzi wa Kimsboy Mwanapropaganda Wa Ki-Shia kwa Upande wa Afrika Mashariki.
 
Niliposoma mwanzoni nikaanza muona jamaa mbona fala anafurahia rafiki yake kupigwa, halafu anataka aambiwe kila kitu kwani yeye mkewe.
Ila nilipofika kwenye shamba arusha na kokoto nikajua anajaribu kuzungumzia kitu kingine kabisa wala siyo rafiki yake wala nini.
Ila najaribu kuunga dots kuhusu anayozungumza sijapata fununu ya kagame kumpiga magu. over
Wabongo kuombeana dua mbaya ndo zetu. Haya umepata faida gani.
Inasemekana kuwa Kagame kampiga jamaa Tanzanite kupitia wslinzi aliomwazima
 
Back
Top Bottom