hujakosea wala sijakosea. Hao wanaoingiza 6,000 au pungufu unadhani hawatoi vitu kwa wapi wapenzi wao? kama sichanganyi madesa sijui ni kwenye post hii au ipi lakini leo nimesema swala ni kupata mwenzi anayeridhika na unachompa. KUTOA ni kupenda na kupenda ni kutoa. Kama mtu anaona 6,000 ni kubwa kwa saluni dawa si kulalamika au kumwambia mtu asiende saluni, bali kutafuta anayeenda saluni ya 500 au anayependa kupewa vitu vingine ambavyo si hela au visivyohitaji hela au ajiongeze kuboresha kipato.
Kila mtu anastahili kupenda na kupendwa ndiyo. Manake ni kuwa kila mtu anastahili kutoa na kupokea kama Baba yetu alivyotupenda hata akamtoa mwanawe wa pekee kwa ajili yetu. Na sisi tunatakiwa kumpenda kwa kumrudishia utukufu, heshima, sifa, na shukrani. Hapo kwenye shukrani si shukrani za mdomo tu. Acha uanaharakati kwenye malavidavi. Mkono mtupu haulambwi na pesa ni sabuni ya roho, alisema hata Sulemani.