aachane na mapenzi mpaka atakapokuwa tayari kiakili na kiuchumi. Na kama 6,000 ni nyingi ina maana yuko daraja la chini la kijamii na kiuchumi. Atumie muda wake kujikwamua badala ya kutaka kuzuia mafuriko kwa mkono. Hata mpenzi asipoomba hela ya saluni mapenzi ya mjini bado yanahitaji hela. Sasa wanakutana wapi? kwenye viambaza au chini ya miti? Acheni kulialia bana tafuteni hela. Tatizo wengine wanakulia kwenye zile jamii ambazo ukishabalehe na kuweza kununua kitanda tu unakuwa umefaa kuoa. Unakuta nyumba ina baba, mama, wana, wakamwana na wajukuu. Chai wanakunywa saa 6, usiku wanakula kijipane cha samaki na ugali......... ni shida.