HUYO NI DAKTARI AU NURSE....JAMANI SERIKALI IACHE UTANI.
Supervisor wa hoteli, mwenye elimu ya kidato cha sita au Co-ordinator analipwa zaidi ya hiyo hela 750,000/=-1,500,000/= kwa mwezi, analipwa malipo ya huduma (service charge), hii ni kutegemeana na uzo au pato la mwezi la kampuni husika na asilimia walizokubaliana.
Anasaidiwa kupata mkopo tena usiozidi riba ya 22%.
Anapewa chakula, usafiri, hata kama matibabu ni kupitia BIMA ya afya, bado huyu mtu ana amani na kazi yake. Anapatiwa usafiri wa kwenda na kurudi nyumbani pindi awapo kazini. Analipwa malipo ya ziada (Over time).
Mwajiri anachangia katika akaunti yake ya malipo ya uzeeni, hata kama atayachukua kabla ya huo uzee. 10% mwajiri, 10%yeye=20% inaingia katika mfuko wa pensheni. (eg PPF, LAPF,NSSF etc).
Hainiingii akilini kabisa kusikia Daktari...jamani si mmesema Daktari aliyesomea kazi yake(simaanishi hawa wauguzi wa kawaida) Huyu Dr awe na shahada ya uzamili (Masters) au uzamivu (Ph.D) yaani 900,000/=? sikufanikiwa kusikiliza hotuba ya Mhe.Rais lakini nitaipata hard copy yake, nitumieni jamani wapendwa.
Swali kwa wenye weledi wa mifuko ya pesheni......Je kuna riba yeyote au nyongeza kwenye hayo makato pindi wanapostaafu?
Namkumbuka mzee wangu Festus Mogae Aliyekuwa rais wa Botswana), yule mwanaharakati wa masuala ya ukimwi, pamoja na Jerry Rowlings ( Rais wa zamani wa Ghana)hawa wote waliboresha malipo na maslahi katika nyanja hizi ( Hospitals, madaktari wanalipwa hela ya kutosha, Ma-Engineers, na Walimu bila kujali)utaratibu huo haujabadilika bado uko palepale.
Kwanini rais asijifunze kwa John Atta Mills wa Ghana leo? au Rafiki yake Ian Khama Seretse Khama wa Botswana leo?
"BADO SIPATI PICHA" :A S-confused1: